Meya Arusha asikitishwa na upigaji wa RC Gambo fedha za Rambirambi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
KAlisti Lazalo meya wa jiji la Arusha amemshukia mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo kueleza umma fedha za rambirambi zilivyochangwa na Watu mbalimbali yakiwemo makampuni na taasisi za umma anazodaiwa kuzitafuna.

Fedha hizo zinadaiwa kufikia sh, milioni 300,hivi karibuni aliwatangazia wanahabari kuwa wahanga wa tukio hilo la Ajali kila mmoja amepata kiasi cha sh,milioni 3.8 matokeo yake baadhi yao waliambulia sh,milioni 2.8 hatua ambayo imezidi kunogesha utafunaji wa fedha hizo .

Wakazi wa Arusha wamemtaka Gambo kurejesha mamilioni ya wahanga hao aliyoyatafuna .

Meya ametoa siku tatu kwa Gambo kutoa ufafanuzi wa jambo hill kabla ya jtano na akishindwa ,ataweka wazi fedha zilizotafunwa kwani anajua wrote waliochangia na kiasi cha fedha kilichopatikana.

A

Tunasubiri kuona huo mchanganuo.
 
Siku tatu alizotoa Meya kwa Mkuu wa Mkoa Arusha

ARUSHA.png

Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaroamempa siku tatu kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutoa taarifa sahihi ya michango ya rambirambi zilizotolewa kwa familia za watu 36 waliofariki katika ajali iliyotokea Karatu Arusha.

Meya Kalist amesema >>>Kumekuwa na maneno mengi hapa Arusha kuhusu pesa za rambirambi, watu wamekuwa wakinipigia simu na kuuliza lakini kwavile hakuna mtu yeyote aliyehusika kukusanya na kutumia michango zaidi ya Mkuu wa Mkoa namtaka atoe ufafanuzi wa fedha zilizochangwa.

Nampa siku ya leo na kesho asipokuja hadharani kuwaeleza wananchi nama fedha zilivyotumika nitaweka hesabu niliyonayo mimi hadharani kwasababu wananchi waliopeleka hela kwa Mkuu wa Mkoa ni wa Arusha<<<- Meya Kalist Lazaro

Siku tatu alizotoa Meya kwa Mkuu wa Mkoa Arusha

ARUSHA.png

Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kutoa taarifa sahihi ya michango ya rambirambi zilizotolewa kwa familia za watu 36 waliofariki katika ajali iliyotokea Karatu Arusha.

Meya Kalist amesema, ''Kumekuwa na maneno mengi hapa Arusha kuhusu pesa za rambirambi, watu wamekuwa wakinipigia simu na kuuliza lakini kwavile hakuna mtu yeyote aliyehusika kukusanya na kutumia michango zaidi ya Mkuu wa Mkoa namtaka atoe ufafanuzi wa fedha zilizochangwa.

Nampa siku ya leo na kesho asipokuja hadharani kuwaeleza wananchi nama fedha zilivyotumika nitaweka hesabu niliyonayo mimi hadharani kwasababu wananchi waliopeleka hela kwa Mkuu wa Mkoa ni wa Arusha'' Meya Kalist Lazaro.

Ikumbukwe alinukuliwa akisema serikali ya mkoa ndio itagharamia shughuli nzima ya msiba na sio pesa za rambirambi za taasisi na watu binafsi.
 
Meya amekosa kazi ya kufanya kwa kweli.

Any way kila moja atavuna alichopanda 2020. Suala la muda tu.
 
Jana Nyalandu ameeanzisha mchango wa kujenga ICU kwenye hospital ya mkoa wa Arusha ,zikitokana na walioanza kuchangia matibabu ya majeruhi watatu kabla ya kupata ufadhili
BALAA ni kwamba amemtaka Gambo awe mweka hazina
TWAFAAA
 
mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu ili ampige vizuri najua huyo "lord loffa"alitumwa arusha kuja kumvuruga mh lema bila ya kujua kuwa lema ni mpango wa yehova
aliloandika mungu ameandika siku zote "juhudi haishindi kudra"
 
Hii laana utawatoa roho watu! Kwenye maandiko MUNGU anazuia kabisa kunyanyasa yatima na wajane. Sasa sijui kama anaruhusu wafiwa wadhulumiwe rambirambi! Maana kwa yatima na wajane anawaambia wale wanaowanyanyasa kwamba atawaua wake zao au waume zao nao wawe wajane na wana wao wawe yatima. Sasa Gambo naye asije akakumbana na gadhabu ya MUNGU kwa kunyang'anywa na yeye watoto wake ili naye aonje machungu!
 
Back
Top Bottom