Mengi alia na mafisadi; na yeye achunguzwe!

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,951
2,000
Mengi ananikumbusha alivyo teleza Mwakyembe kuwa kuna mambo wameyaficha kulinda heshima ya serikali sasa Mengi naye anaficha kutaja majina ya mafisadi analinda heshima zao....duh sasa si wananchi tumsaidiaje hapo??
 

Haki.tupu

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
254
195
Mimi nadhai Mengi anaonewa kwa hili! Apeleke wapi kesi yake, serikali yenyewe ndio inayowalinda mafisadi! Apeleke police ipi! Mzee wa watu amepiga sana kelele ya mafisadi kupitia mdomo wake mwenyewe na kupitia magazeti yake (hasa thisday na kulikoni).

Watu wanaacha hoja wanaishia kumtuhumu anavita na wafanyabiashara wenzake! Hata kama ana vita kinachosemwa kuwahusu hao akina Manji nk si ni cha kweli wameiba NSSF nk! Si na hao wafanyabiashara wengine wafichue siri za Mengi! Huyu mzee angekuwa na kashfa za maana zingefahamika mapema sana, maana ana maadui wa kumtosha.

Mimi namwona mengi ana courage sana ya kujitetea! Hajali kutofautiana na mtu (hata kama ni nani!) Watu wengi wanaonewa lakini wanakufa na tai shingoni! Mimi nadhani anajitahidi sana kusimamia haki yake. Suala la udhaifu, wake liongelewe kama mada nyingine!

Mengi achunguzwe! Halafu report ya uchunguzi apewe nani? Maana hata polisi TZ nao wanaishia na report ya uchunguzi sio mashtaka linapokuja suala la wakubwa!

Mwacheni Mengi apigane na mafisadi kwa staili yake na wengine nao wapigane wanavyoona inafaa.
 

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
1,225
Kuhusu Mengi huwa ndio tabia yake, wakati anaanzisha ITV, wakati ule kulikuwa na TV zilizokuwa chini ya Wadosi. Akasema ametishiwa maisha kwa kuanzisha ITV. Akapewa ulinzi. Likaja sakata la kuuzwa Kilimanjaro Hotel, akashindwa, sijui mchakato ulikuwaje, akahamia kwa wananchi. Wakati huu akisuguana na Masilingi na kusema Masilingi amemtishia maisha.

Ilipokuja suala la Manji akahamia tena kwa wananchi. Lakini huwa anapata huruma yetu manake ni mtoa misaada huku vyombo vyake vya habari vikimfagilia kwa muda mrefu (huwa anapewa muda na vyombo vyake mrefu hata kama kuna matukio muhimu).

Sasa anakuja na jingine, sijui nani wanavutana katika biashara, tusubiri karibia atashusha bomu kwa mwingine. Ila yeye ni ushindani wa kibiashara, akishindwa hutafuta kitu apate huruma za wananci.
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,527
2,000
Wakuu sikilizeni. sikubaliani na wale mnaosema kuwa Mengi anatafuta Majority support or Sympathy toka kwa Wananchi. Afadhali yeye anahusisha wananchi kwa kuwa amekuwa akifanya mambo mengi ya kijamii mazuri bila kujali dini wala cheo cha mtu. Hana haja ya kutaja mafisadi kwa kuwa magazeti yake yametaja mpaka yamechoka na wengine walitaka kupeleka vyombo vyake vya habari mahakamania na wakaogopa kwa sababu wanajua Mengi ana editors na wanahabari mahiri (they do researched journalism and reporting). Unataka kuniambia kuwa Manji na Rostam ambaye ni big friends wa Jk na system yake wanampenda mengi? Kwanza wanataka business wise awe na downfall!!! Kila binadamu ana mapungufu yake, ila Mengi hajawahi kuwa FISADI. Kilichotufikisha hapa tulipo na maisha magumu ni RICHMOND, IPTL, EPA, MWANZA POWER GENERATORS AMBAZO HAZIJAWAHI KU GENERATE HATA MEGA WATT 1 NA IMELIPWA, KIWIRA, DEEP GREEN, MEREMETA, MIKATABA MIBOVU YA MADINI AND OTHER NATURAL RESOURCES INCLUDING UWINDAJI HARAMU NA USIO NA TIJA KWA FAIDA. Jamani list haitakwisha. Sasa Mengi akiandika yote hayo kupitia This Day, Kulikoni and other papers anazohusiana nayo huoni kama wahusika ambao wote mnajua fika ni hatari wanaweza hata kumdhuru Mengi? Kwanza ana bahati sana, Mungu wake anampenda, maana wengine wanatamani hata angekufa!!!! unafahamu ni vitisho vingapi ameshatumiwa yeye na wahariri wake? Fikiri kwanza kabla hujaandika, do a bit of analysisi first. Thanks.
 

Haki.tupu

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
254
195
Kwa kweli... Huyu mzee anaheshimika lakini amekuwa na tabia fulani ya kutuweka Watanzania upande wake kila akizungumzia matatizo yake na wafanyabiashara wenzake!!! Nakumbuka hata wakati wamepelekana mahakamani na Manji alipohojiwa alikuwa anajiunganisha na Watz kana kwamba tunajua bifu lao. Nimemfuatila kwa muda mrefu ni mtu anayetafuta public sympath siku zote.

Itabidi naye achunguzwe, mbona kodi alizokwepa watu wanaelewa na hawasemi? au tuanike uozo wake hapa Jf? Nadhani hajawa msafi kiasi cha kujiunganisha na watanzania kana kwamba tuna vita moja na yeye!

Sio kweli hata kidogo!!!! Na wewe kwa maana moja au nyingine ni.....

Kwa jinsi watanzania tunavyoishi bila kufuate sheria, unaweza kukuta kila mtanzania alitakiwa awe jela kwa idha kukwepa kodi (hata mmachinga na mama ntilie) au kuendesha gari bila kufuata sheria!!!!

Kwa nini unamfichia mengi siri! Toa hizo data, naye ajumuike kwenye list ya mafisadi kama anastahili! Kwa kutokutoa siri za Mengi kama unazo nawe unaweza kujikuta unalea ufisadi!
 

Fugwe

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,676
1,250
Nitamtambua Mengi kuwa anasaidia wananchi wakawaida kama atafanya kitu kinachoitwa au kuepuka 'Nepotism'. Kwani misaada yake si anaielekeza kasikazini maeneo mengine hawajwahi hata kunusu senti ya Mengi. Wakuu niambieni kanda ya Magharibi wamenufaika nini na utajiri wa Mengi? yeye aendelee kufaidisha maeneo fulani fulani kwa sababu anazozijua yeye. Kwa hilo ameteleza
 

Fisadi Mtoto

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
639
195
Mengi anasumbuliwa na unafiki na wivu kwa wengine wenye umaarufu na mafanikio ya kibiashara, kumbuka jinsi ambavyo RPC Maji alivyofukuzwa kazi kisa ni Mengi ambae alijaribu kudai Dewji akae jera kwa madai kuwa alipanga kumuuwa,Maji akaona haina uzito akampa mdhamana.matokeo yake Maji akafukuzwa kazi kwa malalamiko ya Mengi...Mengi anadai mafisadi waombe radhi kwa Mungu wao...Mungu aangalii dhambi ya aina moja.....yeye keshamuomba radhi mkewe kwa kumtekeleza na kwenda kufanya udhinifu na Madame Ritha,..ni aibu kwamzee kama yeye kujifanya anashindwa kuishi na mke wake na kukaa na wanawake,sisi wakristu hii ni laana.
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Huyu Mengi ni wa kupuuzwa tu hana jipya kila siku wimbo wake ni ule ule tu kimasomaso mwanagu msimuone! Tutajie halafu sisi tutamalizana nao hapa ndegeres!
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
...bora ya Mengi ambaye practically kutokana na biashara zake amesaidia familia nyingi sana through ajira na analipa kodi na kutuletea services nyingi tuu,impact ya Mengi ni kwa maelfu for the better....akifilisika msifikiri he'll go down by himself ni wengi watahangaika sana,i respect mengi kwa anayofanya ingawaje naona mmeanza kumponda eti its all publicity,waulizeni ambao watoto wao wanakula na kwenda shule kwa ajira za mengi ndio mtaelewa,hope tungekuwa na Mengi wengine maelfu tungeendelea sana...heshima mbele kwa watu kama kina Mengi sio wanasiasa uchwara wa CCM ambao ni kulinda maslahi yao tuu na matumbo yao!

Mengi analipa kodi? Are you sure?
 

Pundamilia07

JF-Expert Member
Oct 29, 2007
1,439
1,225
Reginald Abraham Mengi,

Kama anayoyaongea ni ya kweli basi ajibu maswali yafuatayo kuhusu fedha za SKUVI:

1. Je alipokea fedha hizo kutoka wapi?

2. Alipokea kiasi gani?

3. Aligawa kiasi gani na je orodha ipo?

4. Je ni kiasi gani tayari ambacho kilirudishwa?

Kama taweza kujibu maswali haya basi nitajua jamaa ni msafi kweli.
 

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,503
1,225
Kumbe sikuwa peke yangu......!

