Men only (inahusu wanaume)

Men only (inahusu wanaume)

Haya lala atakuletea hapo kitandani.

Kusema hivo sikumaanisha mtu ndo abweteke akisubiria riziki!
Anapaswa kuchacharika na vile vile kumuomba Mungu!

KAMA IPO IPO TU!
 
Ushauri mzuri sana huu kwa wanaume.
Koromeo udumu milele.
Wanaume wa siku hizi baadhi yao wamesahau wajibu wao.
 
Last edited by a moderator:
Itakua umezodolewa wewe roho inauma.

Hapana, sijazodolewa kama ulivyosema. Huu ushauri unawahusu wanafunzi wa vyuoni wenye boom na wahitimu wa vyuo wanaotafta kazi. Imenilazimu kusoma ili nijue inahusu nini kabbla sijakujibu, nimejua inawahusu hao.

Mimi sio mwanafunzi wa chuo kwa hiyo sipati boom wala sihusiki,vile vile mimi sitafti kazi na bahasha na kuchagua kazi. Lakini hii akili ya kwamba usichague kazi niliipinga sana miaka ile namaliza chuo, kwa kweli nilikua nachagua kazi, kazi za kibwege ----- sikutaka hadi nilipokuja kupata kazi niliokua naitaka na sehemu niliyokua naitaka.

Nadhani umenielewa, sijazodolewa kama ulivyosema kiongozi.
 
HESHIMA PESA, NDEVU HATA MBUZI ANAZO.

Sio nia yangu kuponda au kusolola mtu kumdogofisha au kufanya ajiskie mnyonge. Ila haya mambo tusipoyasikia toka kwenye vinywa vya watumishi wa Mungu haitaleta uzito.

Kuna wanaume wengi ambao sasa inabidi kusema bila kuficha kuwa wanatia aibu. Hakuna kitu kibaya duniani kama Mwanaume kukosa hela au nguvu ya kiuchumi.

Hata maandiko yanaweka wazi kuwa hekima ya maskini hudharaurika. Mwanaume kuwa na maneno mengi na mfuko tupu utaishia kukasirikia watu na kuweka vinyongo.

Wengi wanakwambia kazi hakuna, sijui ajira ngumu ila ukweli ni kwamba ni wavivu na wanachagua kazi.Unakuta mtu anamcheka muuza mkaa au muuza machungwa, anamdharau dereva wa bodaboda wakati yeye anakaa kwa shemeji hana mbele wala nyuma.

Dereva wa bodaboda anaingiza faida ya elfu hamsini kila siku 50000/= na hiyo ni kwa siku ambayo biashara haikuwa nzuri. Wako watu wanavibanda vya matunda wanaingiza mpaka laki moja T.Shs 100,000/= hakatwi TRA wala NSSF kwa siku. Wewe unaita hiyo kuwa ni kazi ya kijinga huwezi kufanya.

Umekalia kuzunguka maofisini na Bahasha ya kaki kutafuta ajira ambayo hata ukiajiriwa unalipwa Milion moja, ikikwanguliwa Makato unakuta kwa mwezi unapokea laki Saba au less.700,000/= ukipitia hesabu ya nauli kwenda na kurudi kazini, chakula na vocha unakuta mwezi mzima unafanya kazi shilingi laki moja 100,000/= ambayo mwenzako anaingiza kila siku. Usidharau kazi.

Usibweteke kama Mwanaume ukabaki kulaumu watu kuwa wamegoma kukusaidia. Mwanaume jiongeze. Kesho tu utakuwa Baba wa familia, kwani mkeo naye unategemea kaka zako watakusaidia kutunza?

Unawaza nini juu ya maisha ya kesho?Mwingine uko Chuo unalipwa Boom unanunua simu ya laki Saba na jeans, hata kusoma husomi kutwa uko Facebook, WhatsApp na Instagram unatupia picha tu.

Kesho simu halina hata vocha huwezi ku-access internet unabaki kucheza game. Wakati wenzako hilo Boom wanajinyima wanaanzisha miradi. Mpaka anamaliza Chuo tayari alishajitengenezea ajira.

