Membe kuwania urais 2015...

Membe kuwania urais 2015...

Jamani naweza nisiwe na hoja ........

Ni vema umejitambua na kujihukumu mapema na kwa haki.

......Katika swala la Pesa za radar, jambo moja ambalo niliona Membe ana kifua kipana ni pale alipotamuka kwamba pesa lazima zirudi .......

Sasa wacha tukusaidie ili ukirudi uwe na hoja.

Ndo maana nilisema kwenye hoja yangu ya msingi kwamba hili jambo naliacha ili watu walichokonoe na kulijadili kwa upana zaidi. Mh. Membe alidandia tukio ambalo lilikuwa lazima litokee katika mkondo na staili lilivyotokea. Naamisha fedha kurudishwa Tanzania tena kupitia serikalini ilikuwa si jitihada za Kamati ya Mh. Membe wala hisani bali lazima kutokana na amri ya mahakama-Uingereza na msukumo wa serikali ukichagizwa na wabunge. Matamko ya serikali za wenzetu yanaogopwa kama baa la njaa, na amri pamoja na hukumu za mahakama zao zinaheshimiwa. Sio kama Serikali ya Tanzania inatunishiwa kifua na Meneja wa Kampuni kama BP kisha inanywea.

Baada ya hukumu ya BAE iliyofuatiwa na kauli za serikali ya UK zikishagizwa na wabunge wakitaka BAE watekeleze hukuma kama walivyoagizwa, Mh. Membe akapata fursa ya “kuokota mpira nyavuni” wasiojua wakashangilia wakidhani Mtanganyika Mh. Membe ndiye kafunga goli!

BAE na kampuni yoyote ile haina jinsi yoyote ambayo inawawezesha kudharau au kutotii hukumu na amri za mahakama na zikabaki salama kibiashara katika nchi za wenzetu. Ndo maana walikubali haraka kulipa fine kwa baadhi ya vifungu vya kesi yao hata bila kusikilizwa. Mh. Membe analijua hili ndo maana akaandaa timu ya Wabunge na kuwatengenezea nafasi ya kula posho za ziara za kikazi nje ya nchi kwa shughuli isiyokuwepo. Vyombo vya habari vya ndani vikalishwa na kulisha watu kasa kuonyesha ukinzani usiokuwepo katika kulipa serikali fidia.

Hivi nikuulize swali; wafanyakzai wa BOT waliopokea hela za KAGODA zilizorejeshwa na Manji nao ni majasiri?
 
........Ila watu ndo wanapenda huyu Membe awe rais nafikiri kwa sababu ya haiba yake na mvut kwa watu. Ninja mengi ya kuamini kwamba kiongozi huyo ni presidential material.
......

mlagha,
Mbona tunaangushana na hoja uzuri wa sura?
Baba wa Taifa si alikwisha wapa jibu mwaka 1995, kama mnamchagua mtu kwa uzuri wa sura yake, basi si ombeni miadi naye mkanywe nae chai tu?!
 
Omutwale,

Unanishangaza kidogo unapoanza kwa kusema kuwa Membe hajakuvutia na kukushawishi kuwa anafaa kuwa mgombea urais. Kwanza kabisa, hoja yako ingekuwa na mantiki ikiwa Membe angekuwa ametangaza nia na kuanza kushawishi wanachama wa CCM na wananchi kuwa anataka kuwa mgombea. Sasa unataka ushawishikaje na mtu ambaye si mgombea wala hajaanza kazi ya ushawishi? ...............

Rejea hapa:

Katika orodha ya wanaotajwa kuwania uteuzi wa ccm kwa nafasi ya urais wa JMT-2015, namba mbili (2) katika nisio shawishika nao ni Mh. Bernard Membe....:

Nawatakia Mwaka Mpya Mwema na Wenye Mafanikio.
Omutwale kutoka Kanyigo.

Nimesema HAJANISHAWISHI kuepuka tabia ya waliowengi kutaka kujichukulia nafasi ya jamii nzima na kutaka kuonyesha machaguo yao ndiyo yanastahili kuwa machaguao ya jamii nzima. Lakini pia ikumbukwe nami pia ni mpiga kura mwenye haki zote stahili za kumchagua iwapo nitashawishiwa na kukubali kufanya hivyo. Even a single vote, counts!.
 
