Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Kuna ugonjwa umeingia CCM,kitaalamu unaitwa Ukosefu wa Vyeo Vya Upendeleo (UVVU).Ugonjwa huu umeingia nchini punde tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015 na Dr John Pombe Magufuli kutangazwa kuwa rais wa JMT,na waathirika wakuu wakiwa wanasiasa waandamizi,wabunge walioanguka majimboni/kura za maoni,viongozi waliowahi kushika nyazifa za uwaziri na maeneo mengine ndani ya serikali ya CCM.
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.

Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.

Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
Ni kweli kabisa kwamba JK atakumbukwa kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao, lakini hata Rais aliyeko madarakani sijaona aliyenyimwa uhuru huo na ndio sababu hata mheshimiwa hapo juu pamoja na yote aliyosema bada Mr Presd yupo calm, na wanaomkosoa Bwana Membe kwa hayo anayosema pia wanatumia uhuru wao wa wa kutoa maoni kama anavyotumia yeye.

Kama uhuru huo wa kutoa maoni kwenye awamu ya sasa usingekuwepo wengi humu tungeshaanza "kunyea debe" manake watu wako huru mpaka uhuru wenyewe sasa unatumika vibaya kwani wapo wanaodiriki mpaka kuwakashifu hata viongozi wakuu.
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.

Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.

Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
Zile nyakati za zidumu fikra za mwenyekiti na watu wakashangiria zimeshapitwa na wakati .

Kukosolewa ni sehemu ya kujifunza na pia inamfanya mtu atafakari kwamba kuna upande wa pili wa shillingi.narudia tena yote aliyosema membe sasa yatakuja kuonekana hapo mbele kidogo .

Muda ndio utaamua kama yuko sahihi au hayuko sahihi
 
Membe alianza kwa kujipendekeza kumsifia JPM kwa kufuta safari za nje na kumponda swahiba yake baba Mwanaasha kwamba "walikuwa wanapishana angani kama nyumbani kunawaka moto"akijua kwamba Magufuli anapenda POROJO atampatia tena wizara,ikumbukwe kwamba baada ya mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM kulikuwa na tuhuma za chini kwa chini kwamba JK alishindwa kumbeba Membe mpaka hatua za mwisho.Na ya Membe kusahau upendeleo na fadhila zote za JK.Haya anayoyasema sasa hivi Membe ni baada ya kuachwa pembeni na Magufuli na sasa hivi ndio anakumbuka fadhila za JK alivyombeba kwa kipindi chote cha miaka 10.HAKUNA ASIEJUA KIWANGO CHA HALI YA JUU CHA UNAFIKI WAKE MEMBE
 
Kwani kuna kipi cha ajabu hapa,Membe hakuongelea suala la uchaguzi Zanzibar?
Sasa kama aliweza kuongelea suala zito kama lile hili atashindwa vipi?
Ninaunga mkono jitihada za Mh Maembe za kupaza sauti. Acha na yeye atusaidie, tumepiga kelele sana kuhusu haya magamba. Hayo tuyaweke kando, jamani Nifah unaweza kuwa na habari za Hajat Faiza Fox? Sijamsikia siku nyingi.
 
Hata sina habari zake mkuu,namuona kwa nadra sana humu ndani.
Hebu nimuite aone salaam zake hizi.
FaizaFoxy
 
Aendelee tu kusubiri talaka tena yake ni tatu hakuna kurudiwa.
 
Umeambiwa ujibu kwa hoja kama hujamwelewa kaa kimya wajibu tu waliomwelewa Membe, Tatizo ndani ya ccm imeshakuwa kama utamaduni akitoea mtu yeyote akikosoa uongozi awe mwana chama wa ccm asiwe mwana chama basi ni adui this is non sense katika ulimwengu wa sasa hivi hakuna mambo yanakuwa mazuri zaidi mtu anapokubali kukosolewa mfano mdogo tu whatsap, facebook na applications zingine kila mara wana update applications zao na kuwa nzuri kwa kutumia comments za wanaowakosoa. Mazuri mengi anayofanya Magufuli sasa hivi ni kutokana na comments za wapinzani na wana ccm wazalendo thidi ya serikali iliyopita lakini hawezi kuwa perfect 100% kwa sababu yeye tayari ni binadamu nasi tu dhaifu ndo mana atazidi kukosolewa ndiko kutazaliwa kufanya vizuri zaidi
nafikiri nia ya membe kukosoa ni kumjenga zaidi mr. president, hakuna mtu aliye mkamilifu,ukikosolewa ndio unapata njia iliyo bora zaidi ya kujiimarisha.
 
Huwezi kumuelewa kwa sababu unapokuwa unamsikiliza au kusoma alichokisema akili yako na roho yako vina kuwa havina ushirikiano,

Kwamba Roho yako inakuwa inamchukia kwa chuki binafsi na akili yako inataka kumsikiliza au kusoma.

Ila kwa hili la juzi ameeleweka sana na kila mwenye mapenzi mema na nchi hii wamekubaliana nae na wana muunga mkono Membe
hayo mapenzi mema kayaona sasa,hivi milion 700 zile zingenunua madawati mangapi,hawa wakwere hamnazo na milele hamtapewa nchi tena,
nchi ilinuka ufukara kwa ku expatriate resources,na membe akiwa mstari wa mbele leo anajitutumua kama jipu la kwenye masaburi kuhubiri kuhusu pombe.!!!!!!!!!!
 
Huyu aliewahi kusema Thomas Sankara alikuwa raisi wa Benin,Membe bwana ni wa kumpuuza tu
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.

Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.

Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
huo uhuru wa maoni wa jk mbona ulitoa mwanya kwa majungu na nafasi kwa ufisadi kushamiri.
 
Back
Top Bottom