Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Duuh!mwalimu wako wa hesabu alikuwa nani? Una uhakika kama 1sq.km ni sawa na 1000sq.m,? hayo ndo matatizo ya kukurupuka kutetea hoja! Wewe na muhongo wako wote ni wazushi.
 

Hii ni Makala, Taarifa au Habari? Very Dunce! You're boring and Next time Please observe Brevity in Writting.
 
Mengi ni wa kupuuzwa tu. Alikuwepo kwenye kongamano na alitoa mada. Kwanini hakujibu pale pale anasubiri akafiche na kurekebisha data kwanza. Mfu tu huyo hana mpya

Kuwa mkweli na nafsi yako ishuhudie kuwa unaongea ukweli. Muhongo aliwasilisha mwishoni na baada ya hapo hakukuwa na fursa ya kuchangia presentation yake. Nilimuona mzee Mengi akuhangaika sana kumuomba mwenyekiti aongeze muda ili hoja alizoongea waziri zijibiwe, mwenyekiti wa ule mdahalo akapotezea. Na baada ya presentation tu Muhongo aliondoka mara moja, Mengi angejibu saa ngapi hapo?

Mimi nitawalaumu UDASA, walipaswa kuhakikisha kuwa waziri anapresent mwanzoni ili presentation yake ijadiliwe. Kuna mambo mengi ambayo waziri aliyasema na yalihitaji mjadala mpana. Lakini pengine walifanya vile kwa maslahi ambayo wenyewe UDASA wanayajua!
 

Inasikitisha sana! tuombe wasitufanyie madudu haya kwenye gesi
 
Prof Muhongo anatekeleza sera za chama kwahiyo ametumwa na ccm kufanya anayofanya. Mengi ni kada maarufu wa ccm. Hizi personal attack zinatoa tafsiri gani kwa watanzania walioipa ccm ridhaa ya kuongoza?

It doesnt matter who is right and who is wrong, who wins and who loose. Watanzania tunachotaka ni maendeleo siyo malumbano period.

Ingekuwaje kama Mengi angekuwa cdm??
 

Kwakweli hili lilikuwa ni kosa kubwa katika lile kongamano.Nafikiri watakuwa wamejifunza kupitia tukio hili.
 
Mengi nae muongo mbona haja sema mgodi wa madini ya dhahabu anaomiliki mkoani tanga! Anasema ana tanzanite tu!
Mengi anataka kuumbuliwa zaidi na Profesa
 
Asante Mkuu kwa taarifa

Ila kwa data hizo, japo inaonyesha ameingia ubia yaani JV, lakini kwa takwimu hizo tu zilizo kwenye link hapo juu, anakaribia sawa na mkoa wa Dar es Salaam, yaani sq. km 1800!
 
Hallow mimi nilikubali speech za prof. Ni kweli tanzania inaumizwa na watanzania kwani mengi katika speech yote ya prof. Ameona la kujibia ni hili la dar es salaam tatu?vipi kuhusu zile gharama za uwekezaji anazimudu?watu wampatie?mimi naona mengi ni walewale tu kulilia maslahi yake,kwani akipewa nafasi katika gesi ni maisha yake au ya watanzania?na hilo eneo analomliki ni maisha yake na watoto wake na klyn au ya watanzania.
 
Mengi nae muongo mbona haja sema mgodi wa madini ya dhahabu anaomiliki mkoani tanga! Anasema ana tanzanite tu!
Mengi anataka kuumbuliwa zaidi na Profesa


Nimejitahidi sana kufuatilia hoteli aliyeijenga huyu bwana baada ya kuikosa Kempiski sikufanikiwa kuiona, sijui alikua na nia gani katika hili.
 

Dar es Salam moja ni 1800sq km, ukizikunjua mara tatu ni zaidi ya hapa hadi Chalinze hivi, sasa mmmh, ni eneo kubwa, nani mkweli nani mwongo inakua shida kuupata ukweli!
 
Ila kwa data hizo, japo inaonyesha ameingia ubia yaani JV, lakini kwa takwimu hizo tu zilizo kwenye link hapo juu, anakaribia sawa na mkoa wa Dar es Salaam, yaani sq. km 1800!

Asante Chaza kwa maelezo ... JMali amechangania na his findings ni kwamba jamaa ana around 1200sq km na dar iko 1800sq km hizi ni kampuni za madini tu I would like to know Dr Mengi anamiliki aridhi kiasi gani yeye na makampuni makampuni ambaye yeye anaubia
 
Mengi ni mlafi wa kupindukia,he is next to Rostam for his worthness but still exploiting his employees and not paying their salaries at regular and right time !....analilia uzawa?....

Hichi kitu nimekisema kitambo tu....
Hawa matajiri wetu kwakweli hamna kitu, ndio maana mimi huu wimbo wa "uzalendo" na "uzawa" kwa hawa matajiri wetu wala siwezi kuimba nao pamoja....
Vikampuni vya Mengi vipo vizuri sana kwenye unyanyasaji wa wafanyakazi.... Tujikumbushe case Rehema Mwakangale (RIP).....
Sina hoja za kumtetea Mengi!!
 
KAma Muhongo kasema Uwongo, kwa kutumia "Facts and Figures" kuukanusha uongo wake inabidi kutumia hizo hizo.....supporting evidence hapa ni ipi? Kusema tu "nina sq km moja haitoshi
 
Dar es Salam moja ni 1800sq km, ukizikunjua mara tatu ni zaidi ya hapa hadi Chalinze hivi, sasa mmmh, ni eneo kubwa, nani mkweli nani mwongo inakua shida kuupata ukweli!

Mkuu kama unavyosema shida ni kuthibitisha ni nani mkweli kati ya Muhongo na Mengi!

Mimi nadhani baada ya Mengi kukanusha taarifa zilizotolewa na Muhongo mbele ya waandishi wa habari, angekwenda mbele zaidi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Mh. Muhongo kwa kutoa taarifa za kupotosha ambazo bila shaka zimemchafulia jina lake.

Naona hii ndiyo njia sahihi ya kuwaonyesha wananchi ukweli kuhusiana na hili swala!
 
Duuh!mwalimu wako wa hesabu alikuwa nani? Una uhakika kama 1sq.km ni sawa na 1000sq.m,? hayo ndo matatizo ya kukurupuka kutetea hoja! Wewe na muhongo wako wote ni wazushi.
Nashukuru kwa kuwa umeelewa nilichokuwa nataka kumanisha sio kosa lako mpo wengi wengine wamesema jana kikwete aliongea broken as if yeye ni malaika mnajua sana kuyaona ya wenzenu ila nyie ya kwenu ni ya malaika
 

Si-ha-sa..........wacha kujipa presha umethibishaje kuwa Mengi yeye ni mkweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…