Meremeta & TANGOLD Revealed!

Na wizi ni siri, hivyo kuutoa nje ni kuidhalilisha serikali-Hon.Marmo
 
Ngoja tusubili nini kitakea endeleeni kutupa news.....
 
Asante Zitto,Nakushukuru Mwanakijiji...Leo najua patachimba,

Je watakuwa na Uwezo wa kumfungia Tena?
 

Duh Mh. Zitto as daring and bold as ever...kaamua kabisa kutimiza ahadi yake ya juzi hapa,Halisi Dr. Slaa yumo pia ukumbini?na Mh. Pinda?
 
Pinda alikua Kigoma, sina hakika kama karudi!! Nimesikiliza lakini sijaangalia vyema, kwa wanaofuatilia labda watuambie kama karudi Dodoma
 
na amesema kwenye kamati ya madini ya raisi kulikuwa na watu wa kawaida /wafanyabiashara ambao hawakuwepo chini ya kiapo sasa huo usiri a usalama wa jeshi uko wapi?
 
Ukweli kuhusu MBIVU na MBICHI utaeleweka LEO !!! Heko kijana wa Chadema (Kigoma), Mh. Zitto sema usiogope kwani walalahoi wote tuko nyuma yako HASA kwa SALA !!! Mwaga nyuki rusha MAWE mpaka kielewekeee hapo BUNGENI maanake wamezoea kutudanganya HATA KAMA SISI NI WADANGANYIKA !!!!!!!!! Mwisho wa siku utaeleza na kuchambua yapi MAKAPI na upi MCHELE !!!!!
 
Muhimu kwa walio Dodoma kuweka hapa maelezo yote ya Zitto LEO MCHANA
 
Marmo atang'ang'ana na mambo yake ya "classiFISADI documnets" ili kuendelea kuwalinda majambazi yaliyovaa sura za Mkapa,Chenge,Rostam,Lowassa,Karamagi,Mgonja,Mramba na mengine...
 
Ongera Mh. Zitto. Hila pia serikali kama imeshindwa kuwashughulikia mafisadi badala ya kutumia hila kutudanganya, basi waturuhusu wananchi tuwashughulikie wenyewe. Vinginevyo itakuwa ni unyanyasaji tu.
 
tunasubiri kwa hamu kuwafahamu hao wezi, wanaoilisingizia jeshi
 
Duu, wakaieni kooni, kwani ukweli siku zote hujitenga na uongo!

Lakini pia wanajeshi tusaidieni hivi hizo hela mlizikula kweli? ama ni jeshi la wapi lililo pewa mabilioni hayo?

Come on wajeshi unajua nanyie mkiamka mkasema kweli mkaacha kubebeshwa mizigo ya mafisadi mtakuwa mmesaidia sana katika ukombozi wa Tanzania yetu bila kutumia SMG!
 
Hivi hawa wakati wanachunguza hawakuwa wakijua kwamba ni mambo ya kijeshi? Mbona walipewa maelekezo na serikali yenyewe? Na huko hawakubaini hata chembe ya "MAMBO YA KIJESHI NA USALAMA WA NCHI!" kama alivyo 'copy and paste' kaka Pinda


SOURCE: THISDAY Saturday, May 17 2008

http://www.thisday.co.tz/News/3980.html
 
Zitto alikuwemo kwenye kamati ya madini kwahiyo nina uhakika anajua anachokisema.

Pinda ilitakiwa asome hiyo report kwanza kabla ya kuingia kichwa kichwa bungeni.
 
Zitto alikuwemo kwenye kamati ya madini kwahiyo nina uhakika anajua anachokisema.

Pinda ilitakiwa asome hiyo report kwanza kabla ya kuingia kichwa kichwa bungeni.

Atakuwa ameisoma na anajuwa wazi kuwa anasema uongo. Hao majangili ni lazima washughulikiwe. Hawawezi kuendelea kutufanya wananchi kama mazezeta na wanafanya na kusema wanavyotaka.
 
Now we're pretty certain kuwa hofu za baadhi yetu kuhofia uwepo wa Zitto kwenye kamati ile hazikuwa na msingi. Bila kuwemo mengi kuhusu Meremeta yangefichwa !
 
Zitto alikuwemo kwenye kamati ya madini kwahiyo nina uhakika anajua anachokisema.

Pinda ilitakiwa asome hiyo report kwanza kabla ya kuingia kichwa kichwa bungeni.

Mkuu Mtanzania uko sahihi kabisa, hebu kumbuka hizi story: na kwa taarifa ni kwamba Kamati ya Makatibu Wakuu wote, chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, imeyakubali kwa asilimia 100 mapendekezo ya Kamati ya Rais ya Madini, likiwamo la kuifanyia uchunguzi Meremeta na hatua kuchukuliwa. Sasa Pinda anakurupuka kama alivyokurupuka Mkulo kuhusu EPA. lakini sishangai, hayo ni mapendekezo/maamuzi/usanii wa vikao vya CCM ambavyo Mkapa aliibuka na kushiriki na sasa mambo yote yanayomhusu Mkapa nasikia harufu ya kuyasafisha!!!! Watanzania wa leo si wale wa enzi zake bwana Mkapa, ambao alikua anawafokea waandishi wanaokemea rushwa kwa kuwahohi kwamba, "na wao waseme wamepata wapi mitaji yao"


SOURCE: Thisday: Tuesday, June 03 2008

http://www.thisday.co.tz/News/4076.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…