La pili membe ni miongoni mwa mawaziri wachache ambao angalau wamejenga hata hospitali na shule katika majimbo yao. lowassa kaishia kujenga nyumba na kununua nyumba yeye na mwanaye huko London na Arusha kuchukua kila eneo na kujenga majumba.
.

Haya ndo mambo ambayo nayaona kama majibu kwa hoja yangu japo, ukizitaja hizo hospitali na shule itakuwa vizuri zaidi kama ushahidi.
 
...Membe habagui watanzania walio nje na wa ndani kama mnavyotaka. Yeye anaona ni watanzania wanaostahili kuheshimiwa na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Ninyi mnataka wabaguliwe kwa sababu tu wameenda kuosha macho ulaya. Hii dhambi gani jamani..

Tofautisha kwenda nje ya nchi yako kusaka utaalamu au mali na kurudi na kuwa na uraia wa nchi mbili. Anayekwenda kuosha macho ni tofauti na anayeondoka au anayekuja lakini anataka apate kote.
 
Maskini Omutwale, chuki na kutumiwa kumekunyima fursa adhimu ya kufanya utafiti wa mambo ambayo ni very basic.

1. Membe amekuwa mbunge wa jimbo la Mtama kuanzia Novemba 2000 na muhula wake wa kwanza ulikwisha mwaka 2005. Katika historia ya jimbo la Mtama hakujawahi kutokea mbunge aliyetekeleza ahadi na kuanzisha miradi ya maendeleo Kama Membe. Kitakwimu, Membe ni kati ya wabunge wachache sana hapa nchini waliowekeza majimboni kwao, labda akitanguliwa na Mh. Nimrod Mkono. Ukiangalia miradi ya maji, afya, elimu na hata miundombinu na masuala ya kiimani utagundua kwamba ulichongea wewe hakina hata chembe ya ukweli kuhusu utendaji wa Membe jimboni kwake. Swali la kujiuliza ni je, ni mgombea yupi, akiwemo Slaa mwenye sifa ya utumishi bora jimboni unaomshinda Membe?

2. Msimamo kuhusu rada ulikuwa ni msimamo wa serikali na Membe Kama waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje. Msimamo wa serikali ulikuwa ni kwamba chenji irejee serikalini, kosa lake Kama mtendaji na mtendaji na mtekelezaji wa maamuzi ya baraza la mawaziri ni nini? Mgombea makini angefanya tofauti na hivyo? Hiyo isingeitwa insubordination? Msimamo wa mgombea wako makini katika hili ni upi?

3. Hakuna siri kwamba Gadaffi alikuwa ni kiongozi wa nchi ambayo ilikuwa na uhusiano na Tanzania. Uhusiano huu haukuanza leo na wala haukuanza wakati wa uwaziri wa Membe. Leo hii hata ICC wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo chake. Hii ni kwa vile kilikuwa cha kikatili na kisichostahili katika mazingira hayo. Msimamo wa serikali wakati wote ni kutatua mgogoro huu kwa amani. Ndiyo ulikuwa msimamo wa AU pia. Mtu anaweza asiupende msimamo huo lakini kwa kutokubaliana nao haumfanyi Membe kuwa mtu asiyefaa kuwa Rais japonica yeye mwenyewe hajawahi kutangaza nia.

4. Suala la mahakama ya kadhi na suala la OIC ambayo ni moja ya kero za muungano lililo chini ya wizara ya nje yalikuwa ni sehemu ya ahadi za CCM kwa wana chi 2005 na walioitunga ilani hiyo wanafahamika na winging leo ndo wapiga debe wa baadhi ya wagombea wanaosifiwa sana. Yeye alijibu kwamba watu waache kuwatia wananchi hofu juu ya OIC na badala yake waachwe wajadili faida na hasara zake na baadae akaliarifu bunge juu ya kusitishwa kwa mchakato kuruhusu mageuzi ndani ya taasisi hiyo. Tatizo liko wapi?

5. Siri za baraza! Kichekesho Kikubwa! Ilibainika kwamba Membe hakuwepo kwenye kikao husika na isingewezekana avujishe siri ambazo alikuwa hazijui na Rais alipogundua kwamba hizo ni adolescent machinations za waliokata tamaa akazipuuza na watuhumu (those who were baying for Membe's blood) wakaaibika sana.

Ninachokiona katika thread hii ni woga na kuweweseka kwa mgombea mmoja ambaye kila mara amekuwa akijigamba kuwa na mtaji wa kimtandao lakini kila siku ushahidi wa kumiss kujiamini kwake kunadhihiri, kwa kupaka matope wenzie, kuwatisha na hata kudiriki kudhuru wenzie. Lakini si ni vyema tukahoji miaka zaidi ya 20 ya ubunge wa jimbo lake ana nini la kujivunia? Na ile ahadi ya ng'ombe kwa kila kaya chini ya "kopa ng'ombe lipa ng'ombe" ya mwaka 2003 kule mikoa ya kusini imeishia wapi?

Hoja yako haina mashiko na haina mnunuzi kwa sababu imekosa chembe chembe muhimu za kuipa sifa ya kujadiliwa kwa mapana. Ndo maana kuna kujihami kwingi. Mradi umeanza, basi utapata haki yako.
 
Tofautisha kwenda nje ya nchi yako kusaka utaalamu au mali na kurudi na kuwa na uraia wa nchi mbili. Anayekwenda kuosha macho ni tofauti na anayeondoka au anayekuja lakini anataka apate kote.

Inaelekea hii concept ya diaspora ambayo sasa imeshika kasi katika nchi nyingine zenye viongozi makini, wewe na wakubwa zako hamuijui na sishangai maana inahitaji elimu zaidi ya ile ya sanaa za maonyesho kuijua. Halafu unataka kujua shule na hospital ili uthibitishe nini? Uliza ikulu, ziara ya Rais 2007 ilifungua miradi ipi jimboni Mtama halafu utajua. Katika uchaguzi uliopita Membe alishinda kwa zaidi ya 75 asilimia. Ulitaka landslide iweje? Unataka iwe Kama jimbo la yule jamaa ambaye alipata kura nyingi kuliko idadi ya wakazi?

Petty issues ulizozileta zimeibua kukosa utafiti na ufahamu wa siasa za nchi, Mtama na hata hukumu la waziri Membe na wizard yake. Ni vizuri ukatumia muda huu kuendelea kumtakasa na kumpaka manukato mgombea wenu ka la hamjamleta tumsulubu kwa kutuibia hazina na rasilimali zetu. Kama Membe Hana sifa kwa nini tumjadili? Si stamina mwenyewe?
 
Mbopo kama hii ndo haki yangu, basi nimedhurumiwa.

Kweli hela ni noma. Unakesha humu kuilinda hoja yako, ndio maana nusu ya post humu ni zako. Put in simple terms: EL anaugulia possibility ya Membe presidency na sasa hajapata dawa ya kuzuia hili. Nakushauri uende Mtama, badala ya kutumika tu. Hujachelewa.
 
Well welii membe lazima ashinde urais maana kampeni inaongozwa na mtoto wa kigogo mkubwa lakini ni ngumu kufanikiwa hasa anapojitahidi kucheka na kumimitate bwana mkubwa wa nchi.......Membe ni chaguo la Mungu japo Mungu haungi mkono unafiki sasa hapo sijui itakuwaje.
 
mkubwa,unavyosema huu umbea hapa utadhani kuna uhalisia wowote.
tafadhali hata kama mmetumwa leteni hoja na sio hadithi za kutunga sebuleni kwa EL.
OTIS

Mmh yangu macho; hii ni hoja ya nguvu ama nguvu ya hoja?
 
..rekodi ya Membe ni ipi?

..Mahakama ya Kadhi hajafanikisha.

..OIC hajafanikisha.

..Uraia pacha bado.

..ni kitu gani amekifanya mpaka astahili kugombea uraisi.
 
Maskini Omutwale, chuki na kutumiwa kumekunyima fursa adhimu ya kufanya utafiti wa mambo ambayo ni very basic.

1. Membe amekuwa mbunge wa jimbo la Mtama kuanzia Novemba 2000 na muhula wake wa kwanza ulikwisha mwaka 2005. Katika historia ya jimbo la Mtama hakujawahi kutokea mbunge aliyetekeleza ahadi na kuanzisha miradi ya maendeleo Kama Membe. Kitakwimu, Membe ni kati ya wabunge wachache sana hapa nchini waliowekeza majimboni kwao, labda akitanguliwa na Mh. Nimrod Mkono. Ukiangalia miradi ya maji, afya, elimu na hata miundombinu na masuala ya kiimani utagundua kwamba ulichongea wewe hakina hata chembe ya ukweli kuhusu utendaji wa Membe jimboni kwake. Swali la kujiuliza ni je, ni mgombea yupi, akiwemo Slaa mwenye sifa ya utumishi bora jimboni unaomshinda Membe?

