Membe: Sitogombea Ubunge 2015

Membe: Sitogombea Ubunge 2015

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1,200
Reaction score
908
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

"Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge," alisema Membe.

Aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.

Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.

Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila faida.

"Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo," alisema Membe.

Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.

Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka mpya.

Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.

MY TAKE:
Kwa upande wa CCM naona kuna uwezekano mkubwa sana Membe ndo akapitishwa kuwa mgombea wa urais kwani series of events kama zilivyojitokeza katika uchaguzi wa NEC ambapo bila ya Kikwete ujumbe huo angeukosa,si hilo tu lkn pia inaelekea tujiandae kwa upande wa CCM kuwa its either Lowassa au Membe.

God Help Us.
 
....ni haki yake kugombea...ni haki yetu kuchagua kilicho bora...
 
Mjomba naye anataka kuingia magogoni tunawatakia kila la kheri ktk maamuzi yao magumu
 
Sijui ni kitu gani kinawasukuma hawa watu kutaka kutuongoza ikiwa tu hawajui kwanini Tanzania ni maskini.
Kibaya zaidi utagundua kuwa hao wote ni wasanii tu,tene bora hata ya lowassa kuliko huyu Membe,huwa namuona kama mtu ambaye hajielewi,na Membe ndo chaguo la Rais coz anaonekana anaweza kulinda status quo na kulinda maslahi ya JK,Lowassa akiingia madarakaNI nahisi JK hatakuwa salama.
 
Sijui ni kitu gani kinawasukuma hawa watu kutaka kutuongoza ikiwa tu hawajui kwanini Tanzania ni maskini.

uchu na uroho wa madaraka, pasipokujua ua pengine wanajua ila hawataki kufanya kile wanachotakiwa walifanyie Taifa.
 
Ah ndo kwaanza ngoma inaanza! Ila kwa ccm hakuna wa kumpinga laigwanan
 
Membe bwana, ila najua lazima patachimbika unacheza na laigwani? wanapolala yeye ndo alipoamkia. Natamani sana Membe na EL wagombee ili mnyukano wao uwe hadharani na hatimae tushuhudie nyasi zitakavyoumia
 
Uzuri wa Lowassa kwa kweli ni determination,kujiamini,kupiga kazi,kusimamia anachoikianzisha,kuwadadabisha walio chini yake,tatizo lake tu ni hilo la kupenda pesa kuliko kitu kingine.
 
Na haya ndio mambo yanayofanya tubaki kuwa maskini...viongozi wengi (akiwemo Membe) hawatimizi majukumu yao ipasavyo wamejawa na tamaa, sifa na uroho wa madaraka......at the end hakuna wanalofanya bali hutoa sababu kede kede za kutofikiwa malengo ya mafanikio ya Tanganyika yetu..."samahani ni Tanzania yetu."
 
kwa mtazamo wangu sioni yeyote hapo wa kumpa vote yangu. old fish in a new pan
 
JAMII FORUM,HESHIMA MBELE,UKWELI BILA KIFICHO,JUKWAA LENYE MANUFAA NA LINALOTUFAA,,

TU
NAENDELEA,NA TUACHENI TU WATU WA KUSINI TUENDELEE KUITETEA RASILIMALI HII KWA MASLAHI YA TAIFA,,
KATIKA KILE KINACHOZID KUONESHA NI KWA JINS GANI WATU WA KUSINI TULIVOKOSA UZALENDO,UCHUNGU,NA KUJITAMBUA BERNAD CAMILIUS MEMBE AMEENDELEZA KUTUONESHA NI JINS GANI ALIVYO JOKA LA KIDIMU KWA KUKAA KIMYA HADI WAKATI HUU KAMA WAZIRI MWANDAMIZI WA SERIKALI HII YA MAFISADI HUKU WAPIGA KURA WAKE WAKIZID KUDHARAULIWA PINDI PALE WALIPOONYESHA NIA YAO YA DHATI KATIKA KUIPIGANIA GESI KWA MANUFAA YA WATANZANIA,,
MEMBE NI MIONGONI MWA WALE MALIMBUKENI WA SAMPULI YA LAZARO NYALANDU,HAND TO MOUTH POLITICIANS,NAME DROPPERS,PEOPLE WITH NO CONFIDENCE,HYPOCRITICAL FIGURES NA MENGIYO YA KUCHUKIZA KATIKA SIFA ZAKE,,KWA UFUPI NI LIMBUKENI NA CHAKUBIMBI KAMA CCM YAO,,

KWANINI MEMBE HAZUNGUMZI CHOCHOTE NA YUPO KIMYA KUHUSU GESI??
1.yeye ni wazir wa mambo ya nje,yumkini ni wale wale sampuli ya mkuchika na ghasia na chikawe ambao ni makuwadi wa jk katika kuiuza gesi hii,wote wamechukua 10 percent zao.,

2.kwa kuwa yeye ni wazir wa mambo ya nje upo uwezekano kahusika moja kwa moja kwenye kusign mikataba mibovu ya kuhujum gesi hii ya watanzania,

3.anahofia kwenda KINYUME na boss wake jk hasa ukizingatia jk ndie mwenye mamlaka ya mwisho katika kupitisha jina la mrithi wake katika urais huu unaokuja,

4.ni hulka ya watu wa kusiini ya kuvaa sifa za ujoka la kidimu,kutojiamin,ulimbukeni ili mradi tuh apate mamlaka na kujaza tumbo ili waende chooni,na bila shaka hulka hii leo inawahukumu,,
salam kwa membe,wanakusini na watanzania kwa ujumla tunajua kwanini yeye yupo kimya,ila katika harakati ambazo zimeanzishwa hakuna atakaerudi nyuma,gesi hii itapiganiwa hadi tone la mwisho la damu yetu,tutaipigania gesi hii kwa ajili ya manufaaa ya vizazi vyetu vijavyo,wewe endelea na mbio zako za urais huku ukisahau kuwa gei ndio kaburi lenu kwa kanda hii ya kusini

MODS NAOMBA HUU UZI NA UZI ZINGINE ZA GESI ZISIUNGANISHWE ILI UJUMBE UWAFIKIE KUWA SUALA LA GESI LIMECHUKUA TASWIRA PANA KILA PEMBE YA NCHI HII,,
MEMBE TUTAKUTANA 2015 KAMA KWELI NDOTO HIYO UNAYO..
 
Membe tokea aseme nchi haichuliwi kwa pickup halafu gadaff akafuliwa kwenye kalavati siku hizi kapwaya kwasababu 2015 peopleeeeeeeeeees wanachukua
 
Nilidhani kuna hoja ya kujadili kumbe ni kumjadili mtu? Kila la kheri
 
Opportunities nyingi sana za kuonyesha quality leadership na kujitambulisha anasimamia upande gani katika mustakabali wa nchi hii hatumuoni. HAFAI.
 
Back
Top Bottom