Meter za umeme

mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
Tangia nipo mdogo nilkua nafikiria uwezo wa hizi meter pale unaponunua token na kwenda kuingiza na zikaandka accepted ivi ni kwamba zinatumia network au? Na kama network iyo ni ipi mpka kijijin uko ndan ndan imekua installed na kuweza kuwasiliana na Tanesco servers kujua hii token ni batili au lah... Au kuna tech nyngne zinatumia
Any idea tafadhali
 

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,287
2,000
Hakuna network, ni kwamba ile token imebeba encrypted information ambayo ni meter yako tu inaweza kuidecrypt. Tumeshaongelea sana humu tafuta thread hiyo.
 

mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
Hakuna network, ni kwamba ile token imebeba encrypted information ambayo ni meter yako tu inaweza kuidecrypt. Tumeshaongelea sana humu tafuta thread hiyo.

Apa inatosha mkuu nshaelewa
 

ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
3,052
2,000
hapo nimewapata vyema, nilidhani Meter za luku zinatumia simcard kama vile machine za EFD
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
0
Thread kama hizi za Elimu hazipati sana wachangiaji au wasomaji kwa kuwa tumechagua kuwa Wajinga, tunatamani kujua ila hatupendi kujielimisha!
 

mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
Thread kama hizi za Elimu hazipati sana wachangiaji au wasomaji kwa kuwa tumechagua kuwa Wajinga, tunatamani kujua ila hatupendi kujielimisha!

Nenda kwa uzi za mapenzi patamu uko yan ndio tuko tofaut asee
 

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,518
2,000
Tangia nipo mdogo nilkua
nafikiria uwezo wa hizi meter pale unaponunua token na kwenda kuingiza
na zikaandka accepted ivi ni kwamba zinatumia network au? Na kama
network iyo ni ipi mpka kijijin uko ndan ndan imekua installed na kuweza
kuwasiliana na Tanesco servers kujua hii token ni batili au lah... Au
kuna tech nyngne zinatumia
Any idea tafadhali

Meter yako ya LUKU iko compatible na token uliyonunua. Ndiyo maana token yako ukiipoteza mtu mwingine hawezi kutumia ktk meter yake.
 

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
1,500
Yah kwa jins nilivyoelewa znyw haziitaji sever zmekua built in system ambayo itachukua zle token ku encrypt

nadhani lazima kutakuwa na sever ambayo ndiyo inaimonitor katika token. Maana hata umeme ukipanda yenyewe inajua ya kwamba inapaswa kuwa unit fulani. Hivyo kutakuwa na mawasiliano kwa njia ya satelite ambayo ndiyo inaipa taarifa.
 

mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
Kwa iyo unataka kusema ina network nayo? Ivyo sikubaliani napo maana angalia staffs zote zinazotumia satellites lazma zitegwe mahali fulan cuz waves zaki zinakwenda direct sasa yenywe luku sehem yeyote unaiweka.... Mkuu #comi apo sikubaliani nawe
 

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,287
2,000
nadhani lazima kutakuwa na sever ambayo ndiyo inaimonitor katika token. Maana hata umeme ukipanda yenyewe inajua ya kwamba inapaswa kuwa unit fulani. Hivyo kutakuwa na mawasiliano kwa njia ya satelite ambayo ndiyo inaipa taarifa.

Hakuna server inayoongea na LUKU hizo "unit fulani" ndo zipo encoded katika ile token inayoingia kwenye luku, maswala ya kupanda bei ya unit yote yanafanyika pale unaponunua, zile compyuta za wauzaji ndo zina connection na server.

Pia satelite haina uwezo wa kufanya kazi indoors not to mention gharama ya kuweka mitambo ya communication ya satelite kwenye kila LUKU ambayo inaweza kucommunicate na satelite bila dish ingekuwa ni gharama ya ajabu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom