kiongozi; naomba ukumbuke kuwa ukiwa na ungo (setelite dish) huna haja ya kingamuzi labda upende mwenyewe. Kingamuzi ni shs 39,000,kwa bei ya promosheni.
Mimi najua kuwa huu uamuzi umekuja mapema ila pia naona wamelazimika kwa kuwa nchi za ulaya zote zimezima analalogia, sasa sisi tusipozima tutageuka kuwa soko la takataka zote za ulaya na mara tutakapozima wananchi wa tanzania wangepata hasara sana kwani tayari wangekuwa wamenunua vitu mbali mbali vya analogia kutoa ulaya.
Kwenda digital, nigharama mwanzoni ila tunakoenda utakuja kufurahia sana faida zake muda mfupi ujao. Mfano, bei za simu zitashuka zaidi (umejaribu kutumia airtel tel ukaona unafuu wa bei?) Kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine itakuwa karibu sawa, hivyo hutakuwa na haja ya kuwa na laini nyingi.
Utaweza kuangalia TV kwenye sim yake picha safi na sio zile simu za kichina zinazo onesha mchele mchele.
Kamani mpenzi wa michezo, unaweza kuweka vocha kingamuzi chako ukaangalia kwako na michuano ikiisha ukabaki na chaneli zako za bure.
Nafikiri kwa huo mchango wangu unaweza kuona mwenyewe kuwa kikwete amelazimika kufanya hivyo ili kuepusha nchi yake kuwa dampu la takataka za ulaya