Ndalahwa Fundi
Member
- Oct 16, 2011
- 7
- 1
Hawa watu wanatumia Masaburi kufikiri! Hatuwezi kuwabadili. Ni kuachana nao na sisi kusonga mbele. Sera zao ni kuzua chochote ili mradi kuupinga Ukristu. Ni mitazamo ya karne za zamani wakati wa vita za kueneza dini. Mpaka leo wanadhani dini inaweza kuenezwa kwa lazima. Chema chajiuza! Dunia ya leo yapaswa kuwa ya kistaarabu zaidi tofauti na zama za mababu zetu na wala huwezi kuwalaumu mababu kwa sababu kwa wakati huo binadamu alikuwa na kiwango chake cha uelewa tofauti na binanadamu wa leo. Binadamu wa leo yapaswajue binadamu wote ni sawa na ndugu bila kujali imani za kidini. Wapo wanaotumia dini kwa malengo yao binafsi na watu waaina hii wanatumia udhaifu wa uelewa wawaumini wao kuwaunga mkono kwa maslahi binafsi. Hatakwenye vyama mambo haya yapo, kumbuka CCM inapohubiri kuwa vyama vya upinzani ni vita wakati ikijua kuwa kwa hakika si kweli na kama ingekuwa kweli chama hicho kikiwa tawala kisingeruhusu mfumo wa vyama vingi uruhusiwe kikatiba.