Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Kuendelea kucheza kwa kiwango cha chini kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendela Zanzibar kwa mabingwa zamani wa mashindano hayo kumeibua mambo mengi kutoka kwa baadhi ya wadau wa mchezo huo hapa nchini.
Licha ya kuchezesha kikosi cha kwanza kinachojumuisha wachezaji wao wa kimataifa team hiyo imekuwa ikishindwa kuonyesha kiwango kizuri na matokeo yake kupata ushindi kiduchu kwenye michezo yake.
Simba imeteremka mara 2 kwenye mashindano hayo na kushinda 2-1 na 1-0 dhidi ya team dhaifu za Taifa Jang'ombe na KVZ respectively, huku ushindi wa jana dhidi ya KVZ ukilalamikiwa kuwa haukuwa halali kwakuwa walifunga goli la Offside.
Mdau mmoja wa mchezo huyo ambaye amekuwa akihudhuria match zote za mashindano hayo alisikika akiuliza inakuwaje Simba inayocheza kiwango kibovu hivyo kuongoza Ligi kuu ya Bara ambayo Zanzibar nzima wanaijua kuwa ni ngumu.
Bwana Mohamed Fakhi wa Kibandamaiti naye alisikika akilalamika kutomuona mchezaji anayeongoza kwa kuzifumania nyavu kwenye ligi kuu bara, na kulaumu team hizi kubwa za Bara kwa kudharau haya mashindano na kuwaacha wachezaji mihimili Dar. Hata hivyo alipothibitishiwa kuwa mfungaji huyo muongozaji anayekwenda kwa jina la Shiza Kichuya yupo na amecheza match zote alipigwa na mshangao mkubwa kwa kutoona vitu vyake ambavyo amekuwa akivisikia anavifanya huko kwenye Ligi ya Bara.
Aidha wadau wengine walifika mbali na kuzitaka mamlaka husika kufuatilia mwenendo wa team hiyo kwenye ligi kuu ya mwaka huu Bara wakitilia mashaka matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata ambayo kihalisia hayafanani na kiwango chao halisi cha uwanjani, "kwa namna Simba walivyopania kumaliza ukame wa kutwaa ubingwa wa Bara,huenda wakawa wanatumia mbinu mbadala za kuwawezesha kufanikisha hilo.
Haiwezekani team ikawa na kiwango duni hivyo kama inavyothibitika uwanjani hlf ikawa inaongoza Ligi" alisikika akilalamika mdau mwingine ambaye hoja yake iliungwa mkono na Mshabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina 1 la Ahmed ambaye alisema kwa kiwango hiki hata Simba ingekuwa inashiriki ligi kuu ya Zanzibar inayojulikana kuwa ni nyepesi isingeweza kuwa hata kwenye Top 3.
Naomba kuwasilisha.