Men only (inahusu wanaume)

Men only (inahusu wanaume)

Mkuu umenena watu wanabaki kuilaumu serikali wakati mtaji wameukalia
 
Umeeandika point zenye GB 500 big up bro wambie watoto wazembe wafanye kazi. Sio kudownlord movie mpya na kucheza play station..
 
Shukrani mkuu....
But umewasahau wanaotafuta pesa then wanaishia kuhonga viwanawake...
 
Uzi makini sana huu,kwa mwenye akili ya kujiongeza atapata chochote, sio ku criticize hata hoja za msingi
 
Nikiwa Kama Mchungaji Iyo Imekaa Vzr, Mungu Alipomuumba Adamu Kazi Ya Kwnz Kumpa Ni Kuilima Na Kuitunza Bustani (Mwanzo 2:15). Na Sifa Ya Kwnz Ya Mwanamume Anaestahili Kuwa Mume Ni Uwezo Wa Kufanya Kazi, Nina Libariki Neno Hilo Kwa Jina La Yesu Kristo.Amen
 
HESHIMA PESA, NDEVU HATA MBUZI ANAZO.
Sio nia yangu kuponda au kusolola mtu kumdogofisha au kufanya ajiskie mnyonge. Ila haya mambo tusipoyasikia toka kwenye vinywa vya watumishi wa Mungu haitaleta uzito. Kuna wanaume wengi ambao sasa inabidi kusema bila kuficha kuwa wanatia aibu. Hakuna kitu kibaya duniani kama Mwanaume kukosa hela au nguvu ya kiuchumi. Hata maandiko yanaweka wazi kuwa hekima ya maskini hudharaurika. Mwanaume kuwa na maneno mengi na mfuko tupu utaishia kukasirikia watu na kuweka vinyongo.
Wengi wanakwambia kazi hakuna, sijui ajira ngumu ila ukweli ni kwamba ni wavivu na wanachagua kazi.
Unakuta mtu anamcheka muuza mkaa au muuza machungwa, anamdharau dereva wa bodaboda wakati yeye anakaa kwa shemeji hana mbele wala nyuma. Dereva wa bodaboda anaingiza faida ya elfu hamsini kila siku 50000/= na hiyo ni kwa siku ambayo biashara haikuwa nzuri. Wako watu wanavibanda vya matunda wanaingiza mpaka laki moja T.Shs 100,000/= hakatwi TRA wala NSSF kwa siku. Wewe unaita hiyo kuwa ni kazi ya kijinga huwezi kufanya.
Umekalia kuzunguka maofisini na Bahasha ya kaki kutafuta ajira ambayo hata ukiajiriwa unalipwa Milion moja, ikikwanguliwa Makato unakuta kwa mwezi unapokea laki Saba au less. 700,000/= ukipitia hesabu ya nauli kwenda na kurudi kazini, chakula na vocha unakuta mwezi mzima unafanya kazi shilingi laki moja 100,000/= ambayo mwenzako anaingiza kila siku. Usidharau kazi. Usibweteke kama Mwanaume ukabaki kulaumu watu kuwa wamegoma kukusaidia. Mwanaume jiongeze. Kesho tu utakuwa Baba wa familia, kwani mkeo naye unategemea kaka zako watakusaidia kutunza?
Unawaza nini juu ya maisha ya kesho?
Mwingine uko Chuo unalipwa Boom unanunua simu ya laki Saba na jeans, hata kusoma husomi kutwa uko Facebook, WhatsApp na Instagram unatupia picha tu. Kesho simu halina hata vocha huwezi ku-access internet unabaki kucheza game. Wakati wenzako hilo Boom wanajinyima wanaanzisha miradi. Mpaka anamaliza Chuo tayari alishajitengenezea ajira. Wakati wewe unahangaika na Bahasha kutafuta ajira mwenzako anaitwa Boss anaajiri. Hebu fungua fahamu zako, utakuwa tegemezi mpaka lini?
Mwanaume ni chachu ya mabadiliko. Mwanaume ni kiongozi.
Najua unamaono makubwa na ndoto kubwa lakini kabla ndoto hazijatimia lazima kuwe na chakula mezani, kuwe na mavazi mwilini, na kuwe na nyumba ya kuishi (Kodi). Hayo hayatasubiri mpaka uwe Billionaire ni mahitaji ya kila siku. Pata shughuli ya kufanya. Jiongeze. Usiwaze sijui watu watakudharau, sijui watu watakuonaje? Wakati njaa inakukong'ori utakuwa peke yako chumbani. Potezea watu, weka heshima pembeni, ingia mzigoni. Tengeneza PESA.
Namaliza na waimbaji mnaozunguka na CD makanisani mkitafuta nafasi za kuimba na mwisho mpewe "nauli" hakuna future ktk Hilo. Jipe shughuli itakayokuingizia PESA ili ufanye huduma kwa moyo na sio kwa kutazama pesa. Ndio maana mkialikwa makanisa madogo hamuendi kwasababu mnajua hakuna hela huko. Mnaishia kununuliwa na kuendeshwa. Kipaji bila hela ni mzigo tu. Angalia Muhindi hajui kuimba wala hajui kiswahili vizuri lakini wasanii wanampigia magoti. Pesa ni jawabu. Pambana upate pesa na ni mpango wa Mungu utajirike. Sukuma toroli la maji cha msingi unaingiza pesa. Acha upedeshee na nguo za kuazima. Loh! Mwanaume hasifiwi usafi wala uzuri wa uso, mwanaume anasifiwa uchapakazi. Kukaa kanisani masaa 24 unaomba bila kujishughulisha hiyo ni kazi ya wajane waliovuka miaka 60, wewe toka nje pambana ulete sadaka na fungu la kumi. KUMBUKA HESHIMA PESA, NDEVU HATA MBUZI ANAZO.
Hii nayo ni habari njema. (2Wathesalonike 3:10)
Hapo kwenye red mkuu ni ukweli ulio uchi. Jamaa wa aina hiyo kazi ya ni kutumwa na mke(shemeji) wa kaka yake maandazi asubuhi na mchana kutumwa nyanya gengeni vinginevyo hakuna kupewa chai asubuhi wala ugali mchana.
 
