Membe kugombea urais mwaka 2015 iwapo...

Membe kugombea urais mwaka 2015 iwapo...

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo.

Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini hapa, baada ya kumalizika kwa kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani hapa, lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic.

Membe aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema ingawa muda wa kufanya uamuzi kuhusu mwaka 2015 bado na chama hakijatoa utaratibu, lakini atasubiri ushauri wa Watanzania.

"Naomba kurudia, mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea urais ...ila nasema hivi natarajia sana ushauri wa Watanzania.

"Iwapo Watanzania wataniona nafaa na kunitaka nigombee, nitapima mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka nigombee, basi nitachukua fomu na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu," alisema Waziri Membe.

Maadili ya wabunge Membe alisema hali ya kisiasa nchini inakwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza mambo bila kujitathmini. Alisema mbaya zaidi hata baadhi ya wabunge wa CCM, nao wamekuwa si msaada kwa chama, kutokana na kuzungumza mambo dhidi ya Serikali na chama.

Membe alisema amepata kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 15 tangu Bunge la Spika Pius Msekwa, hadi sasa chini ya Spika Anne Makinda, ila anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo bila kuzingatia kanuni za Bunge, jambo ambalo ni hatari zaidi.

Alisema Bunge linalotazamwa na Watanzania, ni lazima liwe la mfano wa kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza, lakini sasa ndio maana Bunge linaendelea kupoteza mwelekeo.

"Bunge linapoteza mwelekeo kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wanaofikiri wakisema ovyo na kutumia lugha kali katika kuzungumza, wao ndio wanaonekana ni wabunge bora kitu ambacho hakipo.

"Mbunge ni pamoja na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura wako bungeni," alisema.

Membe alisema kutotumia busara katika kujadili mambo bungeni, si ubunge mzuri na bora watambue wazi kuwa wananchi wao wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kama hicho wanachokifanya, ni kuwakilisha wananchi au kujiwakilisha.

"Nawaomba wabunge wawe wazalendo, wawakilishe wananchi waliowatuma badala ya kuligeuza Bunge kama sehemu ya kuonesha ujuzi wa kuzungumza ovyo.

"Nasema tuogope wananchi, mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila mbunge na kwa sasa wananchi wanasikiliza na kutazama ila muda ukifika watakuacha," alisema.

Alisema wabunge wengi ni vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora, ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika na kuangalia amefanya nini katika jimbo lake na watampima kwa kazi aliyofanya na si ukali bungeni.

Alisifu baadhi ya wabunge wa CCM, kwamba wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika majimbo yao, kwa chama na Serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete, kwa kusukuma mbele maendeleo ya Taifa, ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonesha uwezo wa kusema ovyo.

CHANZO: HabariLeo
 
Membe kugombea urais mwaka 2015: WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo. Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini hapa,baada ya kumalizi http://tinyurl.com/d52727r

Mpe pole yake, RAIS HAWEZI KUTOKA KUSINI TENA
 
Du kumbe kuna hadi wa shift za usiku, nilikuwa sijui, sa wa shift ya usiku kazi mnafanyia wapi, lumumba au nyumbani?
 
Membe kugombea urais mwaka 2015: WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo. Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini hapa,baada ya kumalizi http://tinyurl.com/d52727r


Oh hapo Sasa PRINCE atapata Uwaziri; Mama Salma pia Uwaziri...Itakuwa kama VILE utawala wa JOMO Kenyatta -- Mtoto wake Mmoja alikuwa MEYA wa NAIROBI; Mwingine UN Ambassador NEW YORK; Mwingine Naibu Waziri; Mwingine anaendesha Biashara ya Mama yake...

We Really need a New Constitution as SOON as POSSIBLE... sijui kuwa itakuwa leaning one side kwasababu Malipo ni Mazuri kweli... Kwasababu Fatma Said Ally watoto wake walio Nje walikuwa wanasota sasa HIVI UH LALA... Magari Mapya... Kuhamia Nyumba Safi (Owning)... Kwahiyo Hadi Prof. Baregu atakuwa amelegegalega...
 
Mkuu hujasikia kuwa mimi ndiye nitakayepitishwa kugombea Uraisi? Muulize vizuri Membe analijua hilo.
 
Anajifanya anaomba maamuzi ya wananchi wakati alishajipitisha mwenyewe.
 
Membe kugombea urais mwaka 2015: WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo. Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini hapa,baada ya kumalizi
http://tinyurl.com/d52727r

Sina Shaka Juu ya Bernard Bembe huyu jamaa ni Jembe na ndio Suluhu kwa watanzania Anakila Haiba ya kuwa Rais wa 2015 in Tanzania Uchungu wake juu ya Watazania Uelewa wa Siasa za Nje (Kimataifa) pia ni mchapa kazi niombe tu wananchi wa Tanzania tumuunge mkono PResdarrrrr tusijalishe vyama nia yake ya kishujaaa uhakika anaweza!Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki nia ya Bernad Membe 2015 Presdent of Tanzania
 
Hakuna dhambi kwa Mhe. Membe kugombea Urais kama ilivyo kwako pia. Ruksa kutangaza nia yako ili wananchi waweze kuamua nani anafaa. Sasa wewe unataka agombee nani?
 
Sina Shaka Juu ya Bernard Bembe huyu jamaa ni Jembe na ndio Suluhu kwa watanzania Anakila Haiba ya kuwa Rais wa 2015 in Tanzania Uchungu wake juu ya Watazania Uelewa wa Siasa za Nje (Kimataifa) pia ni mchapa kazi niombe tu wananchi wa Tanzania tumuunge mkono PResdarrrrr tusijalishe vyama nia yake ya kishujaaa uhakika anaweza!Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki nia ya Bernad Membe 2015 Presdent of Tanzania
Nadhani hii ndiyo itakuwa ID ya Riz1
 
....Kwani ameshaoteshwa?au sasa anasubiri wananchi (familia ya kwanza) imwambie kuwa anafaa?
 
ccm wakimsimamisha Membe chadema hakuna haja ya kampeni ni kujiandaa kuingia ikulu, kuapishwa na kuanza kushugulikia matatizo ya wananchi bila kusahau kuwashugulikia mafisadi na majangili!
 
Back
Top Bottom