Wakati wewe unahangaika na Bahasha kutafuta ajira mwenzako anaitwa Boss anaajiri. Hebu fungua fahamu zako, utakuwa tegemezi mpaka lini?Mwanaume ni chachu ya mabadiliko. Mwanaume ni kiongozi.

Najua unamaono makubwa na ndoto kubwa lakini kabla ndoto hazijatimia lazima kuwe na chakula mezani, kuwe na mavazi mwilini, na kuwe na nyumba ya kuishi (Kodi). Hayo hayatasubiri mpaka uwe Billionaire ni mahitaji ya kila siku.

Pata shughuli ya kufanya. Jiongeze. Usiwaze sijui watu watakudharau, sijui watu watakuonaje? Wakati njaa inakukong'ori utakuwa peke yako chumbani. Potezea watu, weka heshima pembeni, ingia mzigoni. Tengeneza PESA.

Namaliza na waimbaji mnaozunguka na CD makanisani mkitafuta nafasi za kuimba na mwisho mpewe "nauli" hakuna future ktk Hilo. Jipe shughuli itakayokuingizia PESA ili ufanye huduma kwa moyo na sio kwa kutazama pesa.

Ndio maana mkialikwa makanisa madogo hamuendi kwasababu mnajua hakuna hela huko. Mnaishia kununuliwa na kuendeshwa. Kipaji bila hela ni mzigo tu. Angalia Muhindi hajui kuimba wala hajui kiswahili vizuri lakini wasanii wanampigia magoti.

Pesa ni jawabu. Pambana upate pesa na ni mpango wa Mungu utajirike. Sukuma toroli la maji cha msingi unaingiza pesa. Acha upedeshee na nguo za kuazima. Loh! Mwanaume hasifiwi usafi wala uzuri wa uso, mwanaume anasifiwa uchapakazi.

Kukaa kanisani masaa 24 unaomba bila kujishughulisha hiyo ni kazi ya wajane waliovuka miaka 60, wewe toka nje pambana ulete sadaka na fungu la kumi.

KUMBUKA HESHIMA PESA, NDEVU HATA MBUZI ANAZO.Hii nayo ni habari njema. (2Wathesalonike 3:10)

Mmh haya ni makavu live najua fika kuna watu wanapita kimyakimya na kuachia misonyo mireefu kama utelezi wa bamia lakini habari ndio hiyo
Quinine ni chungu lakini inatibu maralia
 
Wanaume na wasikie, wavulana endeleeni kupiga selfie na majumba na magari ya wanaume, mkikua mje msome hapa.

na kupost picha insta ndo kazi za wavulana..............wao mda wote kiba na domo nan mkali lol..............
 
mada yako ni nzuri ila naona mentality tulio nayo wakati tunasoma ndiohua inatunyima kuthubutu. kila mtu anawaza akitoka chuoni atapata kazi tena nzuri na derva wa kumuendesha. kwa kifup chuoni tunakua hatujajua kitaa kukoje baada ya kusambaza bahasha mwaka bila mafanikio ndo mtu unapata picha ya hali halisi

psychologia ya mtu aliyekosa kazi nadhani anakua anaishi kupitia ndoto kwamba one day yes ndo maana wangi wanashindwa kufikiri nje ya box.

sijawahi kuishi maisha maisha ya kukosa kazi ila nahisi yanachanganya sna. inabid uwe mstahamilivu sana ili kuanza kufanya kazi ambazo wengi wanaamini si za staha. hata hivyo hamna jinsi ili maisha yaende ni lazima ujitoe kupigana kiume haswaaaa tusijali kazi ila tunapozifanya tutumie akili illi kuonesha tofauti kati yako na yule ambaye hakupiga umande

halaf kazi nyingine hata hazihitaji mitaji mikubwa. unakuta mtu anaishi mjini kwa biashara ya chai tu. kazi yake ni kununua mikate na kuipaka blue band usiku asubuhi anabandka sufuria la chai kubwa akiuza mpaka ikiisha ana faida ya kutosha tu. ni wangapi wako tayari kuzunguka na thermos sokoni? inataka moyo sana
 
Tatizo mtoa mada hajatuambia nn cha kufanya....!! Njia za kupitia anatupa lawama tu ....
 
Back
Top Bottom