franklin12xx
Member
- Sep 24, 2014
- 28
- 31
Katika jambo ambalo linanishangaza mno ni suala la ukuu wa mkoa na umeya.Hakika nchi hii ni ya ajabu haina mfano.Inakuwaje mkuu wa mkoa kama wa Dar es Salaam anakuwa anaheshimika na kupewa nafasi katika mambo muhimu huku cheo chake ni cha kuteuliwa tu wakati mameya ndio inabidi wawe na hayo majukumu.
Kwa mfano CRDB walivyotoa mchango wa madawati badala ya kumkabidhi meya wa jiji wamemkabidhi mkuu wa mkoa.
Sherehe na matukio muhimu mkuu wa mkoa ndio anapewa nafasi ilhali meya aliyechaguliwa na wananchi yupo yupo tu.
Matamko muhimu yanatolewa na mkuu wa mkoa huku meya wa jiji yupo tu kimya.
Hii katiba yetu kama ndio inaruhusu huu ujinga ni heri ifutiliwe mbali, haiwezekani mkuu wa mkoa, kateuliwa tu huku meya aliyetokana na kura za wananchi na madiwani wenzake anawekwa kando.
Kiukweli inasikitisha haya mambo.