Membe ni kiashiria cha nini kinaweza kumpata Magufuli mwaka 2020 au katika kumtafuta mwenyekiti

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Sitaki kuamini kama Membe yuko peke yake kimtazamo juu ya Magufuli na utendaji wake bali naamini anawakilisha mtazamo wa wengi ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya vigogo.Wengine nadhani wamekosa ujasiri tu ila mioyoni mwao wanawaza kama Membe.

Magufuli akiendelea hivi kama alivyoonza,basi kina Membe wengine tutawaona wakati wa kumchagua mwenyekiti wa CCM Taifa au katika kumpitisha mgombea uraisi wa CCM mwaka 2020.

Mh.Membe namuona ni kama mtu alieamua kuonyesha njia ili wengine wenye nia nao wajiunge katika safari hiyo.

Let expect more dissenting voices from within the party in the days ahead.
 
Sitaki kuamini kama Membe yuko peke yake kimtazamo juu ya Magufuli na utendaji wake bali naamini anawakilisha mtazamo wa wengi ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya vigogo.Wengine nadhani wamekosa ujasiri tu ila mioyoni mwao wanawaza kama Membe.

Magufuli akiendelea hivi kama alivyoonza,basi kina Membe wengine tutawaona wakati wa kumchagua mwenyekiti wa CCM Taifa au katika kumpitisha mgombea uraisi wa CCM mwaka 2020.

Mh.Membe namuona ni kama mtu alieamua kuonyesha njia ili wengine wenye nia nao wajiunge katika safari hiyo.
Binafsi namchukia membe hakuna mfano. Huyu akipewa serikali itakuwa kama ya mkwere. Hafai hata kidogo na kama ndo anatafuta kiki ya 2020. Atasubili sana mpake mvi zimtoke
 
Magufuli akikabithiwa chama ahakikishe anaua makundi hasa ya waliokuwa mahasimu wa kisiasa membe na Lowasa
Wale wanaoratibu hii mitandao tunawajua wamo kina nchimbi kina Sophia simba na wengine hatari sana asipoangalia........
 
Nawaza tu.

Membe yupo kimkakati zaidi na watu wasipokuwa makini,Membe atakuja kuua upinzani.Membe anaandaa mazingira yakuingia upande wa pili.

Membe kashaona nafasi yu huyo atakae kuwa mpinzani wa magufuli uchaguzi ujao,ana nafasi ndogo yakupitishwa.Membe atakuwa na kundi la vigogo wanao muunga mkono ili aje aendeleze yale yaliyokuwa ccm na hasimu wake.

Membe na ccm yake wanajua wanachokifanya,Inabidi watu wawe makini zaidi na aina ya siasa na matamanio ya yake.Nawaza tu.

KALINZI NYUMBANI.
 
Sitaki kuamini kama Membe yuko peke yake kimtazamo juu ya Magufuli na utendaji wake bali naamini anawakilisha mtazamo wa wengi ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya vigogo.Wengine nadhani wamekosa ujasiri tu ila mioyoni mwao wanawaza kama Membe.

Magufuli akiendelea hivi kama alivyoonza,basi kina Membe wengine tutawaona wakati wa kumchagua mwenyekiti wa CCM Taifa au katika kumpitisha mgombea uraisi wa CCM mwaka 2020.

Mh.Membe namuona ni kama mtu alieamua kuonyesha njia ili wengine wenye nia nao wajiunge katika safari hiyo.

Kiufupi kilichowapeleka JK,Mkapa na Warioba Magogoni ndiyo hicho alichokitema wazi wazi Membe!. Wenye akili walikwisha ng'amua zamani sana!
Falsafa ya hapa Kazi tu kwa gia za 180 ghafla itasababisha gari kukosa breki na kugonga wasiohusika!
 
Magu atarudi tu kwenye njia wanayoitaka vigogo wa ccm sababu atahitaji msaada wao ili kuupata uenyekiti wa ccm. Bado kidogo tu mambo kama zamani.
 
Kwa kifupi tusitegemee mapya kwa serekali hii ya John pombe Magufuli.. Hii falsafa ya hapa kazi tu inaweza kuondoka na wengi.. Wengine watakuwa wamesingiziwa ila kwasababu hapa kazi tu watatimuliwa.. Nakumbuka biblia ngo'mbe wanene kuliwa na Ng'ombe wembamba
 
kwa maghufuli anayo kazi. ccm imedhamiria kumkwamisha. ameanza kutenda kama jk kwa baadhi ya mambo.....
 
