Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
- Thread starter
-
- #121
bunge la afrika lugha ya mawasiliano ya wazungu.....
Kwa hiyo mwakilishi kutoka Tanzania akikutana na mwakilishi kutoka Ethiopia au Benin wanaongea kiswahili? Lugha ya waafrika?
Narudia hakuna anayepinga kiswahili kutumiwa kinachosemwa hapa ni mwakilishi ajue lugha zote mbili! Kisichoeleweka hapa ni nini?
Kwa hiyo tutafika mahali tutasema sio lazima Waziri Mkuu ajue Kiingereza? Au Waziri wa Mambo ya Nje kama anajua kiswahili inatosha? Tuache kujidanganya kwamba kuongea kiingereza ni ukoloni. Unatakiwa ujue lugha zote mbili kama mwakilishi ili iwe rahisi kujenga mahusiano na kujifunza kutoka kwa wengine.
bunge la afrika lugha ya mawasiliano ya wazungu.....
Ndiyo. Kwani wewe unadhani hilo haliwezekani?Kwa hiyo mwakilishi kutoka Tanzania akikutana na mwakilishi kutoka Ethiopia au Benin wanaongea kiswahili? Lugha ya waafrika?
Ajue lugha zote mbili mojawapo ikiwa ya Kizungu wakati yeye ni mwakilishi kwenye bunge la Afrika. Kwa nini asijue lugha mbili zote za kiafrika?Narudia hakuna anayepinga kiswahili kutumiwa kinachosemwa hapa ni mwakilishi ajue lugha zote mbili! Kisichoeleweka hapa ni nini?
Kwa hiyo tutafika mahali tutasema sio lazima Waziri Mkuu ajue Kiingereza?
Kwa waziri wa mambo ya nchi za nje ni tofauti kabisa. Angalia karibu nchi zote mawaziri wao wa nchi za nje wanazungumza Kiingereza.Au Waziri wa Mambo ya Nje kama anajua kiswahili inatosha? Tuache kujidanganya kwamba kuongea kiingereza ni ukoloni. Unatakiwa ujue lugha zote mbili kama mwakilishi ili iwe rahisi kujenga mahusiano na kujifunza kutoka kwa wengine.
Issue ipi ambayo haijaongelewa hapa kuzuia kuongelewa personalities? Vyote vimefanyika. Issue imeongelewa na personalities zimeongelewa. Just swallow both and accept a different opinion or point of view.
Hapa January tunampa umaarufu wa bure. Ni sawa nianze kujilinganisha na Dr. Slaa au Tundu Lissu eti tuko sawa. Ni uendawazimu tu. Suala ni kujifunza kutoka kwao basi. Huyu yeye atakuwa anatafuta ligi. Uzuri ni kwamba Yanga ikiomba kucheza na Real Madrid wataingia watu wengi sio kuiona Yanga bali Real Madrid na kwa vyovyote Yanga wataneemeka na mapato hata kama watafungwa 7-0! Tumpotezee huyu.
Siku ambayo lugha ya kiswahili itakuwa imekuwa na kufundishwa nchi nyingine za Afrika basi itatumika kama njia ya mawasiliano na hakutakuwa na sababu ya kutumia hizo lugha nyingine.
Watawasiliana kwa Kiingereza au Kifaransa au Kireno. Hawatawasiliana kwa Kiswahili. Ikitokea wote hawajui hizo lugha za pili au tatu watawasiliana kwa ishara au hawatawasiliana. Siku ambayo lugha ya kiswahili itakuwa imekuwa na kufundishwa nchi nyingine za Afrika basi itatumika kama njia ya mawasiliano na hakutakuwa na sababu ya kutumia hizo lugha nyingine.
Masahihisho....kiswahili hakifundishwi katika nchi zote za Afrika. Ethiopia na Benin hawajifunzi kiswahili. Ila, ninachosema hapa ni kwamba bado hatujafika mahali kusema wawakilishi wanaweza kuwasiliana nje ya mkutano kwa kiswahili na wakaelewana vizuri. Yeyote atakayeenda kama mwakilishi ni vyema akajua kingereza kama lugha ya pili.
Kwa nini Kifaransa etc na si Kiswahili kwa sababu as of now kiswahili hakitumiki Benin bado. Mpaka tukifikia hapo watatumia lugha hizo za pili.
Kuhusu personality....ningependa usome comments za thread nzima na sio post moja ulioinukuu. Ziko post nyingi na issue zimejadiliwa humo. Am replying using my phone and that makes it hard kureproduce.
Ninachukia sana mtu anayefikiri kuwa msomi ni yule anayejua kiingereza vizuri. Ni mpuuzi tena kiongozi wa wapuuzi. Umeona siku hizi matoto yetu yanaongea kiingereza vizuri lakini moja jumla moja hayajui.
Kiswahili hakina matatizo hayo, lakini wenyewe tunakidharau na wala hatujui hayo.
Kiswahili kina hatari ya kupotea. Jaribu tu kusikiliza redio za bongo siku hizi. Watu wanachanganya lugha pasipo hata na ulazima. Kwangu hiyo ni kero tupu. Huko tunakoelekea sasa mwishowe itazaliwa lugha mpya yenye mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza.
Na haya mazoea ya kuchanganya Kiswahili na Kiingereza yametufanya tusizijue lugha zote mbili kwa ufasaha hususan Kiswahili ambacho ni moja ya lugha rahisi sana kujifunza na kuzijua.