2. Msimamo kuhusu rada ulikuwa ni msimamo wa serikali na Membe Kama waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje. Msimamo wa serikali ulikuwa ni kwamba chenji irejee serikalini, kosa lake Kama mtendaji na mtendaji na mtekelezaji wa maamuzi ya baraza la mawaziri ni nini? Mgombea makini angefanya tofauti na hivyo? Hiyo isingeitwa insubordination? Msimamo wa mgombea wako makini katika hili ni upi?

3. Hakuna siri kwamba Gadaffi alikuwa ni kiongozi wa nchi ambayo ilikuwa na uhusiano na Tanzania. Uhusiano huu haukuanza leo na wala haukuanza wakati wa uwaziri wa Membe. Leo hii hata ICC wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo chake. Hii ni kwa vile kilikuwa cha kikatili na kisichostahili katika mazingira hayo. Msimamo wa serikali wakati wote ni kutatua mgogoro huu kwa amani. Ndiyo ulikuwa msimamo wa AU pia. Mtu anaweza asiupende msimamo huo lakini kwa kutokubaliana nao haumfanyi Membe kuwa mtu asiyefaa kuwa Rais japonica yeye mwenyewe hajawahi kutangaza nia.

4. Suala la mahakama ya kadhi na suala la OIC ambayo ni moja ya kero za muungano lililo chini ya wizara ya nje yalikuwa ni sehemu ya ahadi za CCM kwa wana chi 2005 na walioitunga ilani hiyo wanafahamika na winging leo ndo wapiga debe wa baadhi ya wagombea wanaosifiwa sana. Yeye alijibu kwamba watu waache kuwatia wananchi hofu juu ya OIC na badala yake waachwe wajadili faida na hasara zake na baadae akaliarifu bunge juu ya kusitishwa kwa mchakato kuruhusu mageuzi ndani ya taasisi hiyo. Tatizo liko wapi?

5. Siri za baraza! Kichekesho Kikubwa! Ilibainika kwamba Membe hakuwepo kwenye kikao husika na isingewezekana avujishe siri ambazo alikuwa hazijui na Rais alipogundua kwamba hizo ni adolescent machinations za waliokata tamaa akazipuuza na watuhumu (those who were baying for Membe's blood) wakaaibika sana.

Ninachokiona katika thread hii ni woga na kuweweseka kwa mgombea mmoja ambaye kila mara amekuwa akijigamba kuwa na mtaji wa kimtandao lakini kila siku ushahidi wa kumiss kujiamini kwake kunadhihiri, kwa kupaka matope wenzie, kuwatisha na hata kudiriki kudhuru wenzie. Lakini si ni vyema tukahoji miaka zaidi ya 20 ya ubunge wa jimbo lake ana nini la kujivunia? Na ile ahadi ya ng'ombe kwa kila kaya chini ya "kopa ng'ombe lipa ng'ombe" ya mwaka 2003 kule mikoa ya kusini imeishia wapi?

Hoja yako haina mashiko na haina mnunuzi kwa sababu imekosa chembe chembe muhimu za kuipa sifa ya kujadiliwa kwa mapana. Ndo maana kuna kujihami kwingi. Mradi umeanza, basi utapata haki yako.

Mbopo,
Asante kwa kujitokeza kujibu hoja zangu.

Jambo moja la haraka katika majibu yako, kila ambaye hajashawishika au kuridhika na utendaji wa Mh. Membe basi ni kibaraka wa EL! Na kwa formula hii nyepesi inayosaidia wenye kutafuta uraisi katika kufikiri, Omutwale=Kibaraka wa EL! Mkiitumia kanuni hii mtawapoteza wengi ambao wangekuwa wa msaada kwenu.

Ombi; nivumilie maana huku umeme umekatika. Hapa natumia kitochi cha TECNO. Ukirudi nitakujibu au kuafiki vipengele ambavyo nimekubalina nawe.
 
