Habari kutoka ndani ya kambi ya Benard Membe msaka urais kupitia Chama cha Mapinduzi, zimedokeza kuwa mtu wao huyo ana mzimu unamuandama.
Katika kufunguka kiduchu mtoa nyeti huyo anadai ndugu Membe katika harakati hizo na bidii ya kutafuta uungwaji mkono lakini Membe hauziki yaani ni kama bidhaa iliyododa.
Amefafanua kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiwatafuta wajumbe wa CCM wakiwemo wabunge kuwaomba kumuunga mkono Membe na kukubaliwa lakini baada ya siku kadhaa wakiwarudia wajumbe haohao imekuwa kama wanaanza upya.
Tunafanikiwa kuongea nao na kuwapa chao lakini baada ya siku chache au miezi michache tukiwarudia tunakuwa kama ndo tunatongoza upya anazidi kusema wengine wanadiriki kusema mtu wetu hauziki ni bidhaa iliyododa Anaongeza: hatujakata tamaa japo inavunja moyo
Katika hatua nyingine mtoa nyeti amedokeza kuwa Mheshimiwa wetu amekuwa akimhofu Lowassa na Wassira kuwa ndio washindani wake wakubwa japo Lowassa ni mgonjwa sana.