Mengine aliyofunguka Nape baada ya kutoka kwenye uwaziri!!!

proskaeur

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
1,571
4,925
Habarini wanabodi…!!!

kupitia habari ya Azam Two ya April 20, 2016 aliyekuwa waziri wa habari ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama , Nape Nnauye amekiri kuwa kuondolewa kwake kwenye nafasi ya uwaziri kuna maswala mengine na hakuna atakayethubutu kuyaongelea yote yaliyomsababisha kutokea kwa jambo hilo.

Nape amezungumza na mwandishi wa habari wa Azam Two na kusema kuondolewa kwake katika wadhifa huo kulisababishwa na maswala aliyokua akiyasimamia na misingi ambayo anaiamini, hivyo asingependa kwenda kinyume kwa hicho anachokiamini na hakushtushwa na maamuzi yaliyochukuliwa na mteule wake…!!!

Chanzo:millardayo.com
 
Kumbe hii habari ni ya mwaka ulopita? Lakini tukio la Nape kufukuzwa uwaziri lilifanyika mwaka huu 2017.
Lakini nimeelewa ulichomaanisha
 
Kumbe hii habari ni ya mwaka ulopita? Lakini tukio la Nape kufukuzwa uwaziri lilifanyika mwaka huu 2017.
Lakini nimeelewa ulichomaanisha
Sorry nimekosea mwaka,,, ila nashukuru kwa kunielewa……!!!
 
Back
Top Bottom