Meya wa Arusha amtaka Mrisho Gambo amuombe msamaha ndani ya siku 7

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,662
2,000
MEYA ARUSHA AMJIA JUU RC GAMBO, ATAKA AOMBWE RADHI

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Ijumaa, Lazaro amesema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom