Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Kwani kuna kipi cha ajabu hapa,Membe hakuongelea suala la uchaguzi Zanzibar?
Sasa kama aliweza kuongelea suala zito kama lile hili atashindwa vipi?
Tabia ya mtu hujitokeza hasa anapokosa anachokitaka.huu ni unafiki mbaya sana.siku zote mbona hakuwahi kukosoa utawala was ccm? Ajitokeze kwenye vyombo vya habari atangaze kupinga utawala was magufuli
 
Membe alisema Rais anatumbua majipu kwa wale ambao hawafahamu na angekuwa anawafahamu asingewatumbua.
Kutumbua majipu sawa lakini njia zinazotumika kutumbua hazijakaa vizuri kwa sababu kama mtu ameshindwa kuwajibika ipasavyo angalau apewe muda kidogo kabla hajatumbuliwa kwa sababu wengine walikuwa wazuri lakini wakawa wanafanya kazi kwa maelekezo kutoka juu! Tusijetumbua tukaharibu zaidi kuliko kujenga!
 
Bora Membe anaongea hadharani sio yule wa vipicha vya katuni sijui ni uoga
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje, Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria. Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo. Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe. Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao

Tuangalie zaidi hapo pekundu.... Benard Camillius Membe asijishebedue. Yeye anasifika kwa "kuvunja sheria." Asije akafikiri kwamba tumesahau ile skendo ya "one billion corruption strategy to the state house." Hana mamlaka ya kimaadili kumkosoa hata mtoto wa chekechea achilia mbali Rais Magufuli. Kwake yeye kuufanya ukosoaji kama anavyofanya ni "unafiki wa kutupwa." Sana sana amshukuru "kaka yake" Kikwete kwa kumlinda. Sasa hivi hiyo "one billion corruption strategy" ingekuwa imemfikisha Keko. Ngoja Magufuli aje aifufue tuone....
 
Nahisi kuna mgogoro mkubwa ndani ya CCM,mpaka Membe anajitokeza hadharani kusema haya basi amini nawaambieni kuna kundi kubwa nyuma yake linalompa ujasiri huu.
Hata hivyo wanazidi kuturahisishia kazi 2020 sio mbali.
Kweli mkuu vita ya panzi, harafu wataropoka mengi tu hali inavyoonesha maana huyu kiongozi anashambulia balaa
 
Ni wazi kabisa kuwa team Jk hawafurahishwi na mengi yanayofanywa na Magufuli kwakuwa
1.halikuwa chaguo Lao tangu mwanzo
2.anagusa maslahi yao
3.anagusa maslahi ya 'watu' wao
4.anawavua nguo peupe kwa timua timua ya watendaji walioteuliwa kipindi chao na kuibua kila aina ya uozo
5.ongezeko la mapato ya TRA linawaumbua kuwa hawakuwa makini
Orodha ni ndefu na kwakweli watafanya kila juhudi kumkwamisha ili aonekane hafai
Time will tell. ...!!!
Kwa hiyo Membe ana ile roho ya kwa nini afanye yeye. ?

Walitegemea Magufuli atachemsha ili tuukumbuke utawala wa Msoga bahati mbaya ndio anawaumbua kila kitu kiko wazi.
 
Kwa hiyo Membe ana ile roho ya kwa nini afanye yeye. ?

Walitegemea Magufuli atachemsha ili tuukumbuke utawala wa Msoga bahati ndio anawaumbua kila kitu kiko wazi.
Subiri uone huko mbeleni watakavyotibuana
 
Membe usinyamaze wala usiogope, badala yake endekea kusimamia haki, kuitetea khaki, Na kutenda haki, maovu ya CCM pamoja Na washirika wake Mungu amechoka nayo
 
Huyu Mmwera naona anataka kuichezesha SEBENE serikali
 
Kinachonifurahisha ni kuwa Membe leo ndo anayaona hayo anayoyakosoa kwa Magufuli na anasahau kabisa kuwa serikali ambayo yeye alikuwa waziri ndiyo serikali imelifikisha taifa hapa.Ama kweli nmeamini mapungufu ya mchezo huonekani ukiwa muonaji uko nje ya uwanja.
 
hizo ni trick za kutaka kuaminiwa nawananchi lakini kwa we ye upeo atasubili sana alikuwa wapi wakati wote kama so kutaka kujichukulia umaarufu kwa migongo ya wengine hakuna hoja hata moja iliyo niingia akilini maana watazania tulisha baki maboya wa xxm
 
Haki yake kuongea msitake kumfanya magufuli ni malaika nadhani yupo sahihi jibuni hoja cyo vijembe kwan hoja hujibiwa na hoja
 
Haki yake kuongea msitake kumfanya magufuli ni malaika nadhani yupo sahihi jibuni hoja cyo vijembe kwan hoja hujibiwa na hoja
CCM tunao watu wapumbavu sana... Yaani hawataki Magufuli akosolewe... Ni ujinga... Magufuli sio malaika, hivyo lazima akosolewe
 
Kikwete ng
Mwambieni basi amtaje mtanzania hata mmoja atakayemkumbuka rais mstaafu! Ninachokiona hapa, hili nalo limeiva tena dokta kalichelewesha mno.
Kikwete ndio rais bora kuliko wote waliopita hivi sasa kiongozi wa umma huna uhakika kesho kama utarudi kazini ni presha tu
 
Back
Top Bottom