Au angalau angetujulisha hayo waliyomfanyia hata aseme wanataka kuvuruga amani then we (Tanzanians) ndo tujaji kama ni mbinu za kuvuruga amani au ni personal issues zao yeye na wao. Kuna kilichofichika hapa

Sijui pengine amekisema sikukisikia. mimi huwaga nabadilisha chanel mara awekwapo huyu maana akianza kuhutubia basi wimbo unaanza chanel 5 na kuisha bado akiongea..... anabore sometimes.!

Huyu Mzee AMezoea sasa huruma ya watanzania..Alafu Mod hii mara ya pili unabadilisha jina la thread yangu.

Uwe unaanzisha basi wewe thread au kama vipi tuwe tunakutumia habari then unachagua kichwa cha habari..


Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Mzee Mengi ni chui aliejivisha ngozi ya kondoo, ni silent killer wa wafanyaiasara wenzie kila akizidiwa kete hutumia vyombo vyake kuwamaliza wenzie na haraka anakimbilia kwa wananci kuomba huruma yao.
 

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Nitamtambua Mengi kuwa anasaidia wananchi wakawaida kama atafanya kitu kinachoitwa au kuepuka 'Nepotism'. Kwani misaada yake si anaielekeza kasikazini maeneo mengine hawajwahi hata kunusu senti ya Mengi. Wakuu niambieni kanda ya Magharibi wamenufaika nini na utajiri wa Mengi? yeye aendelee kufaidisha maeneo fulani fulani kwa sababu anazozijua yeye. Kwa hilo ameteleza


Mawazo Haya Yanakatisha Tamaa Sana...Fedha Ni Za Kwake Mengi Mwenyewe Bado Mnataka Kumpangie Azigawe Vipi..!!
 

Kandambili

Member
Aug 5, 2008
84
0
Wengi wanajua ndiko aelekeako hasa haya mambo ya kijipublicise kwa kila afanyanyacho kwa jamii

Huyo Mengi naye kazidi kulalamika, kwani hata mtu ukitaka kugombea ndio unajenga uadui, ANATAKA SANA Sympathy za watu huyo.
Mwenyekiti mzima unaenda mahakamani kusikiliza hukumu ya moja ya kikambuni chako na mtu mwingine?
Mimi binafsi huyu mzee huwa simuelewi, nakumbuka kuna wakati alikuwa mdaiwa sugu wa NBC wakati mule sijui kama alilipa madeni yake huyo?
 

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Mzee Mengi ni chui aliejivisha ngozi ya kondoo, ni silent killer wa wafanyaiasara wenzie kila akizidiwa kete hutumia vyombo vyake kuwamaliza wenzie na haraka anakimbilia kwa wananci kuomba huruma yao.


Mengi Anafanya Biashara Kwa Misingi Ya Kibepari...Mwenye Kuweza Kushindana Naye Ajaribu Kama Walivyofanya Clouds FM, Wao Wameweza; Kama Wengine Hawawezi Wanaweza Pia Kufanya Biashara Zingine Tofauti Na Zile Anazofanya Yeye...Mbona Biashara Zipo Nyingi Tuuuu.
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195

Mengi Anafanya Biashara Kwa Misingi Ya Kibepari...Mwenye Kuweza Kushindana Naye Ajaribu Kama Walivyofanya Clouds FM, Wao Wameweza; Kama Wengine Hawawezi Wanaweza Pia Kufanya Biashara Zingine Tofauti Na Zile Anazofanya Yeye...Mbona Biashara Zipo Nyingi Tuuuu.

Sawa kwanini wakizidiana kete anawakimbilia wananchi?
 

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Sawa kwanini wakizidiana kete anawakimbilia wananchi?


Kwa Sababu "Amewekeza" Kwa Namna Moja ama Nyingine Kwa Wananchi Na Anajua Fika Kuwa Wananchi Watamuonea Huruma...Hebu Baric Gold Au Mohamed Intreprise Walalamike Kwa Wananchi Halafu Tuone Kama Kuna Mtanzania Yoyote Atakayetega Sikio Lake Kusikiliza.
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195

Kwa Sababu "Amewekeza" Kwa Namna Moja ama Nyingine Kwa Wananchi Na Anajua Fika Kuwa Wananchi Watamuonea Huruma...Hebu Baric Gold Au Mohamed Intreprise Walalamike Kwa Wananchi Halafu Tuone Kama Kuna Mtanzania Yoyote Atakayetega Sikio Lake Kusikiliza.

"Amewekeza" kivipi? kuna gawiwo la dividends kwa kila mwaka kwa "wananchi" au kivipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom