'MESEJI' ya HUJUMA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'MESEJI' ya HUJUMA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Jul 11, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Siwezi kuamini.Kweli Tume iliyosheheni Wasomi wa Sheria wabobezi inaweza kucheza mchezo mchafu kama huu?! Ni hivi,leo asubuhi nimepokea ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi. Ujumbe ( ingawa siwezi kuukumbuka neno hadi neno kwakuwa niliufuta haraka kwa woga mkuu) unanifahamisha kuwa nijiandae kwenda Mafia kutetea msimamo wa Tume juu ya Maoni ya Katiba. Sehemu ya Ujumbe huo unasema ifuatavyo : 'tuna taarifa kuwa wewe ni mzaliwa wa Mkoa wa Pwani'.

  Ujumbe ukaendelea:'Wilaya yako ya Kibaha haipo kwenye orodha ya Wilaya za mwanzo kukusanyiwa maoni yako ya Katiba. Kwa kuzingatia umuhimu na weredi wako wa kisheria,tunakualika uambatane nasi kwenda Mafia kwa ajili ya kushiriki kwenye Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba Mpya. Utafanya hivyo tena Wilayani Kibaha. Tutakuwa na Kikao cha uelekezi tarehe....' Nilipofika hapo nikaufuta na kuanza kulia. Nikachanganyikiwa hadi kusahau kuitunza nambari ya aliyenitumia ujumbe.Wakinikumbusha,nitaiweka nambari hapa jamvini. Nisameheni kwa 'kupanic' kwangu...

  Nashindwa kuamini na kuendelea kuandika habari hii. Kwakweli nimelia sana asubuhi ya leo. Kumbe watoa maoni wa Katiba Mpya ni Mamluki? Maoni yenyewe kumbe sio huru na ya haki.Hapa tulikofikia,inahitajika v... au? Sina imani na chochote juu ya lolote la Serikali na Tume.Kamwe...
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nimepita.....
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Nipe namba yako ya simu niuibue kwenye server ya provider wako.
   
 4. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  inabidi tu nikupe pole
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Kabisa unaonekana una agenda yako unayotaka kutuambia, ila umetumia mwanya wa uongo mwepesi!

  Sitaki kuamini kama ujembe wenyewe ndio huo ukufanya ulie na kuufuta haraka kiasi hicho!

  Tuwe na weledi ndugu zangu, jf sio chaka la wajinga wa kupimia uwezo wako!

  Pole sana! Ukiumbuka endelea kulia kwa nguvu zote!
   
 6. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ngoja niendelee kukata majani ya ng'ombe.
   
 7. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hukumaliza kusoma ujumbe ukaufuta! Ukaanza kulia! Namba iliyotuma ujumbe huijui! Hapa jamvini umepakumbukaje wakati hata ulichoandikiwa hukukisoma kujua content?
  Nakushauri mambo ya KIZUSHI hapa siyo mahali pake na usipende kutumia jamvi hili KUKUSIKITIKIA kwa UZEMBE au UONGO wako.
   
 8. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Haueleweki full. mi sujaona kilichokuliza. Au uliogopa kuona neno MAFIA? je wewe ni wajinsia gani mpaka kujisifia kulia.
  Sasa huo umamluki ukowapi hapo kwenye taarifa yako? Unamaanisha nini ukisema watoa maoni wa katiba mpya? au unamaana wakusanya maoni?

  Kama ni ndoto uliota si ungesema tu ili tujue.
   
 9. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 734
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asilimia mia moja, hiyo habar ni ya uzushi, una ajenda yako binafsi. ...Hujamaliza kusoma ukafuta na ukaanza kulia...., kitu gan kimekuliza? Kwa nini ulifuta msg? Acha hizo.
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Je ni kweli wewe ni mzaliwa wa Pwani? je wewe umesomea sheria? tuanzie hapo kwanza
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Dhaifu anatuchezeana pia, Liwalo na Liwe wanatuzingua.
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  VUTA-NKUVUTE, hiyo ilikuwa ndoto tu au maruweruwe. Jana ulikunywa nini na kiasi gani?
  Hakuna ulazima wa mtu kwenda alikozaliwa ili kutoa maoni, unaweza kutoa hata online ukiwa umekaa juu ya lindi chooni.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,273
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  We jamaa hebu acha fitna..haiwezekani uifute hiyo namba. Kwa azingira yetu tulivyo tunafowadi SMS zenye muelelekeo km huu kwa ndugu jamaa na marafiki iweje wewe ulie kisha uifute. Sasa kama umeifuta hatuna haja ya kukuamini..
   
 14. s

  sawabho JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kahawadithie watoto wenzako huko !!! Wacha kuipaka matope Tume ya Katiba, sio kila kitu ni cha kupinga. Yaani utaelekezwaje kwenda kutoa maoini Mafia ilihali wewe sio mzaliwa wa hapo Mafia ? Watu wa Mafia hawatakuona kuwa wewe sio mkazi wala mwenye asili ya huko. Halafu kwa nini umelia, kwani kuna vitisho vya kukudhuru hapo ? Kama unapewa ajira ya muda, mbona ungeenda halafu uje usaidie kufichua hiyo hujuma. Sasa ni-PM namba yako niangalie kwenye server kama umetumiwa sms ya namna hiyo !!!
   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni hadithi nyingine zile zile!!
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Jamani tumuhurumie! Huyu mtu hakufahamu MAFIA ni Wilaya, Yeye alivyoona neno MAFIA akafikiri yale yaliyompata Dr. Ulimboka kule Mabwepande. Ndiyo maana alichanganyikiwa na kuanza kulia!

  But in serious note, huu ujinga ulioleta hapa JF sio mahala pake.
   
 17. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Je ungeambiwa tutaenda Mabwepande kuhakiki wahamihaji waliotoka kigogo??leo siungefungasha kwenda kwenu Moshi!
   
 18. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ndio kwa maswali yote mawili
   
 19. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Utaendelea na msimamo wako nikija na ushahidi Mkuu?
   
 20. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Ndio kwa maswali yote mawili? nimeishia kucheka tu basi, maana inwezekana nimeuliza swali la kuchanganya ngoja niangalie Notes zangu za Darasani
   
Loading...