........ngoja kwaaaanzaaa,hiyo laini uliyotaka pesa ihamishwe ilikuwa ya kwako mzee baba au ndio mambo ya aliyeuza cheni feki kapewa hela bandia!!!!
Hapana mzee baba, stori kamili ilikuwa hivi:
mm nina ndg yangu aliniazima Leseni nipate laini nifanye biashara..baadae tukakorofishana basi akaenda kuswap laini..(tukiwa hapo hapo jirani na laini ikiwa inafanya kazi nikashangaa sipigiwi simu wala kutumiwa sms bali laini ikazimishwa ghafla...nikajiuliza wameshindwa kuniita nipeleke laini ofisini yeye na meneja wake basi nikatulia). Nikamfuata aliyenipa leseni nikamuuliza akakiri amepeleka maombi ya kuswap laini...basi nikamwambia ndani kuna kiasi fulani cha pesa hakikisha meneja anakupatia na unanipa pesa yangu wewe unabaki na laini. Nikaona binti ananipiga chenga anataka atoroke na pesa iliyomo ndani basi nikampeleka mahakamani ili aseme akipewa laini pesa atanipa au hanipi?..
Nako mahakamani akakiri tukapewa kazi ya kufanya hadi pesa itakapopatikana, meneja akadai anamtambua mwenye jina linalosoma ktk laini...mm nikasema sawa, akasema niondoke...ila nikamwambia ndani kuna pesa kiasi fulani. Mda umeenda akampatia laini yule dada, mm namuuliza dada pesa iko wapi?, yeye anasema meneja anasema kaitoa uende wewe mwenyewe kuchukua ofisini kwakuwa imeonyesha tunamgogoro mkubwa. Nikaenda kufuatilia nikamkuta nikajibiwa niweke namba ya simu pesa atatuma....eeeh bwana eeeeh....nimekaa sana kila nikikumbusha najibiwa alisahau...maneno yakawa mengi.
Mwisho juzi kati katuma pesa pungufu, kila nikimpigia na kumtumia meseji kumweleza hajibu wala hapokei simu, nimewasiliana na wafanyakazi wa ofisini pale kuwaeleza naona nao ni wadogo hawana msaada, nao wanasema subiri subiri. Huu mchezo waliuanza tarehe 10 February 2019 hadi sasa hivi, pesa pungufu wanairusha April tena kwa kuwasumbua mara kwa mara
Sasa nakumbushia pesa yangu wamalizie kurusha maana ilikuwa pesa ya kwenye mtaji wangu na hilo salio ndio muamala wa mwisho kabla hawajaifunga laini. Kama vodacom ni wezi basi wawe wazi waseme pesa hupati au unapata.
Bado sijaamua kurudi kwa hakimu aliyetuamuru pesa yote ikipatikana twende tukafute madai, hii kazi ameamua kuibeba meneja.
Pia nawaza inawezekana wakawa wamegawana pesa hiyo kati ya yeye meneja na huyo dada,,,,,bado nalifikiria hili