Meya Arusha aanika mikakati yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya Arusha aanika mikakati yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Meya Arusha aanika mikakati yake Tuesday, 28 December 2010 20:16

  Happy Lazaro, Arusha
  HALMASHAURI ya Jiji la Arusha limejiwekea mikakati mipya ya ukusanyaji mapato na kuhakikisha yanaongezeka kwa asilimia 80, kipindi cha miaka miwili ijayo.

  Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo, alisema mkakati mkubwa ni kuhakikisha vyanzo vya mapato vinaongezeka, huku wakibuni mbinu mpya ya ukusanyaji ambayo haitasumbua wananchi.
  Lyimo alisema badala ya kuwatumia watumishi wake kukusanya mapato, atakuwa wasimamizi na kwamba, watawatumia mawakala na wakusanyaji kodi ili kufuatilia kwa undani zaidi.

  “Tunachotaka kufanya ni kuhakikisha kuwa, ukusanyaji kodi wetu unakuwa wa kisasa zaidi ambao hautasumbua wananchi wetu na kwa njia hiyo, kila mwananchi atapenda kulipa kodi kwa hiari yake,” alisema Lyimo.
  Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa ndani ya miaka miwili, jiji hilo linaweza kukusanya mapato kwenye vyanzo mbalimbali kwa umakini zaidi na kwa muda muafaka bila kusumbua wananchi.

  Lyimo alisema licha ya kuweka mikakati hiyo mipya ya ukusanyaji kodi, pia atahakikisha anaongeza barabara ili kuepukana na msongamano uliopo.
  Aliendelea kuwa barabara zilizopo nje ya mji zitatengenezwa kwa kiwango cha lami, huku nyingine ambazo ni chakavu zikikarabatiwa ili kuongeza hadhi ya jiji.

  Lyimbo alisema kwenye mikakati ya kuongeza barabara, watahakikisha kuwa wanaongeza madaraja mengi iwezekanavyo, lengo likiwa ni kuunganisha kijiji kimoja hadi kingine ili kuboresha mawasiliano.

  Pia, alisema watahakikisha wanaboresha utalii wa ndani kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha milima ambayo ni vivutio kwa watalii walio wengi.

  Kuhusu usafi wa jiji, Lyimo alisema wamejiwekea mikakati mbalimbali kuhakikisha suala la usimamizi wa mazingira linabinafsishwa kwa watu binafsi.

  Alisema sheria zitatungwa kwa mtu anayetupa taka ovyo kuchukuliwa hatua kali, ikiwamo kutozwa faini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Tatizo la uchafu Arusha lianze na kuweka sheria ndo ndog ya kuhakikisha ya kuwa kila nyumba ina pipa la kuwekea uchafu lenye ukubwa kulinga na idadi ya watu.............faini zipo lakini zimeshindwa kutuondolea balaa hili la uchafu.........................

  Hivi kwanza huyu meya ni nani alimchagua?
   
 3. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mbona haongelei swala la uvamizi wa open space wa vigogo na watoto wao?
   
 4. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawezi kuongelea swala la uvamizi kwa sababu hawezi kilishughulikia,
   
 5. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe Meya wa Arusha ameshakubalika?
   
 6. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyu ni meya kwa vipi na alichaguliwa na mkutano ambao haukuwa na koramu.

  Mikakati yake siyo sahihi. Cha maana kwake kama Diwani wa Oloirien, kukamilisha Ofisi ya Kata yale na pia angesemea daraja la Mwanama ambayo ipo kwenye Kata yake. Kila siku anapita hapo na ipo hatarini kuondoka mafuriko yakija.
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  HALMASHAURI ya Jiji la Arusha limejiwekea mikakati mipya ya ukusanyaji mapato na kuhakikisha yanaongezeka kwa asilimia 80, kipindi cha miaka miwili ijayo.

  Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo, alisema mkakati mkubwa ni kuhakikisha vyanzo vya mapato vinaongezeka, huku wakibuni mbinu mpya ya ukusanyaji ambayo haitasumbua wananchi.
  Lyimo alisema badala ya kuwatumia watumishi wake kukusanya mapato, atakuwa wasimamizi na kwamba, watawatumia mawakala na wakusanyaji kodi ili kufuatilia kwa undani zaidi.

  “Tunachotaka kufanya ni kuhakikisha kuwa, ukusanyaji kodi wetu unakuwa wa kisasa zaidi ambao hautasumbua wananchi wetu na kwa njia hiyo, kila mwananchi atapenda kulipa kodi kwa hiari yake,” alisema Lyimo.
  Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa ndani ya miaka miwili, jiji hilo linaweza kukusanya mapato kwenye vyanzo mbalimbali kwa umakini zaidi na kwa muda muafaka bila kusumbua wananchi.

  Lyimo alisema licha ya kuweka mikakati hiyo mipya ya ukusanyaji kodi, pia atahakikisha anaongeza barabara ili kuepukana na msongamano uliopo.
  Aliendelea kuwa barabara zilizopo nje ya mji zitatengenezwa kwa kiwango cha lami, huku nyingine ambazo ni chakavu zikikarabatiwa ili kuongeza hadhi ya jiji.

  Lyimbo alisema kwenye mikakati ya kuongeza barabara, watahakikisha kuwa wanaongeza madaraja mengi iwezekanavyo, lengo likiwa ni kuunganisha kijiji kimoja hadi kingine ili kuboresha mawasiliano.

  Pia, alisema watahakikisha wanaboresha utalii wa ndani kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha milima ambayo ni vivutio kwa watalii walio wengi.

  Kuhusu usafi wa jiji, Lyimo alisema wamejiwekea mikakati mbalimbali kuhakikisha suala la usimamizi wa mazingira linabinafsishwa kwa watu binafsi.

  Alisema sheria zitatungwa kwa mtu anayetupa taka ovyo kuchukuliwa hatua kali, ikiwamo kutozwa faini.

  je huyu Meya ameshatambulika rasimi?Aiisee ulichakachua umeya wako, cjui kama unatambulika au ndo wale wale tu. Ulichakachua kuingia kwenye huo umeya na bado huna hata aibu unaanza kazi, Hivi nyinyi CCM mkoje? au ndio huo utawala wa mabavu?
   
 8. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nchi hii watu wakiambiwa wana uroho wa madaraka watadai una lako jambo! Lakini huyu Gaudence Lyimo ametumia approach gani tofauti na aliyotumia Gagbo wa Ivory coast, Mwai Kibaki au Mugabe wa zimbabwe? Je, ni mtu wa kuaminiwa kupewa nyadhfa kubwa siku za usoni?
   
 9. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Safi sana Mangi Lyimo.

  Tunaunga mkono kuchaguliwa kwako, wape pongezi Madiwani kwa kazi nzuri.

  Usibabaishwe na maneno ya chama cha wanung'unikaji, chapa kazi.
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kishongo, hujui kama uchaguzi wa Meya wa Arusha haukuwa halali?
   
 11. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dosari zilizojitokeza si za msingi, ndiyo maana Mstahiki ameanza kumwaga sera.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  unalolionge uunalijua lakini?
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo:
  Zaidi jaribuni kuona wanawadi wanamatatizo gani na jinsi gani Halmashauri yako ya Jiji itakavyoweza kuwasaidia zaidi ya kukusanya kodi!
   
 14. d

  defence JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 497
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  Mimi nadhani kuna haja tupungue kidogo ili kila
  mtu atambue kuwa hii nchi si mali ya yeyote hata
  ikibidi kuanza na mimi , maana naona kuna wafalme
  ndani ya TZ
   
 15. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi Lymo akiendelea naona sawa tu kwani he has qualities za kuwa Mayor wa Arusha siyo kama kina Lotta Laizer. The guy has below qualities

  1. Amesoma
  2. Hana njaa
  3. Mwadilifu
  4. Siyo mlevi
  5. Hana makuu
  6. Hana siasa za kinafiki za CCM

  Nafikiri Mbunge na madiwani wote wampe support huyu bwana ili tujenge mji wetu wa Arusha.

  Lymo (GAIMO) chunga hizo tender za kukusanya kodi. Wape kampuni ambazo ni capable siyo kupeana kama ilivyo kawaida.
   
Loading...