Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 56,591
- 30,426
Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano
*Abainisha hana ndoto za kuwa mwanasiasa
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi, amesema limejitokeza kundi la mafisadi waongo na vibaraka uchwara, wanaomvumishia kuwa anajijengea umaarufu wa kisiasa, tayari kwa kugombea uongozi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao.
Bw. Mengi amesema kundi hilo la watu waovu, wanataka kuharibu uhusiano wake na viongozi wa kisiasa nchini.
"Nia yao ni kuhakikisha kuwa ushupavu na uadilifu wa wale wote wanaomuunga mkono Mhe. Rais katika vita dhidi ya ufisadi, wanadhoofishwa na wakati huo huo mizizi ya ufisadi, inajichimbia zaidi na mafisadi wanajijenga zaidi na kuimarika," alisema Bw.Mengi kupitia katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Alisema mafisadi hao wanadiriki hata kusema kuwa vyombo vya habari anavyovimiliki na vinavyopiga vita ufisadi, ni adui wa nchi na vinataka isitawalike.
"Sasa tujiulize, adui wa nchi ni yupi, ni yule anayetetea na kulinda mali za nchi yetu au ni yule anayezipora. Je anayetaka nchi yetu isitawalike ni yule anayepora mali ya umma na yule anayepiga vita uporaji wa mali ya umma ?" Alihoji Bw. Mengi.
Aliwaomba wananchi wenye nia njema na nchi yao, wawapuuze mafisadi na waongo, badala yake waongeze nguvu katika vita dhidi ya ufisadi.
Alisema binafsi ameridhika na biashara zake na kwamba anaunga mkono kauli ya Rais kuhusu umuhimu wa kutengenisha shughuli za kibiashara na uongozi wa kisiasa.
"Vile vile naomba ndugu zangu Watanzania waone kwamba heka heka hizi za mafisadi na waongo, zina nia mbaya na ni fitina zenye nia ya kujenga chuki na kuvuruga nchi," alisisitiza ,Bw. Mengi kupitia katika taarifa yake ya kurasa mbili.
Aliwashauri wale aliowaita kuwa ni mafisadi, kuacha fitina za kueneza chuki baada ya kupora mali za umma na kwamba wasitumie nguvu za ufisadi wao kupora amani ya nchi.
"Nawashauri warudishe mali za umma walizopora, waombe ushauri wa viongozi wao wa kiroho, watubu uovu wao na waombe msamaha," alisema.
Alisema litakuwa jambo la kushangaza kuzungumza juu ya kumsamehe yeyote yule wakati mamilioni ya ya fedha yaliyoporwa yamehifadhiwa katika mabenki ndani na nje ya Tanzania wakati wananchi wanakosa fedha za kununulia dawa.