Ni kichekesho serikali kusema wizi hauwezi kujadiliwa kwani umefanywa na Usalama wa Taifa. Hakuna sheria inayoruhusu Usalama wa Taifa au JWTZ kuiba.
Yaani Bunge limwagize CAG akakague shirika lililodaiwa kuiba fedha za umma, kisha serikali isema hakuna ruhusa? Katiba ya Tanzania inasema Bunge litasimamia shughuli za serikali. Ni uvunjaji wa katiba kwa serikali kukataa Bunge kukagua idara zake.
Kwa vyovyote vile, tunapigia mbuzi gitaa. Haiwezekani viongozi waliochota mabilioni ya wananchi wakajifunga wenyewe. Ni mpaka CCM itakapokaa benchi ndipo ukaguzi wa wizi uliofanywa na viongozi wake utawezekana. Najua Slaa anafahamu hivyo. Anavyouliza maswali yake, ni vizuri tu kwani ni namna mojawapo ya kuhamasisha wananchi ili wakubali kuiweka CCM benchi. Then, and only then, ukaguzi wa dhati utafanyika na wezi wa mali ya wananchi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.