Eeeh watu kama wewe mnapaswa muishi maisha marefu ili muendlee kutoa busara zenu kwetu sisi vijana,nmejifunza kitu pia hata kutegemea mshahara wa laki 7 mwisho wa mwez kwa mwanaume nao na uzembe...
 
Safiii! Huu Uzi umetulia,umetugusa vijana wengi wa Leo. Wengi wetu tunajiaminisha ufahari kuajiriwa maofisini, lakini kumbe kujiajiri ni bora zaid! Waweza kupata riziki kwa akili, nguvu na kwa muda wako mwenyewe. Kufanikiwa au kufeli ni utashi wako mwenyewe.
 
Nikiwa Kama Mchungaji Iyo Imekaa Vzr, Mungu Alipomuumba Adamu Kazi Ya Kwnz Kumpa Ni Kuilima Na Kuitunza Bustani (Mwanzo 2:15). Na Sifa Ya Kwnz Ya Mwanamume Anaestahili Kuwa Mume Ni Uwezo Wa Kufanya Kazi, Nina Libariki Neno Hilo Kwa Jina La Yesu Kristo.Amen

Amen...
 

Unawaza nini juu ya maisha ya kesho?Mwingine uko Chuo unalipwa Boom unanunua simu ya laki Saba na jeans, hata kusoma husomi kutwa uko Facebook, WhatsApp na Instagram unatupia picha tu.

Kesho simu halina hata vocha huwezi ku-access internet unabaki kucheza game. Wakati wenzako hilo Boom wanajinyima wanaanzisha miradi. Mpaka anamaliza Chuo tayari alishajitengenezea ajira.

Wakati wewe unahangaika na Bahasha kutafuta ajira mwenzako anaitwa Boss anaajiri. Hebu fungua fahamu zako, utakuwa tegemezi mpaka lini?Mwanaume ni chachu ya mabadiliko. Mwanaume ni kiongozi.

USHUHUDA:

Nikiwa mwaka wa mwaka mwishoni kulitangazwa kuuzwa kwa viwanja vya SALASALA. Enzi hizo unajiona bado mdogo. Unaojiona una mengi ya kufanya kuponda maisha.

Sikuona umuhimu wa hata kufikiria kununua viwanja. Niliwaza kwanza mimi ninataka kuwa na kiwanja kwenye maeneo ya 'low-density' sio vile vya salasala. Nikapuuzia.

Nilikuwa na rafiki yangu aliniambia kuhusu vile viwanja na kuwa yeye alikuwa na mpango wa kununua na alinishawishi na mimi ninunue pia. Mimi sikununua. Yeye alinunua...kwa boom!!!!!!!!!!!!!

Matokeo yake, mwenzangu ameoa mwaka jana...akahamia kwenye nyumba yake. Juu ya hapo, ana mradi wake unamuingizia fedha za kutosha pembeni ya kazi ya kuajiriwa. Mimi ndio kwanza ninahangaika na kununua viwanja na kukusanya pesa za ujenzi...!

Kijana uliyeko chuo sasa hivi, jitahidi kuwekeza. Hata kama sio kwenye ardhi, jitahidi kuwa na mradi yaani hilo boom (au fedha unayopewa na mzazi) hiyo hiyo kidogo itumie izae. Usikae ukafikiri maisha bado. Ulianza kuishi tangu ulipozaliwa, na maisha hayakusubiri ufuje pesa kwanza ndo uanze kujipanga baada ya kumaliza chuo.

Wakati sisi tunamaliza chuo tunasambaza CV kama hatuna akili nzuri, rafiki yangu huyu alikuwa kwenye mradi wake anapiga pesa taratibu. Kazi ilimfuata. Sasa hivi anaweza kusema haishi kwa kutegemea mshahara. Yani kwake mshahara ni kitu tu cha kumwezesha kuchukulia mikopo kukuza biashara zake zaidi.

Ni maisha ambayo kila kijana anaweza kuwa nayo kama tusiposubiri kujifunza kama mimi nilivyojifunza. Usisubiri ukosee wewe ndo ujifunze (Wise is he who learns from others' mistakes).

Amka...jishughulishe! wekeza...anzisha miradi...IT IS NEVER TOO EARLY...!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom