Mengine yaanikwa kampuni ya Bakhresa

Mengine yaanikwa kampuni ya Bakhresa

Watanzania huwa tuna roho ya kwa nini sana. Unakuta mtu ana uwezo kuliko wewe lakini ana kuonea wivu na kidogo unacho pata. Sasa huyo meneja ana sababu gani ya kuto waongezea hao wafanyakazi pesa kama maagizo yametoka kwa mmiliki mwenyewe? Mtu unajidai kuwa mbahili na pesa ambazo hata si zako? Pesa stahili kwa mwenzio?
 
Ninavyomuelewa Bakhressa ni mtu makini, mcha Mungu na anayeguswa na matatizo ya watu walioko chini yake.
Matatizo ya kijinga kama haya ya kuletwa na wasimamizi yanaweza kabisa kuharibu tashwira ya kampuni na kuvuruga kasi ya maendeleo.
Mimi pia namshauri amsimamishe, amchunguze na amwondoe haraka kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Sina uhakika kama akina Petro na Paul wanafanya kazi hapo.
 
Please omar bakhessa n yusuf bakhressa ongeeni na mshua wenu. Kuna watu (the likes of Mbacha) wanaharibu image ya kampuni zenu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndiyo maana bongo karibia kila mtu mwizi halafu ufisadi ni sifa!

80,000 kwa mwezi hapo Dar mtu anaishi vipi?Tena amefanya hapo kwa miaka 15?Ama labda kuna other benefits?

Kuna watu wanaishi hiyo bongo umayoisema na hawana kazi ww unashangaa mtu anayelipwa 80,000?
 
Pole mliofukuzwa kwani hapo hamna labour union ya kuwatetea wafanyakazi? Tunashukuru serikalini tuna tughe inatutetea
 
Ndiyo maana bongo karibia kila mtu mwizi halafu ufisadi ni sifa!

80,000 kwa mwezi hapo Dar mtu anaishi vipi?Tena amefanya hapo kwa miaka 15?Ama labda kuna other benefits?

labda kuiba sukari, hamira kidogo mifukoni. Ndiyo maana maji feki ya Uhai yamejazana mitaani..wafanyakazi hao hao wanapitisha chupa ili kujaziliza vipato
 
Kuna watu wanaishi hiyo bongo umayoisema na hawana kazi ww unashangaa mtu anayelipwa 80,000?

huwezi kuishi dar kama huna kazi ya kufanya-kukuingizia kipato...labda tafsiri yako ya kazi ni lazima mpaka mwisho wa mwezi upewe salary slip.
 
Kuna watu wanaishi hiyo bongo umayoisema na hawana kazi ww unashangaa mtu anayelipwa 80,000?
Mimi nazungumzia wenye kufanya kazi na ambao wame earn the right to get paid.Joblessness ni another topic.Sawa wakusoma?umenisoma?
 
Halafu tunaambiwa huyu ndiye tajiri namba moja Tanzania.
 
Watanzania wanaonewa kwenye nchi yao .. Hakuna haki.. Hakuna pa kukimbilia .. Hadi tembo nao hawana pa kukimbili labda waende kenya

Pamoja na yote Watanzania ni wapiga porojo sana kazini tofauti na majirani zetu hapo kwa UhuRuto,hufanya kazi kwa mazoea,kila siku ni kusingizia kuumwa au kufiwa kumbe ni janja ya kuwahi kwenda kufanya mambo ya kibnafsi
 
Afadhali maana nilijua huyu mzee muungwana mtoa sadaka leo anawadhulumu wafanyakazi wake
 
wenyewe kwa wenyewe.....

Mkuu ni kweli kabisa! Ni wenyewe kwa wenyewe! Ndio maana tunasema siku zote ufisadi hauni dini wala kabila! Adui namba moja wa watanzania ni CCM. Haijalishi kama inaongozwa na rais Mwiislam au Mkristo. Tuungane bila kujali dini zetu tuiondoe!
 
Sina uhakika kama akina Petro na Paul wanafanya kazi hapo.

... Ahaaa! Unaandikia mate, wakati wino upo!
... Marko, Jesca, Yohane, Grace, Mathayo, Elizabeth, Timotheo, Anna, Tito, Mary, n.k HAWANA NAFASI...
Hii ni kwa sababu mwajiri alikuwa anapata shida kutamka majina hayo!
...Ukienda kuomba kazi huko jitambulishe kwa majina ya kimashariki mashariki ya kati...., wala hakuna haja ya kuwa na vyeti vya Elimu yako' sana sana jitahidi kuvaa kivyao vyao...
 
Duh,

Bakhressa si ndio tajiri namba moja Tanzania? halafu anafanya haya mh kweli kuwa tajiri na kuingia peponi ni vitu viwili tofauti. Sasa kama mtu anadhulumiwa mafao yake si uonevu huu. Mafao ni haki ya kila mfanyakazi nchini. Kama ni kweli basi Bakhressa una la kusema kwa muumba kama ni uongo dhidi ya washindani wako pole sana.
 
Watanzania wanaonewa kwenye nchi yao .. Hakuna haki.. Hakuna pa kukimbilia .. Hadi tembo nao hawana pa kukimbili labda waende kenya

Lakini kama mshahara ni mdogo na huriziki nao si unaacha kazi??? au ndiyo kusema na yenyewe tudai maandamano? hoja ya kwanini wakenya aui wahindi imepitwa na wakati kwani swala hapa ni ufanisi kazini? wtz tupo hovyo sana na tunarizika kienyeji sana .
 
Back
Top Bottom