Kwahio unasema kuwa Magufuli awaache wafanyabiashara wasilipe kodi?

Unataka watu waendelee kujenga hovyo kandokando ya barabara na katika vyanzo vya maji?

Unataka Magufuli aache watumishi wa umma wawe kama kambale?

Unataka watumishi wa umma waendelee kutumbua pesa za wakulima kwa safari za nje zisizo na tija kwa nchi?

Membee anafahamika ni mufilisi na chagadema inafahamika imefilisika katika kujenga hoja na haina dira tena kwani rubani wa dira yenu aliwakimbia kwa kumkaribisha fisadi...majaliwa ya magufuli 2020 dalili zake zimeonekana juzi Arusha....
 
soon hata ya jpm itakua kama ya mkwere vuta subira kidogo
Sasa tukiwa na watu kama membe kwenye serikalu lazima turudi kule kule. Namuomba mungu sana angalu tanzania yangu iwe tanzania mpya. Tanzania ambayo mpaka wajukuu zangu wataisimulia kuwa aliwahi toke kiongozi aliye ivusha nchi kwenye mambo makubwa. Rushwa na ufisadi ni aibuu kwa taifa kama hili
 
kw
Sitaki kuamini kama Membe yuko peke yake kimtazamo juu ya Magufuli na utendaji wake bali naamini anawakilisha mtazamo wa wengi ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya vigogo.Wengine nadhani wamekosa ujasiri tu ila mioyoni mwao wanawaza kama Membe. s

Magufuli akiendelea hivi kama alivyoonza,basi kina Membe wengine tutawaona wakati wa kumchagua mwenyekiti wa CCM Taifa au katika kumpitisha mgombea uraisi wa CCM mwaka 2020.

Mh.Membe namuona ni kama mtu alieamua kuonyesha njia ili wengine wenye nia nao wajiunge katika safari hiyo.
kwa sisi wenye kufikiri mbali Membe huyu ni Mfa maji anaye tapa tapa baada ya kukosa vyeo kila kona, moja alikuwa anautaka uraisi akakosa, pili alifikiri lazima atakuwa waziri wa mambo ya nje ndio maana alichelewa hata kukabidhi nyumba ya serikali aliyokuwa anaishi kama waziri kwani aliamini kuwa ni lazima atakuwa waziri,je haya anayo yaongea leo mda wote alikuwa wapi? pili anaogopa kwa kasi ya Magufili maslahi yake lazima yataguswa maana na yeye ni JIPU sugu, kwa sasa wanaoisoma namba ni hawa hawa wana ccm lakini na wapinzania kwa kutokujua wanashabikia kauli za Membe, nafikiri kaka yake Kikwete alifanya kila linalo wezekana ili awe Raisi kwa lengo la kulinda maslahi yao lakini ilishindikana kwa hiyo yeye atulie ANYOEWE.
 
Nchi haiongozwi kutoka kichwani, inaongozwa kwa mjibu Wa sheria na katiba.

Kwa hiyo swala la kulipa kodi siyo la hiari na wala halijaletwa na Magufuli lipo kisheria. Sasa Membe atuambie angekuwa rais yeye angeongoza kutoka kichwani mwake au kwa kufuata sheria za nchi??

Na ndio maana Watz wengi tulikuwa hatutaki rais Wa kuchukua fomu huku ameandama na Kundi la watu ,madhara yake ndio haya, hapa Membe ni lzm anatetea rafiki zake wameguswa..

Asante Mungu kwa kutuebushia mbali watu Wa aina hii kuwa viongozi wetu
 
Na dhahiri. Nyuma ya Membe kuna vigogo/mapapa wakubwa. Hii ilipangwa kwa ufasaha mkubwa. Rejea: Sitta mara moja aliwahi kusema "Magufuli anashauriwa vibaya". Leo Membe anasema hayo. Je kuna uhusiano wowote wa kimkakati kati ya Sitta na Membe? Kwa akili ya kawaida nyuma ya pazia kuna "kitu kikubwa". Magufuli ajiongeze kwa hali zote.
 
Kwanza Magufuli ni rais wa ajali, hana cha kupoteza.

Wasipomchagua system watamchagua.

Na hii kazi anayoifanya ni system ndio inamuambia nini afanye. Analetewa mafaili yeye anatimiza.

Huu uchaguzi huko alipopita alipita kihalali?
 
Back
Top Bottom