MEXICO: Binti mdogo afukuliwa akiwa hai kifusini

MEXICO: Binti mdogo afukuliwa akiwa hai kifusini

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
95422942_hi038804669.jpg


Mtoto mmoja amegundulika kuwa hai baada ya harakati za waokoaji kuendelea katika nchi ya Mexico ambapo tetemeko kubwa la ardhi limeikumba kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Mtoto huyo amegunduliwa katika kifusi cha jengo la shule, hivyo waokoaji wanajaribu kumfikia mtoto huyo aliyefukiwa na kifusi pindi tetemeko lilipotokea jana.

Aidha waokoaji wamekuwa wakijaribu kumpitishia chakula na maji ndani ya kifusi wakati taratibu zikiendelea ili atoke salama.

Watoto 21 waliepoteza maisha baada ya jengo walilokuwemo kuvunjika huku wengine wakiwa bado ya kifusi hicho.


Hivisasa
 
Back
Top Bottom