Kwani jamani wana JF , EL bado ni mwanasiasa wa Tanzania mwenye credibility ya kufikiriwa kwenye urais?
Kweli Watanzania tunahitaji mental emancipation kama alivyosema Mchungaji Mtikila.
Hivi tumelogwa???
Among 42 millions hakuna wengine zaidi ya hawa wenye scandals za kila siku?
Au kuwa credible politicians ni scandals?
Poor Tanzanians, I wish Nyerere angerudi kutusaidia, we are so blind and short sighted.

Wana JF,
Ni umefika wakati mwingine wa kufikiria ustaarabu na mwelekeo tofauti, sasa hivi wimbo ni ule ule, watu ni wale wale, kana kwamba watu wanaotakiwa kuongoza ni hao hao, watu tumesahau sifa za kiongozi ambazo ni uadilifu na kufuata miiko ya uongozi, ukitangulizwa na hekima na busara, hizi nguvu za kuungwa mkono au nguvu za noti ndizo zinazozaa viongozi wasio kuwa na uchungu wa nchi
Nawakilisha
 
Mwaka 2015- Rais wa JMT! Hivi kwa wakati huo Muunganoutakuwepo; au utaondoka na huu mvuke wa katiba – mara inaitwa mpya, wenginewanasema ni ya zamani ktk cover jipya, wengine wanasema 80% ya katiba ya sasaitabaki kama ilivyo na kuongozewa nyama kidogo, ili mradi tu ipatikane kabla ya2015. Wa-visiwani wanataka iwe zamu yao kutoa rais wa JMT, vipi hilolimezingatiwa na vyama vyote vya siasa au mmeziba masikio! Ngome inogile
 
Kweli hela ni noma. Unakesha humu kuilinda hoja yako, ndio maana nusu ya post humu ni zako. Put in simple terms: EL anaugulia possibility ya Membe presidency na sasa hajapata dawa ya kuzuia hili. Nakushauri uende Mtama, badala ya kutumika tu. Hujachelewa.

Unamkosea sana Omutwale kumfanya bidhaa inayonunulika na EL au yeyote yule. Na hizi prejudices jaribuni kuzipunguza. Zina athari zake kwenye mapambano kama haya ambayo hujui kwa usahihi nani tayari kaamua kuwa kinyume nawe na nani akishawishiwa kwa hoja atakuja upande wako.

Katika masuala ya Masoko na Uvumishaji (Katika siasa mnaita Uenezi), suala la kuchukua muda mwingi kukebehi na kukandia bidhaa shindani mbele ya mteja aliijengi brand yako bali linashangia kutangaza bidhaa shindani na kupelekea wanunuzi kutaka kujua hiyo bidhaa shindani ina nini mpaka kila mara huitaje. Namaanisha kwamba kwa Staili hii ya kumbandika EL kwa kila mtu na kumtajataja hovyo si kama mnambomoa bali ndo mnamjenga. EL alikwishajifia kisiasa ila mbinu zenu dhaifu ndo zinamuibua tena.
 
Jamaa ana hata mvuto wa kuwa raisi kabisa......hana hata historia ya kuwa mwanasiasa makini,lakini pia utendaji wa serikali hii ya tatu umepoteza umaarufu wa wanasiasa wengi sana,maana kwasasa kama unataka kuonekana kuwa ni bora kwenye hii serikali unapaswa uwe na jitihada binafsi kama John Pombe Magufuli....kwa ujumla hakuna team work kabisa na hata wale wanasiasa waliokuwa wanaonekana bora baada ya kukubali kuingia kwenye serikali ya JK wamepoteza mvuto kwa jamii mfano Sitta na Mwakyembe...

Kwa ujumla Membe hana uwezo wa kufanya mambo kupandisha credibility yake nje ya serikali ya JK ambayo haina uwezo wa kutoa hiyo nafasi kwasasa,badala yake inatoa nafasi kubwa ya kuua credibility ya wanasiasa wengi waliokuwa wanakubalika kwasasa.
 
kaaaaaaaaazi kweli kweli!
Hivi Ikulu kuna biashara gani? (source:Kambarage wa Mwitongo).
 
kwa upande wangu sishangai wala sitashangaa kwani hata jk hakuwa na jipya allofanya alipoteuliwa kugombea urais, ni kawaida ya chama cha magamba yan ciciemu
 
Back
Top Bottom