Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametakiwa kujitathimini iwapo anastahili kuendelea kuwa mtumishi wa umma katika nafasi aliyonayo baada ya kutiwa hatiani na mahakama kuu mkoa wa Tanga na kutakiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa kosa la kumdhalilisha mtumishi mwenzake kwa matusi.
Kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2015,Gambo alikata rufaa mahakama kuu ,kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama za chini,katika kesi ya madai iliyofunguliwa na mlalamikaji ,Najum Tekka ambaye ni mwanasheria wa halmashauri wilaya ya Korogwe aliyekuwa akimlalamikia Gambo kumtolea lugha ya kumdhalilisha kuwa anadigrii ya nguo ya ndani(chupi).
Kwa mujibu wa hukumu hiyo nakala tunayo, iliyotolewa, Septemba 9 mwaka 2016 na jaji Amour Khamis wa mahakama kuu,mkoani humo,meya wa jiji la Arusha, Kalisti Lazaro alisema kuwa Gambo amekaidi kulipa kiasi hicho cha fedha kilichoamuriwa na mahakama na kuitaka mahakama itoe amri akamatwe na kufilisiwa Mali zake na afungwe.