Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Membe: Sitanyamaza, ni haki yangu

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,067
Reaction score
134,417
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.

Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.

Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
 
Hii nchi ovyo sana chini ya hawa watu kwenye hili lichama.

Mtanzania anaishi kwa kudra na upendeleo wa Mungu baas. CCM haina msaada wowote kwa mlala hoi.
 
Good, let people give their opinions. Membe you are right, Sll men sre fallible no man is infallible. Magufuli is a man and subject to fallibility
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
Chanzo cha taarifa hii?
 
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao
Muache Rais atekeleze majukumu yake kama kumshauri sio kupitia vyombo vya habari omba appointment na Mh Rais akikubali nenda mkajenge nchi, kutoa ushauri kama akiukubali hewala akikataa basi tulia mzee,Mh atekeleze vission zake kwa kufuata mwongozo Ushauri usitumie vyombo vya habari kwa hilo mapumziko mema Mstaafu
 
Nahisi kuna mgogoro mkubwa ndani ya CCM,mpaka Membe anajitokeza hadharani kusema haya basi amini nawaambieni kuna kundi kubwa nyuma yake linalompa ujasiri huu.
Hata hivyo wanazidi kuturahisishia kazi 2020 sio mbali.
 
Hongera Membe ,Tumia Haki yako Kikatiba Ibara ya 18,Uhuru wa Kutoa Maoni.
 
Ni wazi kabisa kuwa team Jk hawafurahishwi na mengi yanayofanywa na Magufuli kwakuwa
1.halikuwa chaguo Lao tangu mwanzo
2.anagusa maslahi yao
3.anagusa maslahi ya 'watu' wao
4.anawavua nguo peupe kwa timua timua ya watendaji walioteuliwa kipindi chao na kuibua kila aina ya uozo
5.ongezeko la mapato ya TRA linawaumbua kuwa hawakuwa makini
Orodha ni ndefu na kwakweli watafanya kila juhudi kumkwamisha ili aonekane hafai
Time will tell. ...!!!
 
Bado kidogo tu atapewa cheo cha ukamanda, nyie subirini muone?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kwa mtizamo wangu naona kuna mgogoro mkubwa sana wa maslahi unaoendelea chini kwa chini, Membe ni mteule wa JK, Anaweza kuwa aidha anazungumza mtizamo wa kambi yake au anatishiwa na maslahi ya kambi yake.
Mfano: Wateule wa TRA na bandari ni wa JK kwa hiyo alichokisema Membe kwa sehemu kubwa kinalenga hapo!!!
Kwa Membe yeye hayuko kwa ajili ya Kuona kuwa maslahi ya Nchi kwanza!! Yeye maslahi yake na kundi lake kwanza. Ndiyo maana anaona watu walioteuliwa kwa maslahi wanaondolewa hivyo inatishia usalama wa maslahi yao.
 
Mwambieni basi amtaje mtanzania hata mmoja atakayemkumbuka rais mstaafu! Ninachokiona hapa, hili nalo limeiva tena dokta kalichelewesha mno.
 
Back
Top Bottom