Jarida la Time limemtaja Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa "Mtu mashuhuri wa Mwaka 2015.
Jarida hilo limetaja mchango wake katika kutatua mzozo kuhusu wahamiaji Ulaya pamoja na mgogoro wa madeni wa Ugiriki kama moja ya mambo yaliyochangia kutawazwa kwake.
Kadhalika, jarida hilo limetaja kuingia kwa Urusi nchini Ukraine.
Bi Merkel ametoa uongozi wa busara katika ulimwengu ambao umepungukiwa, mhariri wa jarida hilo Nancy Gibbs ameandika.
Kiongozi wa kundi la wapiganaji linalojiita Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi ametajwa kuwa wa pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Donald Trump, anayesaka tiketi ya kuwania urais Marekani kupitia chama cha Republican.