Mkuu Kipokola,
1. Kwa vile JK alikuwa foreign, ndipo akawa rais wa JMT, na Ben aliwahi pia kuwa foreign naye akawa rais wa JMT, then its automatically, kwenye CCM, kwa mujibu wa the current trend, aliye foreign ndie anepaswa kuwa next!, hivyo Membe is very right to think he is the one and only derverving to be the next president!. Zile hoja za mpaka akioteshwa, au hizi za kusikilizia wananchi ambao tayari wameisha pangwa na chochote kitu wameshikishwa!, zote ni danganya toto!.
2. Hili la haiba ya urais ndani ya CCM sio issue!, kumbuka JK aligombea na kina nani, linganisha haiba zao, na wezo zao!, lakini aliyepita ni JK!, jikumbushe alipitaje, ngazi gani alitumia, dodoki gani aliogea, pepeo gani lilitumika kumpepea, mbeleko gani iliyotumika kumbebea?, kama hayo yaliwezekana kwa JK, why not kwa Membe?!.
3. CCM hawatafuti mgombea mwenye uwezo, ability, bali anayekubalika!, anayetazamika na anayechagulika ili kuwaletea ushindi!, akishashinda, atajengewa uwezo kwa kupewa timu ya able people kumsaidia!. Swali linabaki jee Membe, ndiye anayekubalika zaidi?. ndiye anayetazamika zaidi?, ndiye anayechagulika zaidi?. If yes, then mgombea wa CCM kwa 2015 ni Membe!, if not, then ni mtu huyo mwenye hivyo vitu vitatu ndiye atakayekuwa mgombea wa CCM na ndiye atakayetua Ikulu ya Magogoni, mpende msipende!.
4. Membe pia anayo turufu nyingine muhimu sana kwenye urais wa Tanzania, hii ni turufu ya "Udin!i". Tukubali tukatae, udini una play a very big role katika determinant ya who is the next president!. Japo Tanzania ni secular state, serikali ndio haina dini, ila watu wake wana dini zao!. Rais hachaguliwi na serikali isodini, bali huchaguliwa na watu wenye dini zao!. Dini kubwa ni Wakristo na Waislamu, hivyo tutake tusitake, tukubali tukatae, rais wa 2015 ni au Mkiristu, au Muislamu!.
Kwa vile urais pia unapatikana kwa kupokezana kwa zamu, Nyerere alikuwa Mkristu, akafuatiwa na Mwinyi, Muislamu, then Ben, Mkiristu, akaja JK Muislamu, hivyo 2015 ni zamu ya Mkristo!. Kwa vile Membe ni Mkisto, hivyo safari hii ni halali yake kabisa!.
Kama ilivyo kanuni fulani ya siri ambayo haijaandikwa popote kuwa kuna makabila fulani kamwe hawawezi kupewa urais wa Tanzania, then pia kuna kanuni ya siri, kuwa rais wa Tanzania, sio tuu lazima awe ni Mkiristu, bali lazima awe ni Mkristu, Mkatoliki!. Nyerere alikuwa Mkatoliki, Ben pia alikuwa Mkatoliki, hivyo rais wa 2015 naye pia lazima awe Mkatoliki!.
Ndugu zetu Wakristu wa madhehebu mengine, samahanini sana, msinilaumu mimi kwa hili, sio mimi ndiye niliyeamua kuwa rais wa Tanzania ni lazima awe Mkatoliki, bali hii ndio hali halisi, kwa sababu Katoliki ndilo kanisa kubwa Takatifu la Mitume, linamiliki mpaka nchi yake ile ya Vatican!. Sasa kwa vile MEMBE naye ni Mkatoliki, ameishamuomba Magufuli ambaye pia ni Mkatoliki asitie mguu, na pia ndiye anayehakikisha yule Mkatoliki tishio aliyeko opposition "is done!" before 2015 to clear the way!. Kama hivi ndivyo mambo yalivyo?!, ndivyo yalivyo! why not?!.
Nikiwa bungeni mwaka jana, wakati Membe akiwasilisha bajeti yake, niliwashuhudia "the brais behind" the "winning coalition" behind JK ile 2005 ikimzunguka Membe kuja kumpa support!,
Japo kwa maoni yangu binafsi mimi kama Pasco wa jf, Membe hauziki hata kwa dawa!, ila kwa vile yule mgombea wangu, amekubali kubaki kuwa ni "sauti iliyo nyika tuu, ikiyanyoosha mapito ya yule yuajaye "the chosen one!", na kwa vile Watanzania siku zote huwa tunachagua kwa kufuata tuu mazoea tuu kwa vile hatujui tunataka nini, hivyo yoyote atakayepitishwa na CCM, "the chosen one", ndiye rais wetu 2015, kama "the chosen one" ni Membe, then Membe ndiye rais wetu wa 2015!.
Pasco.