Membe kuwania urais 2015...

naomba niendelee na nukuu:
'Ikulu ni mahala patakatifu,
Ikulu sio pango la walanguzi'
mwisho wa nukuu.
(Source:Kambarage wa Mwitongo)
 

Umenisaidia mkuu,mimi ndo naenda kuchukua jimbo la mtama,membe anapeleka watu hija kila kijiji,katika jimbo lake,alimnunua mgombea wa kafu mwaka jana ili apite bila kupingwa,unajua yule wa TLP alichelewa kuludishwa
 

Niambie mwenzangu ulipigia kura kituo gani(jimbo la mtama)naona utakua unasimuliwa,mi nimepigia kura Madangwa,Mkono vs Membe=maendeleo katika jimbo mmmmh,hapo umeshemsha,Mkono anajenga shule zen anaipa serikali,Membe amefanya hayo mambo,nenda Nachunyu,mtegu,mnjonjo,ingawali,mnolela,mahumbika,kiwalala,shuka,londo,mtama vijijin,sisi tunataka maendeleo,jamaa ni mbunge wetu,ila hawez kua Rais,amemuangusha Abdul_aziz Lindi mjin(alimuunga mkono Balwany kupitia Cuf)nenda Lindi ukaulize,inaonyesha wewe ujui mambo ya Lindi.
 
Haya ndo mambo ambayo nayaona kama majibu kwa hoja yangu japo, ukizitaja hizo hospitali na shule itakuwa vizuri zaidi kama ushahidi.

Mwambie azitaje izo hospt na shule namsubiri nipo Madangwa
 
- Membe nafikiri ni best ever Foreign Minister we ever had, amepitia ngazi zote za Uongozi wa chini, amelitumikia Taifa kwa uaminifu bila wizi I understand kwamba njia iliyomfikisha hapo alipo haikuwa saafi sana so is Viongozi wetu karibu wote wa CCM na Upinzani, lakini in his case the end justifies the means, kutokana na kazi yake nzito ya kuleta stability huko juu na nidhamu pia, ana kura yangu akigombea!

Super Field Marshall Es!
 

Mimi nilipiga kura yangu Mahiwa. Katika historia yangu ya kupiga kura toka mwaka 1985 na kuchagua wabunge, jimbo la Mtama halijawahi kupata mbunge mwenye rekodi ya utendaji kama Membe. Tumeshuhudia mradi mkubwa wa Maji wa Chiuwe, wenye thamani ya shilingi milioni 800, mradi wa hospitali ya Rondo wa zaidi ya shilingi bilioni 1, mradi wa mahakama Rondo, mradi wa daraja la Nachui, miradi ya barabara. Ujenzi wa makanisa na misikiti na kupeleka mahujaji wa dini zote hija. Kusaidia vikundi vya wajasiri amali, miradi ya mashule na zahanati n.k. lakini kubwa na ambalo amejipambanua nalo ni kule kufanikisha kuvutia uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha cement Lindi mjini ambacho kitatoa ajira za moja kwa moja za zaidi ya wafanyakazi 3,500.

Mohamed Abdul-Aziz amekuwa mbunge wa Lindi mjini toka 1995 na katika kipindi chote hicho hakuwahi hata kujenga tundu moja la choo. Katika chaguzi mbili mfululizo amekuwa akishinda kwa mbinde tena na wapinzani dhaifu na arobaini yake ilikuwa inasubiriwa na kila mwenye akili pale Lindi. Aliposhindwa hakuna aliyeshangaa, hata yeye mwenyewe alijua kwa sababu 'hakuwekeza' jimboni na hata kura za maoni alichakachua.

Take it or leave it, record ya membe jimboni ni ya kupigiwa mfano katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Whether hicho ni kigezo cha urais mimi sijui!
 

Mheshimiwa huwezi sema tofauti na hili na hasa baada ya kujulikana Membe ni bosi wako.....kwanza declare interest kuwa wewe ni nani uko ubalozini.......we ever had.....ni bora kuliko JK na Mkapa kwahio....kwa lipi?siasa za miaka hio tz ikiheshimiwa kimataifa ni sawa na sasa.
 
