Meya Jacob: Marufuku ya Mahakama kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi; "Usalama wa Taifa" umeshinda

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Na Boniface Jacob

IJUMAA, Mei 10, mwaka huu, Taifa lilishuhudia hukumu ya kihistoria katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mahakama ilibatilisha vifungu vya Sheria ya Uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, miji, wilaya na manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu walioongozwa na Jaji Atuganile Ngala. Wengine ni Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo.

Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2008, ilifunguliwa na watetezi wa haki za binadamu wakiwakilishwa na Bob Chacha Wangwe ambaye alikuwa akitetewa na wakili Fatma Karume. Kwanza niwape hongera kwa ushindi wa kesi hiyo ya kihistoria dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Mambo ya msingi yaliyoamriwa katika kesi hiyo ni kwamba vifungu 7(1) na 7(2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Taifa Cap 343 R.E 201, vilikuwa vinawapa uhalali wakurugenzi kusimamia uchaguzi, pia kuteua wasimamizi (returning Officers). Vyote kwa pamoja vimebatilishwa kwani vinaenda kinyume na matakwa ya Katiba Ibara ya 21, 26, 74(14).

Kifungu cha 7(3) kilikuwa kinaipa NEC mamlaka ya kumteua mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi. Mahakama imeona neno "yeyote" lilikuwa halina ukomo au ulinzi wa kuhakikisha huyo "yeyote" anakuwa si mwanachama wa chama chochote.

Walalamikaji walifanikiwa kuishawishi Mahakama pasipo shaka kuwa wakurugenzi wa sasa 74 kati ya 184 waliopo walikuwa wanachama au viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kuanzia sasa, baada ya hukumu hiyo, ikiwa NEC itafanya uteuzi, italazimika kuzingatia kifungu cha 7(2) cha Sheria ya Uchaguzi, ambacho kinataka msimamizi wa uchaguzi awe mtu huru, asiyefungamana na chama cha siasa.

Baada ya hukumu hiyo takatifu, pamezuka pande mbili zinazokinzana na kuzodoana. Upande mmoja wanashangilia, mwingine hawajakubali.

Wote wanakosea. Katika kesi hiyo hakuna chama wala raia aliyeshinda. "Usalama wa Taifa" ndiyo umeshinda.

Simaanishi "Usalama wa Taifa" kama taasisi bali usalama wa Taifa kwa maana ya masilahi ya Taifa.

Ni ushindi wa usalama wa Taifa kwa maana, hukumu hiyo inachora mstari wenye kuhakikisha Taifa linakuwa salama na tulivu wakati wote. Watu wakiwa salama na mali zao hata baada ya uchaguzi.

Kwa lugha rahisi ni kuwa majaji wa Mahakama Kuu kupitia hukumu hiyo, wamezingatia masilahi mapana ya Taifa na usalama wa watu.

Majaji wameliepusha Taifa kuingia katika machafuko. Na huo ndiyo wajibu wa kwanza wa Mahakama, kutoa haki, kusimamia utawala wa sheria, kuepusha kundi au mtu yeyote kutumia njia mbadala kupata haki zaidi ya Mahakama.

Siyo siri kwamba kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Oktoba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani, matumaini ya Watanzania kushiriki uchaguzi huru na haki, yalikuwa yametoweka.

Hata sasa, baadhi ya vyama vimekuwa vikisusia uchaguzi mdogo wa udiwani na ubunge, baada ya kuona hakuna maana tena ya uchaguzi kufuatia vitendo vya wakurugenzi ambao ni makada wa CCM kutumia kila njia kuwapa ushindi wagombea wa chama chao.

Mifano ya vituko vya wakurugenzi makada ni mingi, ila hapa nitataja viwili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe ili chama chake kishinde, alijifungia ofisini mapaka muda wa kupokea fomu za wagombea ulipopita kisha akamtangaza mgombea wa chama chake kupita bila kupingwa. Alijificha ili wagombea wa vyama vingine wasimpate.

Mkurugenzi mwingine aliyekuwa kwenye vielelezo vya kesi Mahakama Kuu, kama uthibitisho wa wakurugenzi makada wa CCM ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambaye katika uchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Kinondoni Februari 2007, aligoma kutoa viapo vya mawakala kwa vyama vya upinzani, alitoa kwa CCM peke yake.

Je, katika mazingira ya namma hiyo, ukimya wa wapinzani ni maandalizi ya Nini? Au ndiyo kama wahenga walivyosema kimya kingi kina mshindo?

Sasa kwa nini tusiishukuru Mahakama Kuu kutuepusha na huo mshindo wa wapinzani? Sababu kila mmoja anajua kuwa mazingira haya ya wakurugenzi kufanya yanayo kipendeza chama chao ni kiashiria kibaya sana cha uvunjifu wa amani.

Najua yatabakia maswali kuwa je, Tume yanyewe ni huru au siyo huru? Swali lingine ni kuhusu uhakika wa watakaoteuliwa kama hawatakuwa mbeleko ya CCM.

Dhana ya usalama wa nchi ninayoijengea hoja ni kama chama tawala kinafanya hujuma au mbinu za kisiasa basi zisiwe zile za wazi wazi kama ambazo tumezishuhudia au kusikia.

Mfano kila mtu anajua kauli zinazosadikika kuwa zilitolewa na Rais John Magufuli kwenda kwa wakurugenzi: "Nakupatia gari nakupa kila kitu alafu umtangaze mpinzani."

Kufanya hivyo hakumfanyi mtu kujiandaa kupita mlangoni hata kidogo. Ni sawa umeziba mlango kwa matofali hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani kujua mapema njia ya kupita ni dirishani tu.

Nchi ingeweza kuweka mazingira salama ya uchaguzi ambayo pamoja na dosari za mfumo wenye malalamiko kama ilivyo Afrika, lakini angalau wapinzani wabaki na imani kuwa upo uwezekano wa kufunguliwa mlango na kupita, sababu wanakuwa wanauona.

Mahatma Gandhi alipata kusema: "I believe that true democracy can only be an outcome of nonviolence. The structure of a world federation can be raised only on a foundation of nonviolence and violence will have to be totally given up in world affairs."

Kwa tafsiri ya kawaida ni kwamba demokrasia ya kweli huletwa na muundo au taratibu za njia zisizomwaga damu.

Uwezekano wa kushinda unatakiwa angalau kurudi kama ilivyokuwa awali tangu mwaka 1995 mpaka 2015, au kupiga hatua zaidi ya kupata tume huru ya uchaguzi.

Najaribu kutafakari kuwa ingekuwaje uchaguzi 2020 kwa makada hawa kusimamia uchaguzi kama siyo marufuku ya Mahakama Kuu?

katika hali ilivyokuwa, kukataa kutoa viapo au kukimbia ofisi siku ya kurudisha fomu ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa, ni dhahiri kama siyo uamuzi wa Mahakama Muu basi Tanzania tulikuwa tunaifuata njia ya machafuko kama Kenya mwaka 2008.

Sababu sote tunajua Watanzania si wajinga na wasingekubali hali hiyo, je dola ilikuwa imejiandaaje kwa nchi nzima ikiwa kitendo cha Mkurugenzi Kinondoni kutotoa viapo kilisababisha majeruhi wa risasa na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini?

Miaka ya nyuma, pamoja na dosari za NEC, lakini wapinzani sehemu nyingi walitangazwa kwa nguvu ya umma. Hata vyombo vya dola vilishauri ili usalama uwepo.

Hali kama hizo zilitokea Ubungo katika kituo cha majumuisho Shule ya Sekondari ya Loyola. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Johnson Kiravu alipata cha moto baada ya kukutana na wanachi waliopindua gari lake getini wakati akiwa anaingia kukagua vituo vya majumuisho vya Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya wananchi kuhisi alikuwa anaingiza laptop za kuchakachukua matokeo.

John Mnyika, mgombea wa upinzani alipokwenda getini kuomba Kiravu aruhusiwe kupita, wananchi walimgeuzia kibao kwa kumshutumu kuwa amepewa pesa. Ilibidi Mnyika awe mpole na wananchi wakawa ndiyo wenye kauli ya mwisho.

Mifano ipo mingi. Hali ilitokea hivyo japo hakukuwa na makada wa waziwazi katika usimamizi wa uchaguzi. Wapinzani walitangazwa baada ya Wananchi kutumia nguvu ya umma. sasa wakurugenzi ni makada bila kificho, hali ingekuwaje Uchaguzi Mkuu 2020?

Mifano ni kama vile majimbo ya Shinyanga Mjini 2010, Nyamagana 2010, Kawe 2010 na 2015, Kibamba 2015, Bukoba Mjini 2015, Arusha 2010 na 2015, Mbeya 2010 na 2015, Moshi 2015, Tarime Mjini na Vijijini 2015, Kinondoni 2015 hapo ni kwa uchache. Wakurugenzi walilazimika kutangaza matokeo baada ya wananchi kuzunguka vituo vya majumuisho na kuamua liwalo na liwe.

