Membe kuwania urais 2015...

Membe kuwania urais 2015...

Kuna Mtu moja tu mzuri kuliko Membe CCM na ni Magufuli wengine wote si wazuri kama Membe kwa mawazo yangu na nimekutana na viongozi wengi isipokuwa Pinda. Membe nimempenda kwa

1. Yuko Tajari kubadilika na hafati mikumbo
2. Anasikiliza
3. Anajua dunia inapokwenda tumechoshwa na watu ambao hawajui dunia inaendaje

Lakini Magufuli ni Mzuri zaidi lakini watu wengi wanamwogopa!
 
How old will Magufuli be i 2015?

and what has he achieved so far as:

a) Politician

b) Minister
 
Hizi habari zimekuwa zinazunguka kwa muda sasa, ila kwa karibuni zimepata kasi na mwelekeo mpya.
Kwa wale wanaokumbuka, vijana wa UVCCM Pwani walitamka wazi kwenye kikao chao kuwa "Rais Kikwete anamjua nani atakuwa Rais", na mengineyo kuwa hatatoka kaskazini. Salva na Premi hawajawahi kukanusha wala kutoa tamko lolote kama kawaida pale ambapo JK 'anasingiziwa' kitu.

Taarifa za watu ambao tumekuwa na mawasiliano nao pale Magogoni na Lumumba ni kuwa sasa mkakati ni kama umekuwa wazi. Kuna masuala ambayo wamekuwa wanafanya na kutekeleza, ila sasa wamekuwa wanaulizwa kila hatua kuwa, je, Membe anajua au Membe amepewa taarifa?
Mengi ya masuala hayo hayahusiani kabisa na shughuli za Membe ki-chama wala ki-serikali, ila ni mambo ambayo yanabidi yaende juu hadi kwa Rais au Waziri Mkuu, au kwa Mwenyekiti au Katibu Mkuu.

Uzito wa masuala hayo yanategemeana na nini. Kuna suala moja zito la ki-serikali ambalo Mkulu alipewa taarifa na yeye akatoa kauli kuwa ‘Mwambie Membe aliangalie'. Masuala ya aina hiyo kawaida hupitia kwa Rais au Waziri Mkuu kwani ni mojawapo ya masuala ya ki-utendaji na ki-maamuzi serikalini, na yanagusa wizara ambazo siyo za Membe.

Kwa upande wa ki-chama, kuna maamuzi na mikakati ambayo imependekezwa na inafanyiwa kazi kwa nia ya kupunguza nguvu nyingi za vikao vya chama, na kumfanya Mwenyekiti au Katibu Mkuu kupitia Sekretariati kuwa na nguvu pasipo kikomo. Yote haya yanasukumwa ili yaweze kutekelezeka kabla ya 2012, ili kupunguza nguvu za Mkutano Mkuu na uchaguzi wa chama 2012. Kuna wanaoamini kuwa hiyo ni njia ya kumpa Membe mwanya ndani ya chama, kwani inaeleweka kuwa hana nguvu yo yote ndani ya Kamati Kuu, NEC wala Mkutano Mkuu, na hivyo hataweza kupata nafasi yo yote ya kupitishwa kwa kutumia katiba na kanuni zilizopo sasa.

Kwa wafuatiliaji wazuri wa masuala haya, tutakumbuka kuwa Moi alijaribu kufanya hivyo 2002 wakati wa KANU na Project Uhuru. Moi alibadilisha uongozi wa juu wa KANU, na kuvuruga taratibu zote za ki-chama ili kumpa nguvu Uhuru ndani ya KANU ili aweze kugombea na kushinda u-Rais wa Kenya. Matokeo yake ni kuwa akina Odinga (NDP), Kamotho, Kilonzo, Ntimama, Saitoti, Mudavadi na wengine waliitosa KANU na hatimaye kusababisha KANU kupoteza. Na pia kutokana na mabadiliko hayo, yaliidhoofisha KANU kiasi kwamba kanuni na taratibu zao mpya, zikawa ndiyo kikwazo cha KANU kujaribu kufufuka tena.

Mukama, kwa ushauri wa Kikwete na Membe, wanaipeleka CCM huko huko na Mukama anaelekea kuifanya CCM jinsi alivyolifanya Jiji la Dar, kabla ya jiji kuja kuokolewa na Keenja.

Lakini vile vile hili linaweza kuwa jambo jema, kwani hakuna kitu kibaya kama kubadilisha sheria na kanuni mathubuti ili kuwabana watu au kundi fulani, halafu kesho na kesho kutwa mabadiliko hayo hayo yanakuja kuwabana hao hao walioasisi.

Tumeona Kenya kwa KANU, Malawi kwa Mulunzi, Zambia kwa Chiluba, South Africa kwa Mbeki na kabla ya hapo De Clerk kwa Mandela, Ivory Coast kwa Gbagbo, Mexico kwa Salinas/Fox, na pengine sasa inaweza ikawa zamu yetu pia.

924mousetrap.jpg
 
Hizi habari zimekuwa zinazunguka kwa muda sasa, ila kwa karibuni zimepata kasi na mwelekeo mpya.
Kwa wale wanaokumbuka, vijana wa UVCCM Pwani walitamka wazi kwenye kikao chao kuwa “Rais Kikwete anamjua nani atakuwa Rais”, na mengineyo kuwa hatatoka kaskazini. Salva na Premi hawajawahi kukanusha wala kutoa tamko lolote kama kawaida pale ambapo JK 'anasingiziwa' kitu.

Taarifa za watu ambao tumekuwa na mawasiliano nao pale Magogoni na Lumumba ni kuwa sasa mkakati ni kama umekuwa wazi. Kuna masuala ambayo wamekuwa wanafanya na kutekeleza, ila sasa wamekuwa wanaulizwa kila hatua kuwa, je, Membe anajua au Membe amepewa taarifa?
Mengi ya masuala hayo hayahusiani kabisa na shughuli za Membe ki-chama wala ki-serikali, ila ni mambo ambayo yanabidi yaende juu hadi kwa Rais au Waziri Mkuu, au kwa Mwenyekiti au Katibu Mkuu.

Uzito wa masuala hayo yanategemeana na nini. Kuna suala moja zito la ki-serikali ambalo Mkulu alipewa taarifa na yeye akatoa kauli kuwa ‘Mwambie Membe aliangalie’. Masuala ya aina hiyo kawaida hupitia kwa Rais au Waziri Mkuu kwani ni mojawapo ya masuala ya ki-utendaji na ki-maamuzi serikalini, na yanagusa wizara ambazo siyo za Membe.

Kwa upande wa ki-chama, kuna maamuzi na mikakati ambayo imependekezwa na inafanyiwa kazi kwa nia ya kupunguza nguvu nyingi za vikao vya chama, na kumfanya Mwenyekiti au Katibu Mkuu kupitia Sekretariati kuwa na nguvu pasipo kikomo. Yote haya yanasukumwa ili yaweze kutekelezeka kabla ya 2012, ili kupunguza nguvu za Mkutano Mkuu na uchaguzi wa chama 2012. Kuna wanaoamini kuwa hiyo ni njia ya kumpa Membe mwanya ndani ya chama, kwani inaeleweka kuwa hana nguvu yo yote ndani ya Kamati Kuu, NEC wala Mkutano Mkuu, na hivyo hataweza kupata nafasi yo yote ya kupitishwa kwa kutumia katiba na kanuni zilizopo sasa.

Kwa wafuatiliaji wazuri wa masuala haya, tutakumbuka kuwa Moi alijaribu kufanya hivyo 2002 wakati wa KANU na Project Uhuru. Moi alibadilisha uongozi wa juu wa KANU, na kuvuruga taratibu zote za ki-chama ili kumpa nguvu Uhuru ndani ya KANU ili aweze kugombea na kushinda u-Rais wa Kenya. Matokeo yake ni kuwa akina Odinga (NDP), Kamotho, Kilonzo, Ntimama, Saitoti, Mudavadi na wengine waliitosa KANU na hatimaye kusababisha KANU kupoteza. Na pia kutokana na mabadiliko hayo, yaliidhoofisha KANU kiasi kwamba kanuni na taratibu zao mpya, zikawa ndiyo kikwazo cha KANU kujaribu kufufuka tena.

Mukama, kwa ushauri wa Kikwete na Membe, wanaipeleka CCM huko huko na Mukama anaelekea kuifanya CCM jinsi alivyolifanya Jiji la Dar, kabla ya jiji kuja kuokolewa na Keenja.

Lakini vile vile hili linaweza kuwa jambo jema, kwani hakuna kitu kibaya kama kubadilisha sheria na kanuni mathubuti ili kuwabana watu au kundi fulani, halafu kesho na kesho kutwa mabadiliko hayo hayo yanakuja kuwabana hao hao walioasisi.

Tumeona Kenya kwa KANU, Malawi kwa Mulunzi, Zambia kwa Chiluba, South Africa kwa Mbeki na kabla ya hapo De Clerk kwa Mandela, Ivory Coast kwa Gbagbo, Mexico kwa Salinas/Fox, na pengine sasa inaweza ikawa zamu yetu pia.

Kwanza naomba nikiri kwamba sijawahi kuona thread ya kijinga, iliyojaa uongo, upotoshaji wa maneno, matukio na takwimu kama hii. No wonder aliyepost amevizia watu wakiwa wamekwendaakulala ili asije aka-incur wrath hiyo.

Kwanza hajaeleza maamuzi hayo ambayo yanapelekwa au yanafanywa kwa nia ya kumpendelea Membe ni yapi, yanahusu nini na yalitolewa wapi na lini? Mtu makini angeweza ku-cite hata mfano mmoja ili kuhalalisha hoja yake lakini anaishia tu kutoa maneno ya jumla. Kwa mara nyingine huu ni uthibitisho kwamba kumbe pamoja na mbwembwe zote zile za kwamba mkubwa wao kamrejeshea gamba mwenyekiti, na kuzunguka parokia kwa parokia, kigango kwa kigango kwa kigango na hata usharika kwa usharika, chombo kinaendelea kuchota maji na karibu abiria wataanza kujitosa ili wajiokoe. Fedha zilizomwagwa Dodoma na kwenye harambee bado hazijatakasa na kununua mapenzi ya wananchi.

Katika mfumo wowote wa utawala wa nchi na chama kuna watu wanaweza kuombwa ushauri na kutoa input katika hili au lile na inawezekana kwamba (kama kuna ukweli) Membe alishauriwa ili atoe wamoni yake kutokana na weledi wake kwa jambo hilo na si vinginevyo. So far hatujaona mabadiliko ya katiba au kanuni yanayoweza kuashiria kwamba kuna namna ambayo inaandaliwa kumpendelea yeyote kati ya wale wanaowania urais (kwa bahati mbaya Membe hajatangaza kuwania. Infact amekanusha kwamba ana mpango wa kuwania).

Upotoshaji:

1. Musalia Mudavadi hakuondoka Kanu baada ya Uhuru kuteuliwa kuwa mgombea. In fact Musalia alikuwa Mgombea Mwenza wa Uhuru na hata alizawadiwa kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa muaminifu kwa Moi.
2. Raila odinga hakuwa NDP. NDP ilikufa mwezi Februari, 2002 pale New Kanu ilipozaliwa Kasarani.
3. Wilson Mukama hakuwa jiji kabla ya Keenja. Yeye amekuja baadae tena baada ya kuwa Kinondoni, Temeke na Ilala zimeshakuwa Manispaa. Hilo la kwamba Keenja alikuja kunyoosha makosa ya Mukama ni uongo na selective memory. labda kama ulikuwa jela wakati huo au ulirukwa na akili.

Ushauri:

Mimi nakushauri wewe, na wanamaliwato wenzio wa mafisadi mjitahidi kuja hapa na takwimu na hoja za maana na zenye ukweli, siyo kukurupuka tu kutokana na hofu na kuchanganyikiwa kunakotokana na kutotimia kwa malengo yenu. Kwa taarifa yako, kanuni hazitabadilishwa kwa nia ya kumpendelea Membe au yeyote yule. Zinaweza kubadilishwa kuzuia mtu asiye na sifa ya kuwa na urais, kutokana na uwezo wake wa uelewa, uadilifu wake na afya yake (sifa ambazo Lowassa zinambana).

Huko nyuma ilishaelezwa kwamba WE MAY NOT KNOW WHO WILL BE THE NEXT PRESIDENT, BUT WE KNOW FOR SURE WHO WILL NOT BE. IT IS EDWARD NGOYAI LOWASSA!

Watch this space!
 
Mbopo, naona umefura povu na hakika siyo bure.

Hapo kwenye Red Bold juu naona unamsemea kwa kukubali na papo hapo unakataa. Rejea pia bandiko langu, hakuna mahali nilitaja ni nani mlengwa wa mabadiliko ya hizo kanuni. Glad to see that you 'catching up' really fast.

Je, bado unaamini kuwa kanuni na katiba hazibadilishwi ili kupunguza nguvu za akina ENL ndani ya CCM? Rejea taarifa za Nape na Mukama kutaka kujua nani kavujisha siri za ndani au mikakati ya chama. Na vile vile kutishia kuwashitaki au kushitaki gazeti mojawapo.

Usiwe blinded na loyalty kiasi hicho. Try and step away from behind the camera, and may be you can get a better perspective of where you are standing.

Na kuhusu hivyo vipengele vitatu ulivyoviorodhesha hapo kama nukuu ya upotoshaji, ni wazi kuwa unachojaribu kufanya ni ku-split hair ili uonekane umechambua. It is still the same damn hair.

1. Ni kweli Moi alimpa Musalia u-vice wiki sita za mwisho kuelekea uchaguzi ili ampe support Uhuru, lakini ambacho husemi ni kuwa Musalia alimtolea nje Uhuru na haku-campaign naye hata mara moja pamoja na yeye Musalia kuwa VP wa Moi wakati huo. Musalia alizawadiwa na Odinga 2007 kwa 'ushujaa' huo japokuwa alisota miaka 5 bila ubunge wala nafasi yoyote kubwa.

Kwa hiyo anaweza kuwa hakuondoka KANU per se, lakini matendo yake yalimtupa Uhuru ambaye alikuwa ni Project ya Moi.

2. Raila alikuwa NDP hadi hiyo 2002, walipovunja old KANU na NDP kuunda KANU mpya. Ni upotofu unaposema kuwa Raila Odinga hakuwa NDP. Raila ndiyo kaiingiza NDP katika mseto na KANU baada ya kupewa uwaziri. NDP ilivunjwa kama trick ya Moi ku-consolidate support within KANU, na baadaye kuipeleka hiyo support yote kwa Project Uhuru.

3. Ok, inawezekana hili la Mukama kuwa jiji kabla ya Keenja labda kweli nilikuwa jela kipindi hicho (usinikumbushe maumivu hayo, bado naugulia). Lakini urahisi zaidi, jiulize Mukama alikuwa wapi kabla na hasa kipindi cha Sumaye akiwa Waziri Mkuu? Jibu ni rahisi sana, na hakuna haja ya kufoka mapovu.

Kwa taarifa zako pia, sasa suala la mabadiliko ya kanuni na katiba ya Chama linawawia ugumu na hii yote ni kutokana na kufanya mambo kienyeji bila kuwa na ushauri wa kisheria.

Muundo wa Tume ya Maadili na Nidhamu umekwama, siyo kwa utashi bali ni kwa kuwa wanashindwa kupata majina Bara na Visiwani ambayo hayataleta muelekeo wa kupendelea upande wo wote, lakini pia mtu wako abebwe. Yaliyoikwamisha Kamati ya Mwinyi, Msekwa na Kinana yanajirudia tena.

Na pia muhimu zaidi ni kuwa, mabadiliko yote yanayogusa Katiba ya Chama (siyo kanuni) ni lazima yapate baraka za Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu kabla ya kufanyiwa kazi. Japo wamejaribu kuiita hii ni 'Tume' yenye maamuzi na siyo Kamati, ili kukwepa kuigusa Katiba, suala linakuja ni wapi 'Tume' inapata nguvu ya Kikatiba ya kutoa maamuzi nje ya Kamati zinazotambulika na Katiba? Na nani anaipa 'Tume' hiyo hizo nguvu nje ya Kamati Kuu, NEC na Mkutano Mkuu? Ngoma inogile!

Labda Mpobo unaweza kujitolea kuwapa ushauri wa ki-sheria.

Hili la Lowassa kuwa Rais ni suala ambalo linamla sana "Joka La Mndimu", nadhani pengine kuliko hata Lowassa mwenyewe. Soma maandiko yangu sehemu mbali mbali katika forum hii na utagundua kuwa mimi ni mmojawapo wa wasiotaka Lowassa kuwa Raisi, kama vile ambavyo nisingetaka Membe kuwa Rais vile vile. Sifichi.

Na kama ikibidi kati ya hawa wawili Membe na Lowassa mmoja wao apite kuwa mgombea wa CCM, then ni bora mara mia iwe Lowassa kwani nitajua nasimamia wapi na ninapambana nacho kuliko iwe Membe asiye na msimamo, ambaye ni Kikwete katika sura nyingine. Tulifanya makosa hayo 2005 kwa kuaminishwa kuwa 'akiingia Ikulu atabadilika', na sasa anamaliza akiwa yule yule tuliyemjua na probably even worse kwani sasa kashika rungu sokoni.

And I am not blinded by ignorant loyalty, simply because I am only loyal to my own cause.

Subiria mrejeo wa akina Mbita, Mangula, Ameir katika siasa za ki-taifa ndani ya CCM, halafu tuongee tena. Mark my Words.
 
Salaam,

Nipo diamond jubilee kwenye uzinduzi wa album mpya ya mrs. Shusho, ila nasikitika kusema kuna baadhi ya maneno ambayo nimeyasikia mwenyewe ambayo yanaashiria kuwa mheshimiwa Membe ameanza campaign kwenye makanisa ya pentekoste! Yupo hapa na vijana wake wawili, mmoja kutoka wizarani na mwingine wa chama!
Mc, kuna maneno aliyasema wakati anamtambulisha na mimi hapo ndio nikathibitisha kuwa mambo kwisha haribika kwa hii shughuli!

I'm truly disappointed with some of my pastors for not being able to stand this none sense! I can't say much now...
 
tutashuhudia mengi sana kutoka kwa watu wa lowassa na huyu membe mpaka kufikia 2014!maana kila mmoja anavizia kusikia mwenzake karopoka nini.....analileta hapa na sisi tunalijadili
 
nasikitika kusema kuna baadhi ya maneno ambayo nimeyasikia mwenyewe ambayo yanaashiria kuwa mheshimiwa Membe ameanza campaign
...
Thread ina-hang.
Umewahi kuanziasha thread?
 
Yatafune mwenyewe haya mamifupa yako makavu I will be back later
 
Salaam,

Nipo diamond jubilee kwenye uzinduzi wa album mpya ya mrs. Shusho, ila nasikitika kusema kuna baadhi ya maneno ambayo nimeyasikia mwenyewe ambayo yanaashiria kuwa mheshimiwa Membe ameanza campaign kwenye makanisa ya pentekoste! Yupo hapa na vijana wake wawili, mmoja kutoka wizarani na mwingine wa chama!
Mc, kuna maneno aliyasema wakati anamtambulisha na mimi hapo ndio nikathibitisha kuwa mambo kwisha haribika kwa hii shughuli!

I'm truly disappointed with some of my pastors for not being able to stand this none sense! I can't say much now...
Funguka mkuu maneno gani hayo aliyoyasema?
 
Naungana na wenzangu kuomba ufafanuzi, maneno hayo ambayo huyataji kayasema Membe au MC? Kama ni MC sasa Pastors wamefanya nini au kosa gani? Lakini umesema shughuli yenyewe ilikuwa ni utambulisho wa album, ulitaka mgeni rasmi awe nani? Na vijana wawili wa Wizarani na Chama wanamaanisha nini kisiasa au wana uhusiano gani na kuanza kwa kampeni? Vijana hao walikuwa wanagawa posters na mabango au? Pole sana kwa kuji-dissapoint.
 
Je viongozi wa kisiasa hawaruhusiwi kuingia nyumba za ibada na swala kama makanisani na misikitini? kama ndivyo, Nani atapona labda tuwe na viongozi wasio na dini.....wapagani. kimsingi, ni heri kuwa na viongozi wa kisiasa wanajitangaza wawapo kwenye ibada na harambee kuliko wanaokwenda kimya kimya na agenda zao za siri.
 
we bazazi hebu tuwekee basi hayo maneno hapa! hatuwezi kuanza kutoa lawama kwa huyo mende bila kuona alichokisema kwani inawezekana kabisa kuwa wewe ndo umemuelewa vibaya.Ingawa mimi binafsi simfagilii huyu mwanasiasa mnafki nachelea kushusha madongo kwa vile sijaona alichosema.
 
Back
Top Bottom