Siku mbili zilizopita vyombo vya habari vimeripoti kwamba NEMC imetangaza kwamba kuanzia sasa mirindimo yoyote na kelele zozote zinazohusiana na sherehe, matangazo, sauti kubwa kutoka majumba ya starehe, magari ya poromosheni, makanisani yatakuwa yanalipiwa shilingi milioni 5 hadi milioni 10. Na kwa yule atakayekiuka atatozwa shilingi milioni 50 ama kufungwa jela.
Kiuhalisia, hakuna kanisa ambalo litaweza kulipa shilingi milioni 5 kwa mkutano wa Injili ya Kristo kwa siku moja hata ingekuwa kwa mwezi. Kwa maana nyingine makanisa yamefungwa speed governor ya kutangaza Habari Njema za Ufalme wa Mbinguni.
Chini ya utawala huu wa awamu ya tano, iwapo NEMC watatekeleza hiyo sheria yao, basi Habari Njema za Ufalme wa Mbinguni zitaadimika kwa kiasi kikubwa.
Historia ya kanisa inaonesha kwamba yeyote aliyejaribu kuzuia makusudi ya Mungu wa mbinguni, mtu huyo aliondoshwa kabla kusudi hilo halijapotea. Mfano mzuri wa Biblia ni ule wa mfalme Herode ambaye tunasoma habari zake katika kitabu cha Mathayo sura ya pili.
ANGALIZO: Wote wenye mamlaka tufahamu kuwa mamlaka kuu ni ya Mungu wa Mbinguni; tuelewe kwamba hakuna atakayenyoosha kidole karibu na mboni ya jicho la Bwana akanusurika, mfalme Belshaza wa Ukaldayo; dola iliyokuwa ikitawala takribani dunia nzima; alijikinai akidhani ni mkuu mno mwenye kuweza kuchafua na kunajisi vyombo vya hekaluni kwa Mungu. Mungu alimfutia ufalme wake akaugawa kwa Waajemi na Wamedi. Daniel sura ya 6.