Hivyo, ingawa Mwanasheria Mkuu anayo nafasi ya kuukatia rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu, akifanya hivyo ajue atakuwa anakatia rufaa "Usalama wa Taifa".

Jambo pekee kwake na kwetu katika kutafakari uamuzi huu wa kihistoria, tuepushe ushabiki wa pande mbili kuona kuwa wapo walioshindwa na walioshinda.

Badala yake pande zote mbili zione kuwa usalama wa Taifa umeshida kwa sababu wana CCM na wapinzani wote wanataka amani. Mwanasheria Mkuu pia anataka amani na utulivu wa nchi yetu.

Dunia itashangaa kama Mwanasheria Mkuu atakatia rufaa uamuzi wenye masilahi mapana na nchi kwa sababu ulioshinda ni Usalama wa Taifa letu.

Bila shaka hiki ndicho kilikuwa kipaumbele kwa majaji wetu wazalendo wa Mahakama Kuu. Kama kuna mtu atataka kwenda kinyume na jambo hili jema basi lawama hazita kuwa mikononi mwao sababu wameupatia ushindi Usalama wa Taifa letu.

Imeandikwa na
BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
 
Attachments

  • IMG-20190513-WA0063.jpg
    IMG-20190513-WA0063.jpg
    79.4 KB · Views: 62
  • IMG-20190513-WA0064.jpg
    IMG-20190513-WA0064.jpg
    80.3 KB · Views: 36
  • IMG-20190513-WA0061.jpg
    IMG-20190513-WA0061.jpg
    57.3 KB · Views: 65
  • IMG-20190513-WA0062.jpg
    IMG-20190513-WA0062.jpg
    59.3 KB · Views: 61
  • IMG-20190513-WA0060.jpg
    IMG-20190513-WA0060.jpg
    57.3 KB · Views: 37

Asante Sana Meya Wangu Jacob Nakupenxa Sana na Mungu akubariki.

Vile vile nakukumbush mshughulikie Maswala ya Rushwa pale kwenye manispaa yako ya ya Ubungo. Kuna wala rushwa wengi section ya Aridhi, nyumba na makazi.
 
Meya Jacob unatosha kabisa kuwa katibu mkuu chadema maana mbinu zote chafu za ccm unazifahamu na unazimudu
 
Asante Sana Meya Wangu Jacob Nakupenxa Sana na Mungu akubariki.
Vile vile nakukumbush mshughulikie Maswala ya Rushwa pale kwenye manispaa yako ya ya Ubungo. Kuna wala rushwa wengi section ya Aridhi, nyumba na makazi.
uki quote uzi wote unatusababishia uvivu wa kusoma
 
Uchambuzi gani wa boniface wala hajui kitu huyu self made msomi. Jacob ni mtu mwenye mwelekeo wa fujo na ukisoma uzi huu wake anatishia usalama kama uamuzi huu ukibatilishwa kwa rufaa.
Hii hukumu inakatiwa rufaa na inashinda kabisa. Huweze ku assume mtu yeyote kwa kua tu ni mwanachama wa chama fulani basi hawezi kua msimamizi wa uchaguzi. Kitu kikubwa ni mtu kutekeleza masharti ya usimamizi. Ndio maana msimamizi anakula kiapo. Wala tume hua haiulizi mkurugenzi kabla hajakula kiapo yeye ni chama gani au hana chama. Mambo ya kua na chama au kutokua mwanachama ni kitu binafsi na haki ya kila raia. Wapinzani lazima wakubali wasimamizi lazima watoke nchini na kugharamikiwa na serikali yetu. Hawawezi kutoka umoja wa mataifa au umoja wa ulaya au kwingine. Wafanye siasa hadi kukubalika sio kufikiri tume ndio inawanyima kuongoza nchi.
 
Tena katika kundi la waliofurahia zaidi uamuzi huu nadhani ni wakurugenzi wenyewe. Hukumu hii imewaweka huru kabisa dhidi ya mashinikizo yaliyokuwa yakiwapa taabu sana baadhi yao kati ya kuamua kwa haki au vinginevyo.
 
