Meya wa CCM abwaga manyanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya wa CCM abwaga manyanga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Jan 31, 2011.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HUYU MEYA AMESOMA ALAMA ZA NYAKATI AKAONA ANAPWAYA

  MEYA wa Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Samweli Kisabwiti kupitia CCM ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, zikiwa zimepita siku 45 tu tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo.

  Hatua ya hiyo ya Meya Kisabwiti imekuja siku chache tangu naibu meya wa jiji la Arusha, Michael Kivuyo kujiuzulu wadhifa wake kufuatia mchafuko yaliyosababisha damu kumwagika wakati polisi waluipopambana na waandamanaji wa Chadema.

  Kwa upande wake Kisabwiti alijiuzulu kwa kile kinachosemekana ni ubatili wa matokeo ya kura yaliyofanyika mjini hapo Desemba 18, mwezi uliopita.

  Alisema amechukua fursa hiyo kulinda heshima yake binafsi na ya chama chake, baada ya kuandamwa kuwa ana elimu duni.

  Meya Kisabwiti amedumu kwenye nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na nusu tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo Desemba 17, mwaka jana ambapo alikuwa mgombea pekee baada ya mgombea wa Chadema kujitoa.

  Alishinda kwa kupigiwa kura za ndiyo na hapana, ambapo kura 12 zilimkubali na kura 9 kumkataa. Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya madiwani 21 kati ya hao 16 ni wa CCM, wanne wa Chadema na mmoja ni diwani kupitia tiketi ya DP. Hii inamaanisha kwamba miongoni mwa waliopiga kura za hapana ni madiwani wa CCM.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake mjini Sumbawanga, alisema amefikia uamuzi huo baada ya kung'amua kwamba uongozi katika nafasi kubwa kama meya ni kitu muhimu sana katika kufanya kazi kwa ufanisi na hivyo anahitaji muda wa kutosha ili aweze kujifunza.

  "Kwahiyo nimeona nipate muda wa kujifunza na kupata uzoefu kupitia nafasi yangu ya udiwani wa kata ya Katandala na kupitia vikao mbalimbali hivyo basi nivema nikaachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine wenye uzoefu kwani nafasi hiyo ni nyeti sana na inahitaji uzoefu na elimu ya kutosha,''alisema.

  Kwa mujibu wa Meya huyo alisema tayari amekwishamuandikia barua mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kumueleza uamuzi wake wa kujiuzulu na kwamba ofisi ya Mkurugenzi imepokea barua hiyo rasmi Januari 28 mwaka huu.

  Aliongeza kusema kuwa pia amepeleleka nakala ya barua hiyo kwa taarifa kwa Katibu wa CCM wa Taifa, Katibu wa CCM wa mkoa wa Rukwa na katibu wa CCM wa wilaya ya Sumbawanga.

  Alisema amefikia uamuzi huo kwa hiari yake mwenyewe bila kupata shinikizo lolote kutoka sehemu yeyote ile isipokuwa aliendela kusisitiza kuwa amefanya hivyo kwa kuendelea kulinda heshima yake binafsi na chama chake kutokan na maneno mengi yaliyozagaa mjini Sumbawanga kwamba hana sifa ya kuwa kiongozi wa siasa.

  Alisema awali alipopata nafasi ya udiwani alikubalika lakini baada ya kugombea na kushinda nafasi ya umeya wa Manispaa hiyo ndipo yalipoanza kuibuka maneno na tuhuma mbalimbali kwamba yeye hana elimu ya kutosha ya kumwezesha kushika nafasi hiyo nyeti.

  Meya huyo alisema kutokana na maneno yaliyozagaa mjini hapa yeye binafsi siyo rahisi kuendelea kuliongoza baraza la madiwani ambalo nalo kuna baadhi ya madiwani hawamkubali na kumwona kuwa ana haja ya kusoma na hivyo wanaona ni bora aachie ngazi hiyo ili apatikane msomi wa kuwaongoza tofauti na yeye ambaye ana elimu ya shule ya msingi darasa la saba.

  "Awali ya yote kusudio langu kubwa lilikuwa kujiuzulu kuanzia nafasi ya udiwani hadi umeya lakini rafiki zangu wa karibu na wanachama wa chama changu walinisihi nijiuzulu nafasi ya umeya kwani kama ningejiuzulu na udiwani ingelazimu uchaguzi mdogo ufanyike kitendo ambacho huenda CCM ingeipoteza kata hiyo,"alisisistiza.

  Akifafanua alisema "Pamoja na kuandika barua ya kujiuzulu endapo chama changu kikisita kunikubalia siwezi kubadili uamuzi huu nilioufikia wa kujiuzulu nafasi hiyo,"alisema.

  Alieleza kuwa changamoto alizozipata kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu akiwa meya ni pamoja na kukosa usingizi na kwamba hata biashara zake zimedorora kwa kiasi cha kutisha.

  Meya huyo ambaye anamiliki maduka kadhaa ya nyama mjini, hapa alikiri kuwa nafasi hiyo sio tu ni nyeti bali pia ni dhahabu kwamba kama angekuwa hana pengine pa kushikia asingeweza kuthubutu kujiuzulu.

  Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Sumbawanga mjini Charles Kabanga alipohojiwa alidai kuwa yeye binafsi kama ofisi hawajazipata rasmi taarifa yake hiyo ya kujiuzulu lakini alisema Meya huyo ana hiari ya kufanya hivyo na iwapo itatokea basi chama CCM kitafuata taratibu na atapatikana Meya mwingine kuziba pengo hilo .

  Aliongeza kuwa kujiuzulu kwa Meya huyo hakutakiathiri chama chao kisiasa kwa sababu kama kiongozi anaona nafasi imemshinda au ameshindwa kuimudu ni bora awajibike ili kutoa fursa kwa wengine wenye uwezo kuliko kuendelea na hatimaye kuharibu.

  SOURCE: Gazeti la Mwananchi
  Gaudensia Lyimo aige mfano hapo.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Muungwana ni vitendo, safi sana
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hana namna lazima na yeye ajiuzulu
   
 4. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Good,kumbe hata wa darasa la 7 wanaweza kusikia vilio vya wananchi wao wakang'atuka. Kwaio kiongozi wao mkuu ni ubishi tu, au mbumbumbu
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bado Meya wa CCM Arusha na maeneo mengine mengi kulikofanyika Uchakachuaji.

  Lakini wasijiuzulu wote maana bado tungependa kukiona chama hiki CCM kama chama cha upinzani chenye nguvu ili kutupa changamoto ya kuchapa kazi zaidi baada ya People's Power kushika hatamu kipindi kifupi kijacho.
   
 6. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui yule meya wa geita (darasa 7)anasubiri nn?angefata busara hizo nae aende kwenye biashara zake
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Hata mbunge wa CCM Sumbawanga Mjini (darasa la 7) anatakiwa ajifunze kutoka kwa Meya huyu. Yule wa CHADEMA asingejitoa angepata kura zote za CCM, sasa naye amechakachuliwa na mbunge!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Muungwana ni Vitendo, Jakaya hajayaona haya!
   
 9. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kusoma alama za nyakati kuliko kusubiri kuondolewa kwa aibu.
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Huyu wa Arusha yupo yupo tu mafichoni kwake, kazi hafanyi , wala nini.Sijui ataendelea kukaa hivyo kwa muda gani. Hana uhuru wa kutembea jijini kwake na akijitokeza tu vijana wanajitokeza ghafla .... MEYA WA KICHINA HUYOOO>>>>>>>>>>> aibu tupu .
   
 11. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Meya huyu shujaa maana viongozi wengine ni wagumu kujiuzulu mpaka wangolewe kwa nguvu. Mimi nampongeza naye namuita the greatthinker
   
 12. babaT

  babaT Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  busara imetumika
   
 13. w

  whale New Member

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hata yule mbuge wa Jimbo la Nyagwale-Geita ni darasa la 7. ni mfanyabiashara wa bajaji kariakoo
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Meya CCM abwanga manyanga
  Sunday, 30 January 2011 21:22

  Mussa Mwangoka, Sumbawanga

  MEYA wa Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Samweli Kisabwiti kupitia CCM ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, zikiwa zimepita siku 45 tu tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo.

  Hatua ya hiyo ya Meya Kisabwiti imekuja siku chache tangu naibu meya wa jiji la Arusha, Michael Kivuyo kujiuzulu wadhifa wake kufuatia mchafuko yaliyosababisha damu kumwagika wakati polisi waluipopambana na waandamanaji wa Chadema.

  Kwa upande wake Kisabwiti alijiuzulu kwa kile kinachosemekana ni ubatili wa matokeo ya kura yaliyofanyika mjini hapo Desemba 18, mwezi uliopita.

  Alisema amechukua fursa hiyo kulinda heshima yake binafsi na ya chama chake, baada ya kuandamwa kuwa ana elimu duni.

  Meya Kisabwiti amedumu kwenye nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na nusu tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo Desemba 17, mwaka jana ambapo alikuwa mgombea pekee baada ya mgombea wa Chadema kujitoa.

  Alishinda kwa kupigiwa kura za ndiyo na hapana, ambapo kura 12 zilimkubali na kura 9 kumkataa. Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya madiwani 21 kati ya hao 16 ni wa CCM, wanne wa Chadema na mmoja ni diwani kupitia tiketi ya DP. Hii inamaanisha kwamba miongoni mwa waliopiga kura za hapana ni madiwani wa CCM.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake mjini Sumbawanga, alisema amefikia uamuzi huo baada ya kung’amua kwamba uongozi katika nafasi kubwa kama meya ni kitu muhimu sana katika kufanya kazi kwa ufanisi na hivyo anahitaji muda wa kutosha ili aweze kujifunza.

  "Kwahiyo nimeona nipate muda wa kujifunza na kupata uzoefu kupitia nafasi yangu ya udiwani wa kata ya Katandala na kupitia vikao mbalimbali hivyo basi nivema nikaachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine wenye uzoefu kwani nafasi hiyo ni nyeti sana na inahitaji uzoefu na elimu ya kutosha,’’alisema.

  Kwa mujibu wa Meya huyo alisema tayari amekwishamuandikia barua mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kumueleza uamuzi wake wa kujiuzulu na kwamba ofisi ya Mkurugenzi imepokea barua hiyo rasmi Januari 28 mwaka huu.

  Aliongeza kusema kuwa pia amepeleleka nakala ya barua hiyo kwa taarifa kwa Katibu wa CCM wa Taifa, Katibu wa CCM wa mkoa wa Rukwa na katibu wa CCM wa wilaya ya Sumbawanga.

  Alisema amefikia uamuzi huo kwa hiari yake mwenyewe bila kupata shinikizo lolote kutoka sehemu yeyote ile isipokuwa aliendela kusisitiza kuwa amefanya hivyo kwa kuendelea kulinda heshima yake binafsi na chama chake kutokan na maneno mengi yaliyozagaa mjini Sumbawanga kwamba hana sifa ya kuwa kiongozi wa siasa.

  Alisema awali alipopata nafasi ya udiwani alikubalika lakini baada ya kugombea na kushinda nafasi ya umeya wa Manispaa hiyo ndipo yalipoanza kuibuka maneno na tuhuma mbalimbali kwamba yeye hana elimu ya kutosha ya kumwezesha kushika nafasi hiyo nyeti.

  Meya huyo alisema kutokana na maneno yaliyozagaa mjini hapa yeye binafsi siyo rahisi kuendelea kuliongoza baraza la madiwani ambalo nalo kuna baadhi ya madiwani hawamkubali na kumwona kuwa ana haja ya kusoma na hivyo wanaona ni bora aachie ngazi hiyo ili apatikane msomi wa kuwaongoza tofauti na yeye ambaye ana elimu ya shule ya msingi darasa la saba.

  “Awali ya yote kusudio langu kubwa lilikuwa kujiuzulu kuanzia nafasi ya udiwani hadi umeya lakini rafiki zangu wa karibu na wanachama wa chama changu walinisihi nijiuzulu nafasi ya umeya kwani kama ningejiuzulu na udiwani ingelazimu uchaguzi mdogo ufanyike kitendo ambacho huenda CCM ingeipoteza kata hiyo,"alisisistiza.

  Akifafanua alisema "Pamoja na kuandika barua ya kujiuzulu endapo chama changu kikisita kunikubalia siwezi kubadili uamuzi huu nilioufikia wa kujiuzulu nafasi hiyo,”alisema.
  Alieleza kuwa changamoto alizozipata kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu akiwa meya ni pamoja na kukosa usingizi na kwamba hata biashara zake zimedorora kwa kiasi cha kutisha.

  Meya huyo ambaye anamiliki maduka kadhaa ya nyama mjini, hapa alikiri kuwa nafasi hiyo sio tu ni nyeti bali pia ni dhahabu kwamba kama angekuwa hana pengine pa kushikia asingeweza kuthubutu kujiuzulu.

  Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Sumbawanga mjini Charles Kabanga alipohojiwa alidai kuwa yeye binafsi kama ofisi hawajazipata rasmi taarifa yake hiyo ya kujiuzulu lakini alisema Meya huyo ana hiari ya kufanya hivyo na iwapo itatokea basi chama CCM kitafuata taratibu na atapatikana Meya mwingine kuziba pengo hilo .

  Aliongeza kuwa kujiuzulu kwa Meya huyo hakutakiathiri chama chao kisiasa kwa sababu kama kiongozi anaona nafasi imemshinda au ameshindwa kuimudu ni bora awajibike ili kutoa fursa kwa wengine wenye uwezo kuliko kuendelea na hatimaye kuharibu.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Alisema amechukua fursa hiyo kulinda heshima yake binafsi na ya chama chakebaada ya kuandamwa kuwa ana elimu duni.
   
  Meya Kisabwiti amedumu kwenye nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na nusu tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo Desemba 17mwaka jana ambapo alikuwa mgombea pekee baada ya mgombea wa Chadema kujitoa.
  Kumbe nchi hii tusikate tamaa kabisa kwa sababu maadili hayajapotea kabisa...........................Ukiona mtu mzima anaachia mkate mzima wa Umeya kulinda heshima yake kwa kukiri hana sifa ujue...............even our corrupt leaders in the ccm SHINDIG CAN REFORM.........................
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Mkuu wa nchi anatakiwa atambue kuwa wenzake wanaanza kusoma alama za nyakati.Serikali ya CCM haina muda itaanguka
   
 17. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Uamuzi wa busara na kinachofuata ni kurudisha ikadi ya ccm ili ajiunge ktk harakati za kuimboa nchi yetu haraka, tunamuhitaji
   
 18. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anajua maana ya dhamana na uwajibikaji, hataki kuwa sehemu ya uozo kama wakuu wake, Big Up ndugu
   
Loading...