Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,668
- 15,066
Kwa mujibu wa mbunge wa jimbo la Arusha mjini bwana Mrisho Gambo, baadhi ya viongozi wa jiji wamechukua fedha za halmashauri na kuziweka katika akaunti zao binafsi, akidai kuna mmoja amewekewa Sh103 milioni, mwingine Sh65 milioni akisema wanaifanya halmashauri kama shamba la bibi.
“Halafu wanataka mbunge acheke cheke tu, sasa utakuwa mbunge wa aina gani? Sipiti njia hapa ndio nimefika na nitaangaika na hawa wapiti njia hadi nijue mwisho wao ni wapi? Amesema Gambo.
Haya hivyo, mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda amesema amesikia kilio cha Gambo kuhusu baadhi ya watumishi wa jiji la Arusha kuwekewa fedha katika akaunti zao binafsi.
Mtanda amesema kwa mujibu wa taratibu mtumishi anaweza kuchukua masurufu na kufanya retirement kwa mwajiri wake, ingawa upo ukomo wa kiasi cha fedha kinachopaswa kuchukuliwa kisheria.
“Suala hili limeshachukuliwa hatua na ofisi ya katibu tawala mkoa, nimesoma nakala ya barua wiki moja iliyopita inayomtaka mkurugenzi wa Jiji na maofisa waliotajwa kutoa maelezo juu ya suala hilo. Ikithibitisha kama kuna matumizi mabaya ya fedha serikali itachukua hatua."
“Naamini mbunge pia anafahamu kuwa uchunguzi wa suala hili unaendelea. Tukiacha haya yanayosemwa bila kuyatolea ufafanuzi wananchi wataamini kuwa serikali yao haichukui hatua dhidi ya tuhuma za ubadhirifu, hivyo kuifanya serikali kuwa dhaifu mbele ya macho ya umma,” amesema Mtanda.