Meremeta, CIS, Escrow na Lugumi: Kashfa kabambe zinazodhihirisha uwepo wa Genge la Mafia nchini

HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
2,212
1,552
Habari wanaJF,

Ninaandika thread hii nikiwa na uchungu mkubwa moyoni jinsi umasikini ulivyokithiri nchi hii ilhali kuna manyang'au wachache nchini waliotugeuza mabwege tulio wengi kwa kutuibia kila uchao tena mchana wa jua kali.Tena majizi haya yanaiba bila ya hofu ya kuhojiwa wala kuwajibishwa.Mfululizo wa kashfa za wizi nchini ni mikakati thabiti ya nyang'au hawa.

Miongoni mwa kashfa kubwa zilizotikisa nchi ni mradi wa MEREMETA;hapa tulipigwa mabilioni ya fedha na dhahabu yetu ya Buhemba ikasombwa na majizi yanayofahamika kwa majina.Kashfa hii 'ikauawa' kwa kisingizio cha usalama wa Utaifa.Ikaja kitu kinaitwa ICS (Intensive Commodity Support).Hapa nako mabilioni ya fedha 'hayajulikani yalikokwenda'.Wajanja wamenyuka hizi fedha na hakuna wa kuhojiwa.Ikaibuka kashfa kabambe iliyozua 'kasheshe' Bungeni na taharuki kwa Watanzania wengi.

Ni kashfa ya Escrow.Hii kashfa imedhihirisha wazi kabisa kwamba mifumo yetu ya utawala na utoaji haki IMEKUFA.Kashfa hii ambayo kimantiki ni UJAMBAZI wa dhahiri kabisa,pamoja na watawala wetu kutaka 'kulifunika',bado ni mbichi mno.Sote tunafahamu hapa jinsi jinsi wanaoitwa waheshimiwa walivyogawana mapesa kama karanga zisizo na mwenyewe.Kwa sasa kuna kashfa nyingine inayofukuta,ni kashfa ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi.

Na katika suala hili dana dana zimeshaanza kama kawaida.Kila Taasisi inasema lake.Kamati ndogo ya bunge imeundwa kuchunguza suala hili.Na mantiki yake hapa napata tabu kuielewa kwani vyombo vya kiuchunguzi.Niharakishe kutamka hapa kwamba SITARAJII JIPYA katika hiyo kamati.

Hizo ni kwa uchache tu,lakini kashfa ni nyingi mno.Wizi huu kwa hakika unaratibiwa kwa ustadi mkubwa na wahusika.Ni mkusanyiko wa maharamia dhidi ya mfumo wa utawala wanaopanga na kuratibu mikakati ya kuibia nchi.Ni mikakati ya KIMAFIA dhidi ya umma.

Hili ni GENGE LA MAFIA la hapa nchini.Limeshateka mifumo yote muhimu:mfumo wa kisiasa,mfumo wa uchumi na mfumo wa sheria.Genge ndilo linaloyumbisha nchi,ndilo linalompa hali ngumu Rais Magufuli. Siku yaja nitalielezea kiundani genge hili.

Naomba kutoa hoja.
 
Hivi pale Buhemba walichimba kiasi gani cha dhahabu na chenye thamani gani?Kuwa makini sana
 
Hapa mwisho ndio sijakuelewa genge hili la mafia au kwenye sakata la Lugumi.

Zipo nyingi hizo kuna EPA, Richmond,buzwagi na nyenginezo upepo umetupita tumesahau
 
ni ajabu kupiga kelele kuhusu LUGUMI, ESCROW na hata ICS huku ukifumbia macho EPA na RICHMOND.

Wakati mwingine inatubidi tuwe wakweli pale tunapopigania maslahi ya nchi hii. Masakata ni mengi sana tena ambayo yanatambulika kuliko hata hili la Lugumi.

lakini cha ajabu mtu ambaye kwa madai yake anasema anauchungu na nchi hii juu ya pesa inayopigwa na GENGE analoliita la MAFIA, Kushindwa kutaja mengi anayoyajuu juu ya UFISADI wa Nchi kwa kuwa wahusika wa hayo madudu mengine ni Watu anaowashabikia ama anaojuana nao.

UKWELI KAMA TUNASEMA TUNAUCHUNGU NA NCHI HII LAZIMA TUPIGANE NA WOTE BILA KUJALI HUYU NI NANI NA YULE NI YUPI. Tusipofanya hivyo tutakuwa ni wanafiki wa kubwa
 
Dawa ni kuichomoa ccm madarakani lakini kusema kwamba eti jpm apambane nao wakati na yeye ni zao la ccm na ndio waliomweka madarakani ni ngumu
 
ni ajabu kupiga kelele kuhusu LUGUMI, ESCROW na hata ICS huku ukifumbia macho EPA na RICHMOND.

Wakati mwingine inatubidi tuwe wakweli pale tunapopigania maslahi ya nchi hii. Masakata ni mengi sana tena ambayo yanatambulika kuliko hata hili la Lugumi.

lakini cha ajabu mtu ambaye kwa madai yake anasema anauchungu na nchi hii juu ya pesa inayopigwa na GENGE analoliita la MAFIA, Kushindwa kutaja mengi anayoyajuu juu ya UFISADI wa Nchi kwa kuwa wahusika wa hayo madudu mengine ni Watu anaowashabikia ama anaojuana nao.

UKWELI KAMA TUNASEMA TUNAUCHUNGU NA NCHI HII LAZIMA TUPIGANE NA WOTE BILA KUJALI HUYU NI NANI NA YULE NI YUPI. Tusipofanya hivyo tutakuwa ni wanafiki wa kubwa
Mkuu,mimi ni mwananchi wa kawaida mno,hao unaodai nawashabikia au kuwajua,NAWAONA NA KUWASIKIA TU kwenye vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom