Kwanza naomba nikiri kwamba sijawahi kuona thread ya kijinga, iliyojaa uongo, upotoshaji wa maneno, matukio na takwimu kama hii. No wonder aliyepost amevizia watu wakiwa wamekwendaakulala ili asije aka-incur wrath hiyo.
Kwanza hajaeleza maamuzi hayo ambayo yanapelekwa au yanafanywa kwa nia ya kumpendelea Membe ni yapi, yanahusu nini na yalitolewa wapi na lini? Mtu makini angeweza ku-cite hata mfano mmoja ili kuhalalisha hoja yake lakini anaishia tu kutoa maneno ya jumla. Kwa mara nyingine huu ni uthibitisho kwamba kumbe pamoja na mbwembwe zote zile za kwamba mkubwa wao kamrejeshea gamba mwenyekiti, na kuzunguka parokia kwa parokia, kigango kwa kigango kwa kigango na hata usharika kwa usharika, chombo kinaendelea kuchota maji na karibu abiria wataanza kujitosa ili wajiokoe. Fedha zilizomwagwa Dodoma na kwenye harambee bado hazijatakasa na kununua mapenzi ya wananchi.
Katika mfumo wowote wa utawala wa nchi na chama kuna watu wanaweza kuombwa ushauri na kutoa input katika hili au lile na inawezekana kwamba (kama kuna ukweli) Membe alishauriwa ili atoe wamoni yake kutokana na weledi wake kwa jambo hilo na si vinginevyo. So far hatujaona mabadiliko ya katiba au kanuni yanayoweza kuashiria kwamba kuna namna ambayo inaandaliwa kumpendelea yeyote kati ya wale wanaowania urais (kwa bahati mbaya Membe hajatangaza kuwania. Infact amekanusha kwamba ana mpango wa kuwania).
Upotoshaji:
1. Musalia Mudavadi hakuondoka Kanu baada ya Uhuru kuteuliwa kuwa mgombea. In fact Musalia alikuwa Mgombea Mwenza wa Uhuru na hata alizawadiwa kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa muaminifu kwa Moi.
2. Raila odinga hakuwa NDP. NDP ilikufa mwezi Februari, 2002 pale New Kanu ilipozaliwa Kasarani.
3. Wilson Mukama hakuwa jiji kabla ya Keenja. Yeye amekuja baadae tena baada ya kuwa Kinondoni, Temeke na Ilala zimeshakuwa Manispaa. Hilo la kwamba Keenja alikuja kunyoosha makosa ya Mukama ni uongo na selective memory. labda kama ulikuwa jela wakati huo au ulirukwa na akili.
Ushauri:
Mimi nakushauri wewe, na wanamaliwato wenzio wa mafisadi mjitahidi kuja hapa na takwimu na hoja za maana na zenye ukweli, siyo kukurupuka tu kutokana na hofu na kuchanganyikiwa kunakotokana na kutotimia kwa malengo yenu. Kwa taarifa yako, kanuni hazitabadilishwa kwa nia ya kumpendelea Membe au yeyote yule. Zinaweza kubadilishwa kuzuia mtu asiye na sifa ya kuwa na urais, kutokana na uwezo wake wa uelewa, uadilifu wake na afya yake (sifa ambazo Lowassa zinambana).
Huko nyuma ilishaelezwa kwamba WE MAY NOT KNOW WHO WILL BE THE NEXT PRESIDENT, BUT WE KNOW FOR SURE WHO WILL NOT BE. IT IS EDWARD NGOYAI LOWASSA!
Watch this space!
Mbopo, naona umefura povu na hakika siyo bure.
Hapo kwenye Red Bold juu naona unamsemea kwa kukubali na papo hapo unakataa. Rejea pia bandiko langu, hakuna mahali nilitaja ni nani mlengwa wa mabadiliko ya hizo kanuni. Glad to see that you 'catching up' really fast.
Je, bado unaamini kuwa kanuni na katiba hazibadilishwi ili kupunguza nguvu za akina ENL ndani ya CCM? Rejea taarifa za Nape na Mukama kutaka kujua nani kavujisha siri za ndani au mikakati ya chama. Na vile vile kutishia kuwashitaki au kushitaki gazeti mojawapo.
Usiwe blinded na loyalty kiasi hicho. Try and step away from behind the camera, and may be you can get a better perspective of where you are standing.
Na kuhusu hivyo vipengele vitatu ulivyoviorodhesha hapo kama nukuu ya upotoshaji, ni wazi kuwa unachojaribu kufanya ni ku-split hair ili uonekane umechambua. It is still the same damn hair.
1. Ni kweli Moi alimpa Musalia u-vice wiki sita za mwisho kuelekea uchaguzi ili ampe support Uhuru, lakini ambacho husemi ni kuwa Musalia alimtolea nje Uhuru na haku-campaign naye hata mara moja pamoja na yeye Musalia kuwa VP wa Moi wakati huo. Musalia alizawadiwa na Odinga 2007 kwa 'ushujaa' huo japokuwa alisota miaka 5 bila ubunge wala nafasi yoyote kubwa.
Kwa hiyo anaweza kuwa hakuondoka KANU per se, lakini matendo yake yalimtupa Uhuru ambaye alikuwa ni Project ya Moi.
2. Raila alikuwa NDP hadi hiyo 2002, walipovunja old KANU na NDP kuunda KANU mpya. Ni upotofu unaposema kuwa Raila Odinga hakuwa NDP. Raila ndiyo kaiingiza NDP katika mseto na KANU baada ya kupewa uwaziri. NDP ilivunjwa kama trick ya Moi ku-consolidate support within KANU, na baadaye kuipeleka hiyo support yote kwa Project Uhuru.
3. Ok, inawezekana hili la Mukama kuwa jiji kabla ya Keenja labda kweli nilikuwa jela kipindi hicho (usinikumbushe maumivu hayo, bado naugulia). Lakini urahisi zaidi, jiulize Mukama alikuwa wapi kabla na hasa kipindi cha Sumaye akiwa Waziri Mkuu? Jibu ni rahisi sana, na hakuna haja ya kufoka mapovu.
Kwa taarifa zako pia, sasa suala la mabadiliko ya kanuni na katiba ya Chama linawawia ugumu na hii yote ni kutokana na kufanya mambo kienyeji bila kuwa na ushauri wa kisheria.
Muundo wa Tume ya Maadili na Nidhamu umekwama, siyo kwa utashi bali ni kwa kuwa wanashindwa kupata majina Bara na Visiwani ambayo hayataleta muelekeo wa kupendelea upande wo wote, lakini pia mtu wako abebwe. Yaliyoikwamisha Kamati ya Mwinyi, Msekwa na Kinana yanajirudia tena.
Na pia muhimu zaidi ni kuwa, mabadiliko yote yanayogusa Katiba ya Chama (siyo kanuni) ni lazima yapate baraka za Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu kabla ya kufanyiwa kazi. Japo wamejaribu kuiita hii ni 'Tume' yenye maamuzi na siyo Kamati, ili kukwepa kuigusa Katiba, suala linakuja ni wapi 'Tume' inapata nguvu ya Kikatiba ya kutoa maamuzi nje ya Kamati zinazotambulika na Katiba? Na nani anaipa 'Tume' hiyo hizo nguvu nje ya Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu? Ngoma inogile!
Labda Mpobo unaweza kujitolea kuwapa ushauri wa ki-sheria.
Hili la Lowassa kuwa Rais ni suala ambalo linamla sana "Joka La Mndimu", nadhani pengine kuliko hata Lowassa mwenyewe. Soma maandiko yangu sehemu mbali mbali katika forum hii na utagundua kuwa mimi ni mmojawapo wa wasiotaka Lowassa kuwa Raisi, kama vile ambavyo nisingetaka Membe kuwa Rais vile vile. Sifichi.
Na kama ikibidi kati ya hawa wawili Membe na Lowassa mmoja wao apite kuwa mgombea wa CCM, then ni bora mara mia iwe Lowassa kwani nitajua nasimamia wapi na ninapambana nacho kuliko iwe Membe asiye na msimamo, ambaye ni Kikwete katika sura nyingine. Tulifanya makosa hayo 2005 kwa kuaminishwa kuwa 'akiingia Ikulu atabadilika', na sasa anamaliza akiwa yule yule tuliyemjua na probably even worse kwani sasa kashika rungu sokoni.
And I am not blinded by ignorant loyalty, simply because I am only loyal to my own cause.
Subiria mrejeo wa akina Mbita, Mangula, Ameir katika siasa za ki-taifa ndani ya CCM, halafu tuongee tena. Mark my Words.