PreGE2025 Meya Songea: Miaka minne bilioni 188 zatumika miradi ya maendeleo Songea

PreGE2025 Meya Songea: Miaka minne bilioni 188 zatumika miradi ya maendeleo Songea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan manispaa ya Songea iliyopo mkoani Ruvuma imenufaika kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi bilioni 188 katika kata 21 zinazounda manispaa hiyo.

Akieleza utekekezaji wa miradi hiyo mstahiki meya wa manispaa ya Songea Michael Mbano amesema katika sekta ya afya serikali ya awamu ya sita imehakilisha wananchi wa manispaa ya songea wanapata huduma bora za afya zaidi ya shilingi bilioni sita zimetumika katika ujenzi wa miundombinu katika hospital ya manispaa, vituo vya afya na zahanati.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Aidha katika sekta ya elimu mstahiki meya amesema madarasa 244 katika shule za msingi na sekondari yenye thamani ya shilingi bilioni 5.2 yamajengwa, shule mpya nne zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimejengwa hali ambayo imepelekea idadi kubwa ya wanafunzi wa awali darasa la kwanza na kidato cha kwanza kujiunga na shule.
1742786820071.png
 
Back
Top Bottom