Mkuu Field Marshal!!! Ama kweli sasa mwaka tunaumaliza vizuri,umerudi Kamanda?ulipotelea wapi ?? Kuna siku memba Ashadii alifungua uzi wa vigogo wa jf walio dissapear,na wewe uliunganishwa katika orodha,ilionyesha watu walikumisssooo,karibu Mkuu!
RESPECT! (source:Field Marshall).
 

Ubunge, uwaziri etc is one thing, na Urais is the other. Kuwa waziri mzuri au mbunge mzuri hakumaanishi kuwa utakuwa rais mzuri. I do not see Membe kuwa rais kwa kigezo cha perfomance yake bungeni.

JK was better MP kwa Chalinze, lakini angalia he is the worst Pressident Tanzania has ever seen
 
..rekodi ya Membe ni ipi?

..Mahakama ya Kadhi hajafanikisha.

..OIC hajafanikisha.

..Uraia pacha bado.

..ni kitu gani amekifanya mpaka astahili kugombea uraisi.

Kikwete alistahili vipi? Vigezo vya nani kafanya nini..kuna ambaye angemfikia Salim A. Salim kipindi kile?
 

Wote ni wanafiki na wasio amini wanaokisema!
 
hoja dhaifu kutoka kwa mtu makini.mleta mada wanatakiwa wakae karibu na aweda wajikosoe kabla hawaleta blaa blaa zao hapa.
 
omutwale, una hisa na mgombea yeyote ambaye unadhani Membe ni threat kwake? kwani lini Membe katangaza nia? au umekurupuka tu? Isitoshe robo tatu 3/4 ya posts za hii thread ni zako,, unalala humu kulinda hii thread? Unajiabisha mkuu
 
...........kaka umenena, maumivu tunayopata kutoka kwa jk ndio tutayapata kutoka kwa membe, tena even worse, hatuhitaji rais aina ya jk, rais anayetumia taili ya bendera kuongoza, yaani upepo unakoelekea na yeye kule kule.........
 
Ina maana Membe nae anataka kugombea urais? du hivi hawezi pima upepo? ameshupalia chenji ya rada mbona hatumsikii akisisitiza kukamatwa kwa waliotufikisha hapo na kuhujumu uchumi wa nchi maskini kama Tanzania? kwa ushauri tu kwa chama cha magamba,msimamisheni Membe 2015 ili mkione cha mtema kuni! yaani itakuwa ni ukombozi kwa watanzania.
 
omutwale, una hisa na mgombea yeyote ambaye unadhani Membe ni threat kwake?

Hapana. Sina. Na tena akinishawishi yeye LABDA anaweza kuwa chaguao langu

kwani lini Membe katangaza nia?

Sijasema waliotangaza nia. Nimesema

Omutwale
Katika orodha ya wanaotajwa kuwania uteuzi wa ccm kwa nafasi ya urais wa JMT-2015

..Isitoshe robo tatu 3/4 ya posts za hii thread ni zako,, unalala humu kulinda hii thread? Unajiabisha mkuu

Jibu lake ni rahisi sana. Mimi ndiye nimeanzisha mada. Kuna wanaoiunga mkono na kuna wanaiopinga. Wanaoipinga wanahitaji maelezo zaidi nami nahitaji melezo toka kwao. Kwa hiyo ulitaka nisiwajibu ili waseme nimewakimbia? Hata kwenye filamu kinara (steering) lazima haonekane zaidi!
 
hoja dhaifu kutoka kwa mtu makini.mleta mada wanatakiwa wakae karibu na aweda wajikosoe kabla hawaleta blaa blaa zao hapa.

Onyesha basi huo udhaifu wa hoja. Tuachane na kauli za kijumla jumla. Ebu tuje na mifano itakayotusaidia kuidhoofisha au kuiua kabisa hoja.
 
Mi sijasikia kitu cha maana, nakumbuka alivyomnyong'onyeza Mudhihir, mpaka akampa joka la mdimu, zaidi najua lazima V8 lake liwe jeusi, akiletewa jeupe anaenda kubadilisha liwe jeusi, na benzi moja naona analitumia nalo ni jeusi, najua anavaa cheni kubwa na anafungua kifungo ili ionekana, ki ufupi na namuona kama sharobaro, sina la zaidi ninalo lijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…