Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Wakuu,
Taarifa toka TFDA ni kuwa dawa aina ya Metakelfin inayotumiwa na wengi kwa ajili ya matibabu ya Malaria isitumike kuanzia sasa mpaka itakapotolewa taarifa nyingine. Hii ni baada ya kugundua batch kubwa ya dawa hizi nyingi zikiwa bandia (fake).
Kwa yeyote ambaye anazo anashauriwa ASIZITUMIE.
Ni kwa taarifa tu
Habari yenyewe hii chini:
Margareth Ndomondo-Sigonda akitoa maelekezo kwa vyombo vya habari juu ya namna ya kutambua dawa feki.
MAMLAKA ya Chakula na Dawa(TFDA) imeagiza watu wote na wale wanaouza dawa ambao wana dawa ya malaria aina ya Metakelfin kurejesha waliponunua ili kuzipeleka Laborex Tanzania kwa uchunguzi zaidi.
Dawa hizo zimeelezwa kuwa nyingi zilizopo mtaani ni za bandia na hazikidhi viwango vya kemikali inayotakiwa kutibu malaria.
Pamoja na kuagiza dawa hizo kurejeshwa kwa wahusika pia TFDA imepiga marufuku kwa muda uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Metakelfin hapa nchini hadi hapo itakapotangazwa tena.
Dawa hizo inasemekana hazijawahi kuidhinishwa na mamlaka hiyo kuingizwa nchini.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo-Sigonda (pichani) alisema katika kipindi hiki wagonjwa hasa wanaotumia dawa za SP ambao ni wajawazito wanashauriwa kutumia zenye viambata vya Sulpadoxine na Pyrimethamine kama inavyoelekezwa katika mwongozo wa kitaifa kuhusu tiba ya malaria.