Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 121
- 202
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo ameitaka Serikali ifanye uchunguzi wa kina dhidi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha akidai limekithiri kwa ubadhirifu wa fedha za umma. Amedai imeghushi risiti za EFD kiasi cha Sh. 699 milioni, imemlipa mdhabuni kiasi cha Sh. 36.5 milioni bila kutoa huduma, vifaa vyenye thamani zaidi ya Sh. 123 milioni vilivyodaiwa kununuliwa havijafikishwa eneo la ujenzi.
“Halmashauri ya Jiji la Arusha changamoto kubwa ni ubadhirifu na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri, wanachukua hela hawajali sababu wanajua ngazi ya mkoa na wilaya hakuna cha kuwafanya. Ni vizuri Waziri wa TAMISEMI wakafanya utaratibu wa kuweka jicho la ziada kwenye jiji letu kuangalia matumizi fedha za umma,” amesema Gambo.