Complex
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 4,120
- 4,790
Nianze tuu kwa kusema kuwa hii mada siyo kwa ajili ya kudhihaki jinsia nyingine, wala siyo kwa ajili ya kukejeli, bali ni mada ya kukumbushana na kuelimishana.
Ni kazi ngumu sana kwa mwanamume kuwa mwanaume, siyo kwamba haiwezekani, bali ni ngumu kwa mwanamme kuuvaa uhusika wa uwanaume kama inavyotakikana. Na hakuna atakayelielewa hili zaidi ya sisi wanaume. Kuna changamoto nyingi sana tunakumbana nazo katika kukamilisha majukumu yetu ya uwanaume.
Maandiko na jamii inatambua mwanaume ni kichwa cha familia na kiongozi katika jamii husika. Kwa hiyo kwa kuzaliwa mwanaume, by default jamii inakuangalia kwa jicho hilo kuwa wewe ni kiongozi na mwenye maamuzi. Kwa namna moja ama nyingine itafikia mahali katika safari ya uwanaume wako utatakiwa kufanya maamuzi aidha iwe maamuzi yanayokuhusu wewe binafsi ama yahusuyo mustakabali wa maisha ya wengine (ie familia, jamii nk). Maamuzi hayo yanaweza kuwa mabaya ama mazuri, lakini huwezi kukwepa hili la maamuzi ukishakuwa mwanamume kwani itakupasa uyafanye kwa mustakabali wa maisha yako, ama upoteze uwanaume wako ama uharibikiwe maisha yako
cha msingi katika hili la maamuzi usiogope kufanya maamuzi, kwani umeumbwa kufanya hivyo na hilo ni mojawapo ya jukumu lako la msingi hapa duniani. katika safari ya uwanume kuna baadhi wanakata tamaa njiani, kuna ambao wanashindwa kufika safari na kuna ambao wanafika wakiwa na majeraha na makovu lukuki. Tumeshuhudia wengi wa vijana siku hizi wanatafuta ahueni ya kusaidiwa majukumu yao na wenzetu wanaweke(wenyewe wanaitwa kulelewa). Hili jambo halikubaliki hata mbele ya Mungu (Kwa imani yangu). Kwani misingi ya uumbwaji wa dunia ilimuweka mwanaume kuwa mtafutaji na mpambanaji kwa ajili ya jamii yake inayomzunguka regardless ya chanamoto zinazomkumba. Katika hili hakuna excuse.
Kuwa Mwanamme, yakupasa uwe active katika siku zote za maisha yako.
.......itaendelea