Meneja wa uwanja wa michezo Sheikh Amri Abeid asimamishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meneja wa uwanja wa michezo Sheikh Amri Abeid asimamishwa kazi

Discussion in 'Sports' started by Ngongo, Sep 16, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,056
  Likes Received: 3,416
  Trophy Points: 280
  Meneja wa uwanja wa michezo mjini Arusha Bwana Ngwabi amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa mapato ya uwanja huo.Uwanja wa michezo sheikh Amri Abeid ni miongoni mwa viwanja vingi vinavyomilikiwa na chama cha mapinduzi ingawa viwanja vyote vya michezo nchini vilijengwa na wananchi wote enzi za mfumo wa chama kimoja.

  Bwana Ngwabi ni mfanyakazi wa muda mrefu sana alianzia kama afisa matangazo.barua ya kumsimamisha kazi imeandikwa na kuasianiwa na katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mama Mary Chatanda.
   
 2. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Kwani umesahau kwamba hicho ni chama cha wezi,Afadhali hivyo viwanja virudi serikalini vinaweza kuwa na tija.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa huwa anakula za mabango leo ndiyo wana mshitukia....hata hivyo Ngongo nifikishie ujumbe huu uwanja wa Sheikh Amri Abeidi ulijengwa na wananchi, wanafunzi wa Ilboru na wachina hivyo uwanja huu siyo wa CCM ni wa wananchi...
   
Loading...