Meneja wa TBA Kigoma atiwa mbaroni kwa kushindwa kukarabati shule,Tume yaundwa kumchunguza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Meneja wa wakala wa Majengo TBA mkoa wa Kigoma Mhandisi Mgalla Mashaka amekamatwa na polisi akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.

Meneja huyo amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu,sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo,mabweni,maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika ambapo Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga ameagiza kuundwa Tume kumchunguza meneja huyo.

Kwa upande wake Waziri Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.

Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.

ITV
 
Wataisoma namba, kila siku yanaibuka tu, ingekuwa siye tungeuza hata nyumba kufukia mashimo!
Hela yoyote iliyoibiwa lazima irudi kwa miaka hii 10! Kasoro EPA, Meremeta Gold, Kagoda.....!
 
Kama ana hatia atakuwa hajaitendea haki fani yake.
Hela kachukua na kazi imedorora haki kweli
 
Possible hiyo fedha ililipwa makao makuu TBA Kwa uzoefu wangu
 
Ngoja tusubiri ukweli utajulikana maana wanaotoa hela wanaunda Tume inawezekana hata huyo meneja hela nyingi hazijafika kwake kwa wakati...
 
kapewa mia 4 kati ya mia 9 alafu mnataka kazi ikamilike acheni utani. hakuna pesa ya kukamilisha kitu hapo
 
Nimeskitika sana habari zote za leo wateule wote wamekuwa wakitumia Staili ya Ndalichako kaitumia Mpina Minofu ya Samaki Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.Nchimbi kwenye mambo ya pamba na Mkuu wa Wilaya ya Busega Simkumbuki Jina ... Hii system ya MBWA ni mbaya sana,bila Media nadhani hawakubali kutoa maagizo.
 
Back
Top Bottom