Messi, Miami washindwa kutamba mbele ya wababe wa Afrika, Al Ahly kwenye Club World Cup

Messi, Miami washindwa kutamba mbele ya wababe wa Afrika, Al Ahly kwenye Club World Cup

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Pazia la michuano ya kombea Dunia kwa ngazi ya klabu limefunguliwa rasmi Alfajiri ya leo Juni 15, 2025 ambapo wawakilishi wa Afrika, Al Ahly ya Misri wametoshana nguvu kwa sare tasa na Lionel Messi na wenzake wa Inter Miami katika dimba la Hard Rock, Miami.

1749972607812.png
Wakati mashabiki wa Inter Miami wakitegemea maajabu kutoka kwa mshindi mara 8 wa Ballon d’Or, Lionel Messi, shujaa wa timu hiyo ya Marekani alikuwa kipa mkongwe Oscar Ustari (38) aliyeokoa hatari nyingi kutoka kwa Al Ahly ukiwemo mkwaju wa penalti wa Trezeguet muda mfupi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake mpaka dakika ya 90 licha ya Inter Miami kuja kivingine kipindi cha pili na kupelekea kipa wa Al Ahly, Mohamed El Shenawy kufanya kazi ya ziada kwa kuzuia hatari kutoka kwa Tadeo Allende sambamba na nafasi mbili za hatari kutoka kwa Messi.

Al Ahly ipo Kundi A kwenye michuano hiyo sambamba na Inter Miami, Fc Porto ya Ureno na Palmeiras ya Brazil. FT: Inter Miami 🇺🇸 0-0 Al Ahly

1749972701933.png
 
Mashindano haya marefa wa Kongo wapi,Kenya wapo kwenye ligi ya Siasa marefa wamekimbia
 
Mashindano haya marefa wa Kongo wapi,Kenya wapo kwenye ligi ya Siasa marefa wamekimbia
Pale unampeleka nani
Angalau Seleman Mwalimu atatusimulia kilichotokea ila bongo hakuna refa yeyote atafika Ile level
Kwanza caf wameshaona usanii wote kupitia azam tv
 
Ligi ya Mama
TFF ya Mama
Dabi ya Mama
Goli la Mama
Mama mitano tena
 
Back
Top Bottom