Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 443
- 1,101
Lionel Messi ameitwa tena kwenye timu ya taifa ya Argentina kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin, Oktoba 6, 2026, utakaochezwa katika Uwanja wa Monumental jijini Buenos Aires. Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwa Messi kuichezea Argentina baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa mwezi uliopita.
Rais wa Shirikisho la Soka la Argentina (AFA), Claudio Tapia, amesema Messi amealikwa ili apewe heshima na kuagwa rasmi akiwa mbele ya mashabiki wa Argentina. Tapia pia amewaalika wachezaji wa kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2022 pamoja na familia zao kushiriki katika hafla hiyo.
Messi alitangaza kustaafu timu ya taifa Agosti 31, akifunga ukurasa wa zaidi ya miaka 20 akiwa na Argentina. Hata hivyo, amekubali kushiriki mchezo huo wa mwisho, ambayo itakuwa mechi yake ya 208 kwa Argentina.