asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,039
Kumekuwa na tabia ya watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayofahamu wenyewe kutenga meseji za uzushi kuwatisha watu na kuzisambaza kwenye mitandao ya simu.... kwamfano walianza na meseji ya kuwazimisha simu watu usiku wa saa sita (tarehe nimesahau) kuwa kutatokea migongano ya kimionzi ,kama mwezi mmoja uliopita tena wakawatumia tena watu namba wakidai ni ya freemansoon na leo nimepokea meseji kwenye simu inasema "ukitumiwa pesa na mtu usiyemjua kwenye mpesa, tigo pesa, aun airtel money au mtandao wowote usiitoe. kuna mtu katumiwa 100,000 na mtu asiyemjua kukosa utulivu kaenda kutoa baada ya kutoa kapata sms (Asante kwa kujiunga na freemansoon). kwa upendo wako watumie wote unaowajua. si uongo bali ni habari ya ukweli"
huu uzushi unaleta sintofahamu kwa jamii na zaidi kwa watu wasioweza kuchambua kipi ni kweli na kipi ni uzushi ,kawaida mimi huwajibu huo ni uongo mkubwa sana.
sasa najiuliza ,wanaotunga huu uzushi/uongo ni kina nani?
wanafaidika na nini?
ni nini malengo yao?
hawaoni wanaleta usumbufu usiokuwa wa lazima?
karibuni wadau na nyie mchangie ........