poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 456
- 175
Mshambuliaji matata wa Barcelona Lionel Messi ameibua tetesi za kuondoka Camp Nou baada ya kuanza kufuata ukurasa wa Chelsea katika mtandao wa Instagram.Tetesi za uwezekano wa mchezaji mashuhuri Lionel Messi kujiunga na timu ya Chelsea zimepamba moto baada ya mchezaji huyo kufuata ukurasa wa Chelsea katika mtandao wa Instagram na pia kuwafuata mlinda lango wa Chelsea Courtois na mlinzi Filipe Luis.Kuwekwa katika orodha ya wachezaji mbadala katika mechi yao ya La Liga dhidi ya Real Sociedad pia kulizidisha tetesi hizo.Mchezaji huyo pia hakujiunga na wachezaji wenzake katika mazoezi iliyohudhuriwa na maelfu ya watoto.Hapo awali Mourinho alikuwa amekanusha madai ya kumvizia mchezaji huyo huku akielezea thamani ya juu ya mchezaji huyo kuwa kizuizi.