Kwa ninavyoifahamu mahakama ya rufaa kwa weledi , serikali itaagukia pua tena
Rufaa sio suala la weledi ama opinion ya mtu... ni malumbano ya hoja za kisheria..
Naunga mkono ushindi wa kutowatumia wakurugenzi 74 tajwa... Sina uhakika kama wakurugenzi wasio na vyama watakataliwa pia.
Wasipoangukia puwa tusisononeke na kuiona mahakama kama haifai...ama kuita maagizo toka juu.
 
Hawa 74 wanabainika kuwa makada wa ccm , lakini wote hata hao wengine wameteuliwa na Mwenyekiti wa ccm , hatutaki wasimamizi wa uchaguzi wateuliwe na Mwenyekiti wa ccm
 
Uchambuzi gani wa boniface wala hajui kitu huyu self made msomi. Jacob ni mtu mwenye mwelekeo wa fujo na ukisoma uzi huu wake anatishia usalama kama uamuzi huu ukibatilishwa kwa rufaa.
Hii hukumu inakatiwa rufaa na inashinda kabisa. Huweze ku assume mtu yeyote kwa kua tu ni mwanachama wa chama fulani basi hawezi kua msimamizi wa uchaguzi. Kitu kikubwa ni mtu kutekeleza masharti ya usimamizi. Ndio maana msimamizi anakula kiapo. Wala tume hua haiulizi mkurugenzi kabla hajakula kiapo yeye ni chama gani au hana chama. Mamvo ya kua na chama au kutokua mwanachama ni kitu binafsi na haki ya kila raia. Wapinzani lazima wakubali wasimamizi lazima watoke nchini na kugharamikiwa na serikali yetu. Hawawezi kutoks umoja wa mataifa au umoja wa ulaya au kwingine. Wafanye siasa hadi kukubalika sio kufikiri tume ndio inawanyima kuongoza nchi.
Unafahamu mazingira ya kifo cha Akwiliña source nini?
 
Sipati picha kama Unakuta mkurugenzi ni kada ,Mkuu wa wilaya Kada, Ocd kada,RSO kada, RPC Kidumu chama cha mapinduzi . Hakuna haja ya uchaguzi mahali hapo mana ni kupoteza fedha Bure na Kuja kuumiza watu kwa mabumu yao na risisi zao Bure.
 
Uchambuzi gani wa boniface wala hajui kitu huyu self made msomi. Jacob ni mtu mwenye mwelekeo wa fujo na ukisoma uzi huu wake anatishia usalama kama uamuzi huu ukibatilishwa kwa rufaa.
Hii hukumu inakatiwa rufaa na inashinda kabisa. Huweze ku assume mtu yeyote kwa kua tu ni mwanachama wa chama fulani basi hawezi kua msimamizi wa uchaguzi. Kitu kikubwa ni mtu kutekeleza masharti ya usimamizi. Ndio maana msimamizi anakula kiapo. Wala tume hua haiulizi mkurugenzi kabla hajakula kiapo yeye ni chama gani au hana chama. Mamvo ya kua na chama au kutokua mwanachama ni kitu binafsi na haki ya kila raia. Wapinzani lazima wakubali wasimamizi lazima watoke nchini na kugharamikiwa na serikali yetu. Hawawezi kutoks umoja wa mataifa au umoja wa ulaya au kwingine. Wafanye siasa hadi kukubalika sio kufikiri tume ndio inawanyima kuongoza nchi.
Utakuwa Ni miongoni mwa mapoyoyo tena poyoyo kweli kweli!!!
 
Wewe nawe sijui umetoka sayari ya wapi.

Walichofanya majaji Ni kulinda au kutoa ulinzi zaidi kwa watia Nia, wateuliwa, na wapiga kura bila kuzalisha chama na wasio na chama.

Kwa lugha nyepesi wananchi wote wameongezewa usalama wa kura zao.

Sasa mkata rufaa anamkatia Nani? Kwa faida ya Nani hasa maana matokeo yanawanufaisha wote including mlalamikiwa.

Sasa nilifikiri ilikua wote wapongezane, badala yake Kuna mtu au watu wanataka wananchi waporwe Haki yao na waongezewe mashaka kwamba kura zao haziamui mshindi.

Tumeona mchana kweupe chaguzi za marudio na nyenhine nyingi kiss ukada.

Ushindi wa Bob Chacha Ni ushindi wa watanzania wote na Ni ushindi kwa walalamikiwa pia. Je mnakata rufaa kumkomoa Nani?
 
Back
Top Bottom